Wednesday, November 15, 2017

SIRI ZA MAISHA: JIFUNZE UTOFAUTI KUHUSU KUOANA NA KUFUNGA NDOA


Kuoana ni ile hali ya kufiti,kuwa kwenye kipimo sawa kuendana na hitaji lako au hitaji la kitu ikiwemo hisia,mitazamo,tabia,nk

Kuna tofauti kubwa kati ya KUOANA na KUFUNGA NDOA.

Watu wengi hufunga ndoa wakidhani wameoana, kuoana ni hali,kufunga ndoa ni kitendo,ndio maana huwa kuna siku maalum ya kufungishana ndoa lakini hakuna siku maalum ya KUOANA.

KUOANA maana yake ni MATCHING,KUENDANA

Ni rahisi kwa watu wanaooana kufunga ndoa na kudumu kuliko wanaofunga tu ndoa pasipo kumatch-kuoana.Ni rahisi kufunga ndoa na mtu yeyote lakini ni vigumu KUOANA NA MTU YEYOTE.

Kuoana ni sawa na neno saresare,kama wewe unavaa kiatu namba 40 na kinakutosha basi ujue mguu wako umeoana na kiatu ulichonunua.

Katika kuchanganya maana ya KUOANA NA KUFUNGA ndoa wapo waliojikuta wamefunga ndoa kwa bahati mbaya.Pengine tunaweza kujiuliza,je nitajuaje kama NAOANA NAYE ILI NIFUNGE NAYE NDOA?AU NIREKEBISHE NDOA YANGU?

Ungana nami katika SEMINA ZA SIRI ZA MAISHA