Thursday, November 16, 2017

VITU 7 VYA KUJIFUNZA MSICHANA KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA

Wakati unapofika, kunakuwa na msukumo ambao humfanya msichana kutaka kuolewa, inawezekana ni umri , au ni matakwa ya mwili,  inabidi msichana atulie hapo  kabla hajaanza kutafuta mtu wa kuishi nae. sio tu mwanaume anaetafuta mtu wa kumuoa , na msichana nae pia hutafuta mtu wa kuolewa nae, labda utajiuliza kivipi.
Kwa sababu huendi tu kuolewa na mtu yeyote ni lazima kuwe na sifa uzitakazo.Sifa 23 za kijana anaestahili kuwa na wewe binti. hapa kuna mambo mengi , maana kuna wasichana ambao hujitangaza kuwa wapo tayari kuolewa , wako single n.k. unatakiwa ujifunze kwanza, na utambue kuwa kuna mtu  utakuwa nae kwenye mahusiano , na kama wewe ulishawahi kuwa kwenye mahusiano kabla. lazima utambue kuwa ipo nafasi kubwa ya kuingia tena kwenye mahusiano mengine.
Kama unahitaji mahusiano ya kudumu , basi jifunze hivi vitu vifuatavyo kabla ya kuingia huko.
1.jiulize, shida yako ni nini?
Business woman thinking yes or on in speech bubble
Business woman thinking yes or on in speech bubble
Unatakiwa kutuiza akili yako na  uwe na mtazamo sahihi , kwa sababu sio kuingia ndani ya mahusiano na mtu, na kama unataka mahusiano yawe ya kudumu, lazima ujifunze kwanza maana humo kuna zaidi ya kile unachotafuta wewe, lazima upate mtu anaekuthamini na wewe umthamini.
shida yako ni nini  katika maisha na katika mahusiano? jitahidi kujua hivi vitu, utaepuka kumpenda mtu ambae sio  wa mtazamo wako, na sio chaguo lako.
2.Jinsi ya kuwa huru.1
Jifunze kuwa huru kwanza kabla ya kuingia kwenye ndoa, usitake mwanaume akukimbize katika maisha yako. kwa maana kama huwezi kujitunza , na kujisimamia wewe mwenyewe , utawezaje kuja kujisimamia mwenyewe na kumsimamia mumeo. au endapo utakuwa ni single  huwezi  kujiheshimu , utakuja kujiheshimu vipi ukiwa kwenye ndoa.
Jifunze kutokuwa tegemezi mapema kabla ya kuolewa, usije ukawa mzigo , na ukaanzisha matatizo mengine  ambayo yana majibu  wazi.
3.Jifunze jinsi ya kuwa na furaha. bigstock-Young-Woman-Thinking-10556330-1170x585
Jifunze kuwa mtu wa furaha , furahia maisha yako kila siku iitwapo leo, uwe makini na yule mwenye hia , anayetafuta kuleta   urahisi wa kukushambulia  ili ukose furaha. jitahidi kushinda hivyo vitu. hapo sasa hata ukipata huyo mtu wa maisha yako , utakuwa ni mtu wa furaha siku zote , maana hutakubali mwenye hila akupotezee furaha yako.
4.hivyo huhitaji mtu.
kumpata mtu ambae ndio nusu yako , ya kwamba ni kweli huyo ndiye, inahitajika uwe ni mtu mtulivu sana .Naamini kuwa mahusiano  yasingekuwa ni kiungo muhimu , ambacho  kinakamilisha furaha ya maisha ya mtu, lakini basi isiwe ndio chombo cha kukufanya wewe upate furaha, nielewe vizuri hapa. huhitaji kusubiri mtu kwa ajili ya furaha yako.  mweke mungu  awe wa kwanza na mengine yafuate.
5.Jinsi ya kuwa wewe.TNMCoupleDateRingEngage
rel-09-thinking-about-marriage
Tumefanya wote hayo,kujaribu kuwa  pekee,  kufikiri kuwa  tunahitaji mtu wa  kutufanya ili kuwa wewe ndiye. lakini huhitaji  kubadilishwa na mtu au kuchukua mawazo ya mtu mwingine anavyotaka uwe, hapana. jifunze tu kuwa wewe. unahitaji kupendwa jinsi ulivyo. ndoa nzuri ni ile mtu kukupenda jinsi ulivyo, na kukuelewa ni aina gani ya mtu alienae.
6.Una nini cha kutoa.
Kuwa ndani ya ndoa sio tu kupata mtu sahihi kwako , je wewe ni sahihi?, lazima wewe nawe uwe na kitu cha kutoa, isiwe ni upande mmoja tu. jipime kama ni  muda sahihi  na mazingira sahihi au ni sehemu sahihi? au bado hujakamiika , unahitaji kwanza kukaa single ili ujiandae.
7.Ni wapi ulipokosea kabla.

inabidi ujiulize ni wapi ulikokosea ni wapi ulikojikwaa na kuanguka kwa mara ile ya kwanza ulipoingia kwenye mahusiano  ya kawaida. kutokana na hayo makosa ya kawaida ulioyafanya ili usirudie makosa yale yale, lazima uwe na mtazamo tofauti.  jifahamu kwanza wewe kabla hujaanza kumfahamu mtu mwingine. utapata furaha na mafanikio katika maisha yako.
Angalia jinsi gani unajipenda na uangalie tabia zako zikioje. ndipo utapata mtu sahihi .