Sunday, November 12, 2017

USIKATE TAMAA, NI DHAMBI.

Inawezekana ukawa umesoma sana na ukawa unamiliki vyeti mbalimbali vya kitaaluma lakini mpaka sasa maisha yako bado unaona hayaendi sawa sawa kama unavyotaka au inawezekana pia ukawa umebarikiwa akili na maarifa ya kutambua mengi lakini mpaka sasa huna lolote unaloona ni faida kwako zaidi ya maisha kuendelea kuwa magumu kwa upande wako na huku wengine wakipanda juu na kukuacha ukiwashangaa kana kwamba hukuwa nao hapo mwanzo au kana kwamba wao ndio wenye akili nyingi kukuzidi.

Usikate tamaa wala kujiona huwezi. Kitu cha muhimu hapa ni kujitambua kwanza na kufahamu nia hasa ya Mwenyezi Mungu kukuleta hapa duniani. Binadamu ulipoumbwa na Mwenyezi Mungu na ukaletwa hapa duniani hukuletwa kuja kuteseka au kuja kuwa msindikizaji wa wengine ambao waliumbwa kama wewe ulivyoumbwa.Uliletwa kwa makusudi maalum na kila dakika unayoishi hapa duniani kumbuka hairudi tena na ikishaenda imeenda.

Kwa hiyo unapokuwa unataka kukata tamaa kwa kushindwa kutimiza lengo Fulani kwenye maisha au kwa kufeli shule,kufeli biashara, kufeli kwenye mahusiano/mapenzi, kufeli maisha, kufeli kupata kazi, kufeli kwenye kilimo au hata kufeli kiimani, unapaswa kwanza kutambua lengo la Mungu kukuleta hapa duniani.Hakuna sehemu yoyote iliyoandikwa kuwa umeletwa duniani kuja kufeli.hakuna sehemu yoyote iliyoandikwa kuwa umeletwa duniani kuja kuangalia wengine wakisonga mbele na wewe ukirudi nyuma.

Mungu Ni Mwema Siku Zote, Humpa Kila Mtu Sawasawa Na Mapenzi Yake, Ukishindwa Sehemu Moja Ya Maisha Jaribu Sehemu Nyingine Utaweza Tu, Hakuna Aliyeumbwa Kukosa, Unaweza Tena Sana, cha kufanya ni kujiamini tu.Ukijiamini kama unaweza basi hakuna kitakachokuwa kigumu kwako, usijipe moyo wa kushindwa hata siku moja. Ukikata tamaa tu kila siku utakuwa mtu wa kulia na kujuta na mafanikio kwako yatakuwa magumu sana kupatikana.

Na Hata hayo Matatizo Uliyonayo Ni Ya Muda tU, Mwenyezi Mungu Kakuumba Kwa Makusudi Yake, Jipe Moyo Utayashinda, Yana Mwisho, Unapopata Majaribu Usihuzunike Wala Kukata Tamaa,Mwombe Mungu Atakusaidia huku ukitafakari njia sahihi za kutatua na kama ukishindwa kupata utatuzi wewe mwenyewe usione aibu kuomba msaada kwa wengine.

Kuwa Kilema, Yatima, Mjane, Mfungwa, Mkimbizi, Mgonjwa, Masikini, Na Kadhalika, Kusikufanye Uishi Kwa Majonzi, Unyanyasike Na Kukata Tamaa, Bado Unavuta Pumzi , Inamaanisha Bado Unaweza Kubadilisha Huzuni Kuwa Furaha, Mwite Mwenyezi Mungu Akuongoze Kuanzia Sasa, Hautajuta Wala Kujiona Huwezi. Wangapi ni vilema na wana mafanikio kuliko wazima?, wangapi waliachiwa familia na wake/waume zao baada ya kufariki au kwa kukimbia majukumu lakini leo hii wana mafanikio makubwa tu??! Tunachojifunza hapa ni Kutokata Tamaa na Kujiamini.

Na kitu kingine cha muhimu kwenye maisha ni uwezo wa kufanya maamuzi bila kuyumba. Unapoamua Kufanya Maamuzi Na Ukawa Na Uhakika Kama Maamuzi Hayo Ni Sahihi Basi Hutakiwi Kuogopa, Maisha Ni Yako Na Hutakiwi Kuwa Muoga, Usiogope Majirani Na Wengine Watasema Nini, Haohao Wanaokusifia Leo Ndio Haohao Watakaokucheka Kesho Ukianguka, Be Positive With Your Feelingz/Jiamini. Na Usitegemee Sana Nguvu Zao Kufanikisha Malengo Yako, Wengi Wao Wapo Nawe Mdomoni Tu Lakini Moyoni Wapo Sehemu Nyingine Kabisa, Pigana Kwa Nguvu Zako Mwenyewe Kama Unataka Mafanikio Yawe Upande Wako, Usiamini Mtu Isipokuwa Mungu Pekee.
Kitu cha mwisho kukiangalia kwa wewe unayeona maisha hayakuendei poa kwa sasa ni kuangalia aina ya marafiki ulionao. Ukiona Umezungukwa Na Marafiki Na Ndugu Wengi Na Wenye Uwezo Wa Kukusaidia Kutoka Kimaisha Lakini Kila Siku Maisha Yako Yakawa Yanashuka Badala Ya Kupanda…Basi Huna Budi Kutazama Upande Mwingine, Urafiki Ni Kusaidiana Na Si Kufurahia Pale Unapoanguka Ili Kila Siku Uwatukuze Wao Tu, Haina Maana Kujuana Na Fulani Halafu  Hupati Faida Yoyote.

Kufanikiwa kumewekwa kwa kila mtu hapa duniani bila kujali umri au dini. Usiangalie una umri gani sasa na usiangalie umetokea familia gani wala mazingira ya sehemu ulipo wala elimu uliyonayo, unaweza kufanikiwa kama utaambatana na waliofanikiwa na kuachana na maneno ya waliokata tamaa za maisha. Usiwape Watu nafasi wakucheke, Wape Nafasi Watu wajifunze Kutoka Kwako.Comments