Sunday, November 12, 2017

Kubali ukweli Huu: “Tunakosea mengi wakati tunaanguka katika penzi(Fall in Love)”

Hadithi ya penzi yetu tulio wengi hua inaanza hivi: Mwanaume anavutiwa na mwanamke mmoja mahali fulani(Labda kwenye party, Mgahawani, Ama sokoni n.k). Kisha anamfuata na kumtongoza na muda mchache wanakua wapenzi.
Unadhani huu ni mzaha ama story za kutunga? mambo haya yanatokea sana tuu katika jamii zetu. Ila tukubali tuu ukweli ni kwamba wengi wetu tunakosea mambo mengi wakati tunaangukia katika Penzi(Fall in Love)..
Kama inavyofahamika kwamba hakuna mtu anayetufundisha ni kwa namna gani tunaanguka katika penzi, sio shuleni ama wazazi wetu. Ila Zile movie za mapenzi ndio chanzo kikuu cha kufahamu mambo haya. Tunajikuta tuu kwamba ni Rahisi mtu kumpenda mtu kwa mara ya kwanza na kuangukia katika penzi pasipo kumfahamu mtu yule kwa Kina(Unabisha?).
Lakini kama zilivyo namba ama misamiati mbali mbali, tunapaswa kujifunza na kuyafahamu mambo haya kiundani, Kufahamu zaidi misingi ya mambo haya. Tungekua tunalifahamu hili kiundani, tusingejikuta tunashindwa katika Mahusiano yetu kila siku.
Pengine Utakua umwekwisha liona jambo hili, kwamba unaanguka katika penzi na mtu fulani, mambo yenu yanaenda poa kabisa, mnafanya mambo mapya kila siku Lakini ghafla ukagundua kwamba kuna kitu kimekosekana na hukifahamu ni kitu gani na unahisi kabisa kwamba huridhishwi na penzi hilo.
Ni kwa sababu ulizama katika penzi pasipo kufahamu mambo haya yafuatayo:-

Kutumia muda mwingi kwa pamoja.

Haimaanishi kwamba mtapaswa kukaa kwa muda mrefu kwa pamoja ndipo muanze mahusiano yenu, Hapana. Unapaswa kumtizama mtu yule kwa muda na kumchunguza kuona kama mnaendana na ni yule umtakaye.
Je anawahudumia vipi watu wa familia yake na wale wote wamzungukao, Ni kwa namna gani huwachkulia watu walio chini yake? Je anakujali wewe kama anavyjijali yeye mwenyewe kwa muda wote?
Kwa matendo hayo madogo unaweza kusema mengi. Ila cha msingi angalia ni kwa namna gani anakupa uangalifu wa kipekee na namna anavyo ku-treat wewe na jamaa zake/zako.

Kuuliza maswali yenye maana.

Usimuulize maswali mepesi na ya kwaida mfano ‘Unapendelea chakula gani?’. Maswali haya ni mazuri pia ila kumbuka una maswali muhimu mno kumuuliza.
Maswali hayo ni kama ‘Unapendelea kuishi wapi wakati wa likizo/mapumziko yako? Swali hili nalo linaonekana kuwa la kawaida sana si ndio? HAPANA, swali hili litakupa jibu na kufahamu thamani ya Mtu yule na kumfahamu ni mtu wa aina gani.
Maswali mengine yatakayokufahisha zaidi mtu yule ni wa aina gani ni kama
  1. Ni jambo gani unalojutia katika maisha yako?
  2. Kama ukipata nafasi yakurudi nyuma katika maisha yako, utachagua Umri gani na kwa nini
Majibu ya maswali hayo hapo juu nina uhakika utapata kumtambua kwa undani mtu huyo. Kama ni mla bata ama ni mtu mwenye Focus katika maisha yake.