Monday, November 13, 2017

SANDUKU LA HUDUMA YA KWANZA Kwa Hisia zako ( First Aid Kit)

Huduma ya Kwanza kwa hisia zako inaweza kuonekana kama kitu kigeni kutokana na Mazoea ya kuwa na huduma ya Kwanza KIMWILI kuliko KIHISIA….lakini tulio wengi hupata Matatizo ya kihisia kuliko ya kimwili au vyote kwa pamoja,..mfano Msongo wa Mawazo, kushuka moyo n.k ..na hii ni kwa sababu ya Changamoto tunazokumbana nazo katika maisha na matatizo mbali mbali.
Jitengenezee Sanduku la Huduma ya kwanza la Hisia zako …matatizo ya kihisia hayatibiwi kwa Glucose wala Plasta….Sanduku hili litakusaidia ktk kutokuchukua maamuzi mabovu unapopatwa na Changamoto za Maisha…huwezi kuwaza kukata tamaa wala kufikiria kujiua n.k..kwa sababu sanduku hili ndilo litakuwa Rafiki yako wa kwanza.
Vitu vinavyokamilisha Huduma ya kwanza kwa Hisia zako ðŸ‘‡
1. Namba za simu za watu unaoweza kuzungumza nao unaposhukwa Moyo.
2. Misemo ya kutia Nguvu na Makala zinazotia Moyo na kufurahisha.
3. Orodha ya maandiko yanayofariji aidha kutoka kwenye vitabu vya Mungu.
4. Nyimbo unazipendelea sana kusikiliza.
5. Vitu vinavyokukumbusha kuhusu watu wanaokupenda.
6. Diary au daftari uliloandika mambo mazuri uliyowahi kufurahia.
7. Tembelea Blogs,websites au pages ambazo hukupatia elimu na tabasamu.
Pio Pius…..2017.