Thursday, November 16, 2017

SIRI AMBAZO HUTAKIWI KUMWAMBIA MWENZI WAKO


Namini katika mambo ambayo hutakiwi kuyasema, si kila kitu kinatakiwa kuwa wazi , mambo mengine ni bora afahamu Mungu tu

Pamoja na kwamba kunahitajika kuwepo ukweli halisi bila ya kificho kwenye mahusiano yako.

Kuna muda ambao hutakiwi kuwashirikisha watu mambo yote hata mwenza wako. Ukweli, ukiwashirikisha , si tu utakumbwa na ugonjwa wa moyo, lakini pia itakuwa ni chanzo cha madhara mabaya. Madhara hayo hayatakiwi kabisa kuwepo.

Hapa nitakueleza jinsi ambavyo uwazi unavyoleta madhara zaidi ya kuleta mazuri.

1.Kitu chochote ambacho familia yako au marafiki wamewahi kusema kuhusu mwenza wako.
Ni bora kama hutasema hata kidogo mabaya ya vitendo vyao ambavyo wanavyo au walikuwa navyo. Ni rahisi kupata maumivu ya mawazo hayo na ni ngumu kuyaondoa. Mwenza wako atakuwa anayakumbuka kila mara kuwa yalisemwa, itakuwa ni vithibitisho kuwa familia yako na marafiki walisema na hawampendi na inawezekana hawakumpenda toka mwanzo.

2.Shutuma Za Familia Yake

Wanaweza kupata kitu chochote ambacho hawakipendi, lakini hawangependa wewe uwaonyeshee kidole na kuwasema . wenza hupata ulinzi wanapokuwa wanafahamu jinsi ya kukabiliana na haya matatizo, na huishia katika kushikamana pamoja bila ya kuonyesha madhaifu ya upande fulani.

3.Furaha Uliopata Kwenye Kujamiiana Ukiwa Na Mpenzi Mwingine Kabla Yake.

Watu wengi huwa hawana uhakika katika maisha yao ya mapenzi hasa katika upande wa kujamiiana, hupenda kusikia kuwa wako vizuri katika hilo, hasa kwa wanaume. Hakuna haja ya kuanza kumwambia kuwa ulikuwa unapata furaha zaidi ya mahali hapo. Utaondoa usalama wake. Na sio kumfanya akose uhakika, lakini pia atakuwa anajaribu kutafuta picha hio uliosimulia. Na ukumbuke kuwa hakuna kitu kibaya kama hicho. Kwa sababu atashindwa kuwajibika impasavyo kwa kuhofia kuwa hutafurahia.

4.Hamu Yao Ya kuwa Na Mafanikio Ya Kiuchumi

Unasaidia malengo yao ya kufikia nia yao na kujaribu kuifanya biashara iwe nzuri., lakini kuna siku ungetamani wafanikiwe, wakue na kupata pesa nzuri kwa ajili ya maisha yenu. Lakini kuwa makini, mawazo yako yanaweza yasiwe na usaidizi na yakawa ni ya kuumiza upande wa mwenza wako. Kwa sababu naye anatamani kuona hivyo lakini hasogei. Labda kama hicho kitu amekizoea kutoka kule kwa wazazi wake alikuwa akikifanya na hana wasiwasi nacho.

5.Uwezo Walionao Marafiki Zake Kwenye Ngono.

Hii haiwezi kwisha kwa usalama, kutakuwa na ugomvi wa aina yake, kukosa uhakika na wivu pamoja na kuwa na hisia mbaya kwa marafiki zake. Utakuwa unachunguzwa kila unapokuwepo , mwingiliano wa watu wako utazuiliwa kutoka kukutana na marafiki, na hata kuhisiwa kwa tabia ambazo hauna.
Pamoja na kwamba hakuwa na tabia ya kukufuatilia, utamwanzishia tabia ya kukufuatilia kila mahali. Usifungulie huo mlango. Na uwe makini katika kutoa maneno hayo. Ni ya hatari. Utabomoa barabara.
Mahusiano yana changamoto ya kutosha bila ya kuongeza misongo isio kuwa na umuhimu ambayo itamwingia mtu akilini moja kwa moja. Wakati mwingine , meza hayo unayosikia na uyaharibu yasikae akilini mwako, usiache yastawi ndani mwako, palilia kila siku kubaki mawazo safi tu. Huo ndio uchaguzi mzuri.