“Usione sooo sema nae, mwambie ukweli.
Leo nmepanda hapa MTOKAMBALI nikiwa na swala moja tuu ambalo mara nyingi hunitawala katika fikra zangu na hata kuyaona kwa macho yangu na jambo hilo ni “Uoga katika kumwambia mtu Ukweli ama la Moyoni”
Kuna wale vijana wenzangu mtaani huwa naonaga wakiitwa Madomo zege na Wengine niliwahi kusikia wakiitwa nyoka Kibisa(Yaani hawana sumu), nashindwa kutambua hali hii maana napatwa na maswali mengi kichwani juu ya jambo hili yakwamba Je ni uoga wa kumwambia mtu? je ni Aibu ya kumwambia mtu kitu? ama je ni nini hasa kinachomfanya mtu kuwa katika hali hiyo?(Embu tuongee kidogo hapa)
Leo acha nikuambie ndugu yangu…
Nafahumu kwamba moyo wa mtu siyo wa chuma bali ni nyama, na kila mwanadamu ana haki ya kupendwa na hata kupenda pia.. ila linapo kuja swala la Mapenzi moyo huo huo hujeuka sega la asali ama kujeuka chungu kama shubiri na ndivyo mapenzi yalivyo.
Ila kwa kuwa tumeumbiwa kupenda, hatupaswi kuunyima moyo kile unacho stahili, sasa je ni kwa nini uogope kuuupatia moyo kile unacho kipenda? Je hufahamu kwamba faraja na furaha huja kutoka moyoni?
Kuna wale vijana wenzangu ambao humpenda mtu kwa dhati kabisa na hata kudhamiria kuwa na mtu fulani katika maisha yake ila anaogopa kumwambia mtu yule. Na hii nimeiona hasa kwa Vijana wa kiume, mara nyingi wamekuwa wakitamani kuwa na wachumba wazuri wenye hadhi flani ila wamekuwa wakijikuta katika wakati mgumu pale wanapo taka kufunguka.
Utakuta mtu ana maswali meengi katika moyo wake kwamba je atanionaje? je si atanitukana? je si atanikataaa?
Kakuambia nani kwamba yule unaye mtaka takufanyia hayo unayowaza? Ndiyo yawezekana ukaambiwa hayo maana kuna watu wengine huwa na hulka ya kujiskia kwamba wao ni bora zaidi ila kabla hujafikia huko na wewe jiulize je ukimwambia na akakubali utajiskiaje?(Aibu ama furaha?)
Na ndiyo maana leo hii nakupa mambo kadhaa ya kufanya ili kuondokana na hiyo hali na mwishoni kupata kile ulicho kitamani katika maisha yako.