Yawezekana umekua ukijishtukia ukiwa katika hali ya kusahau mambo kila mara ama kupoteza kumbukumbu na muda mwingi umekua ukitafuta suluhisho sahihi juu ya tatizo hilo.
Jambo zuri ni kwamba kila mmoja anaweza kuongeza uwezo wake wa kuhifadhi kumbukumbu katika ubongo wake kwa kufuata zile njia maalumu na kufanikiwa na hakuna haja ya Kubadili mifumo yetu ya maisha ili kuondokana na tatizo hilo.
Zifuatazo ni njia sita ambazo zitakusaidia kuongeza uwezo wa Ubongo wako kuhifadhi kumbu kumbu.
1.Hakikisha Unapata Usingizi wa Kutosha.
Mara nyingi watu wenye pilika nyingi(Busy) hukosa hata muda wa kulala jambo ambalo hupelekea uwezo wao wa kuhifadhi kumbukumbu kushuka kwa kiasi Fulani. Hakikisha una lala angalao masaa saba hadi tisa kwa siku, jambo hili litaongeza uwezo wako wa kuhifadhi kumbu kumbu katika ubongo wako.2.Jiwekee tabia ya Kutembea kwa miguu mara kwa mara.
Kutembea tembea kwa miguu mara kwa mara ni njia mojawapo ya mazoezi kwani hupelekea mzunguko wa damu kufanya kazi kama inavyopaswa. Damu hubeba Oxygen ambapo oxygen hiyo itasafirishwa katika sehemu muhimu za mwili ikiwamo UBONGO wako.Pata mapumziko baada ya kufanya kazi kwa Muda mrefu.
Unapokua unafanya kazi kwa muda mrefu, akili nayo hufikia pahala na Kuanza kupunguza uwezo kwa Kuhifadhi mambo kama inavyopaswa.