Monday, November 13, 2017

Fanya Mambo haya kuifanya asubuhi yako iwe nzuri


Nilikua mtu wa Kuichukia asubuhi yangu kila kukicha. Nilichukia kuamka mapema, Lakini nilikua nikisikia na kusoma haya mambo na faida za kuamka hasubuhi na mapema. Kuamka mapema kuandaa mambo yako, Kuweka mambo sawa, kuuweka mwili wako fit nk.
Kipekee niliona faida za kuamka hasubuhi na mapema. Na zifuatazo ni njia za kuifanya asubuhi yako na siku yako kuwa nzuri kabisa.

1.Jinyooshe kwa Muda wa Dakika 15.

Punde tuu utakapokua umeamka toka kitandani, jinyooshe na kufanya mazoezi kama Vile Yoga kwa muda wa dakika kumi na tano. Kitendo hichi kitaufanya mwili wako kuchangamka. Nguvu hiyo utakayo pata itakaa na wewe siku nzima.

2.Kaa mbali na Vifaa vya Kielekroniki.

Utakapoanza kushika shika vifaa hivi mfano Sumu, computer nk utakua unajitengenezea Stress(Msongo wa mawazo) na kukuharibia siku yako kabisa. Unaweza kukutana na SMS ama Email ambayo kwa kweli itaweza kukukwaza siku nzima. Hivyo basi, ni vizuri ukaachana na mambo hayo hasubuhi na kufanya jambo jingine ambalo litakusaidia.

3.Tengeneza Plan yako ya siku nzima.

Ikiwa hukutengeneza plan yako kwa ajili ya siku inayofuata mara baada ua kutoka kazini, basi uamkapo asubuhi fanya jambo hilo. Kufanya hivyo kutakufanya wewe kuwekeza mawazo yako na nguvu zako zaidi katika Ufanisi wa kazi zako na Uzalishaji.

4.Pata breakFast ya Nguvu.

Najua unafahamu juu ya swala hili la kupata breakfast ya nguvu hasubuhi kabla ya kuanza shughuli zako. Unapokua unapata kifungua kinywa cha kweli pindi uamkapo unapata Nguvu ya kuanza shughuli zako kiuhakika, utaweza kulenga zidi katika shughuli zako.

5.Fanya yale mambo yanayokupa Furaha.

Furaha ni jambo Muhimu mno katika maisha ya mwanadamu awaye yeyote yule. Unapokua umeamka asubuhi jitahidi kufanya yale mambo yote ambayo hua yanakupa Furaha wakati wote, hii itafanya siku yako kuenda sawa sawia kwani Utakua na amani moyoni mwako na katika fikra zako hivyo kupelekea ufanisi katika katika kazi zako.

6.Kunywa Maji angalao glass Moja.

Ni wazi kwamba unapokua umelala usiku kwa muda wa masaa 8, mwili hupoteza kiasi fulani cha maji, hivyo basi yakupasa kupata maji walao glass moja ili kuongeza maji mwilini. Tia limao kidogo katika maji hayo na hii itakusaidia katika mmeng’enyo wa chakula kukaa vyema na zaidi ya yote utapata nguvu zaidi na mwili kuchangamka.

7.Jiweke teyari, hata kama utakua umekaa tuu nyumbani.

Labda umepanga siku yako kuwa ya Uvivu(Jambo ambalo ni poa pia kwa wakati mwingine), lakini ni vyema kujiandaa na kukaa sawa kwa ajili ya siku yako kwa ujumla hata kama hutotoka nyumbani siku nzima. Hii itakufanya kuuweka mwili wako sawa na hivyo kuwa full organized, jambo ambalo litakuweka poa siku nzima.

8.Anza Shughuli zako na Mungu wako.

Imani ni jambo la muhimu mno, Kila mmoja na imani yake, hivyo ni vyema kabla ya kuanza shughuli zako za kila siku ukanza na Mungu wako. Jambo hili litaluweka sawa kiroho hivyo hekima katika maisha yako itakua na wewe.