Saturday, November 18, 2017

MAMBO YA ZIADA YATAKAYO KUSAIDIA WEWE MWANAUME KUONGEZA UKARIBU WA KIHISIA NA MVUTO “EMOTIONAL INTIMACY” KWA MPENZI WAKO




§  Amua kuweza kuongea na mpenzi wako mara kwa mara, mueleze alivyo wa thamani kwako.

§  Kuwa tayari kumsikiliza mpenzi wako kila wakati ikiwezekana mguse au mshike wakati unapomsikiliza.

§  Angalianeni mara kwa mara hasa nyakati mnapokuwa na furaha au hata zile nyakati furaha inapokosekana

§  Mguse na mshike hata nyakati ambazo hauna haja na tendo la ndoa. Sio kwamba kila ukimgusa ndio ajue muda wa ku “do” umewadia

§  Msilale kama maadui, gusaneni na kumbatianeni, mbona hata wanyama wengine wanafanya hivyo?Ingawa hawana ndoa kama uliyonayo wewe? 

§  Kubali, heshimu na onyesha kupenda vile vitu vizuri anavyovifanya mpenzi wako, sio kila wakati wewe ni wakukosoa na kupinga tu.

§  Mpe tabasamu hatakama huna sababu maalumu ya kutabasamu, kwani unapoteza nini ukitabasamu? Au tabasamu inakugharimu kiasi gani? Mbona kwa wengine unatabasamu?

§  Mara nyingine chukua muda wako simama naye jikoni anapopika au anapofanya kazi nyingine, ongea nae, au onyesha kumsaidia kile anachofanya. Kule kusimama karibu naye hatakama haumsaidii kitu akiwa jikoni kunampa nguvu kuliko msaada wako mwingine katika maeneo mengine. 

§  Mwambie ukimwangalia usoni kwake kwamba pamoja na madhaifu yako yote (yani madhaifu yako wewe mwanaume) bado yeye ndiye mtu wa muhimu kabisa maishani mwako. Usinyamaze tu ukidhani anajua hilo, sema kwa kinywa chako, mwambie, tena sio tu kwa meseji za simu au kupitia meseji za mitandao, mwangalie usoni na umtamkie.