Wednesday, November 15, 2017

Jifunze kupitia mfano huu wa ufutio na penseli ✏

>PENSELI: "Nisamehe sana"
UFUUTIO: kwa nini? Mbona hujanikosea lolote?
PENSELI: Nisamehe sana unaumia kwa ajili yangu, kila ninapofanya makosa siku zote upo kwa ajili ya kuyafuta, ila kila unapofuta makosa yangu unaumia na kupoteza sehemu yako na umaendelea kupungua kadiri unavyofuta makosa yangu……. nisamehe sana ndugu!
UFUTIO: Ni kweli, ila mimi sijali sana.
"Hiyo ni kazi yangu, niliumbwa kwa ajili ya kukusaidia kila pale utakapokosea ingawa najua siku moja nitaisha na kupotea kabisa, ila nina furaha na kazi ninayoifanya".
Hivyo usijali najisikia vibaya ukiwa na huzuni maana inavyoonekana hupendi kukosea, wala hukosei kwa kukusudia ila unajikuta umekosea.
PENSELI: Nashukuru sana ufutio.
Maana yangu ni hii:
¶>Wazazi wetu ni kama ufutio, na sisi watoto zao ni kama penseli.
¶>Siku zote wazazi wetu wapo kwa ajili yetu kufuta makosa yetu na kutuelekeza njia zipaswazo kupita, na wafanyapo haya muda mwingine huumia hudharauliwa na kutengwa lakini wamesimama kidete kuhakikisha tunastawi vema.
¶>hakuna kitu kizuri kwa mzazi hasa waishio vijijini pindi atokapo shambani akikuta kuna chai, sasa umewahi kufikiri akikosa sukari anavyoenda kukopa kibandani ile ya kupima na wewe una katoni za sukari ndani???
¶>Naskia baba/mama yako ukitaka kumpigia simu unapiga kwa jirani yake ili ampelekee, na wewe una smart phone ya bei mbaya ikiwa na kifurushi cha mwezi msima cha elfu 30 umeshindwa kumtafutia hata simu ya elfu 15 halafu marafiki zako wanakuwish kwenye birthday yako at
"uishi miaka 1000 wakati hata vocha ya 1000 hujawahi kumtumia mzazi!
¶>Hivi unajua kwa kijijini elfu 5 ni hela ambayo hata siku 3 inafika? Halafu @ unasema siwezi kutuma 5000 ntawatuma nikichukua mshahara" saa ngapi wewee tuma hiyo hiyo!!!
¶>Watunze sana wazazi wako kama wapo na waheshimu na kuwapenda siku zote.
¶>Hakuna mahali popote Mungu alikoagiza baraka ya kuishi miaka mingi duniani isipokwa ni kwenye kuwaheshimu wazazi wako.
Mungu awape wazazi wako maisha marefu yaliyojaa heri, furaha na afya tele.
¶>Na kwa kufanya hivi sina maana kwamba nina hela, no! Jifunze katika kidogo kugawana na wazazi hasa ukijua maisha yao na mazingira wanayoishi.