Ya kizamani ilikuwa binti unajitahidi kuwa masafi na mwenye tabia njema kisha mwanaume anakuona kuwa wewe ni "ndoa type" then anakuja kwa wazazi wako kuposa kama sio wazazi wake wanakupenda kisha wanawashawishi wazazi wako wakubali uolewe na mwana wao wa kiume alafu from there ndio unaanza kujifunza kama sio kujilazimisha kumpenda aukumzoea kama mume wako ajae.
Kwa bahati siku hizi tunakuwa kwenye mapenzi na mapendo, kisha tunafanya nusu na robo kama sio yote yanayofanywa kwenye ndoa lakini jamaa halitangazi ndoa wala nini na wewe unahisi siku zinakwenda na huna mpango wa kuzaa nje ya ndoa.
Mwenyewe unajitahidi kumpena na kumuonyesha mapenzi yako, unaongeza ubunifu kitandani, unampa uhuru/nafasi yake anapohitaji kwenda kulewa (humfuatilii), mnakwenda kwenye sherehe za ndoa una-comment jinsi ambavyo siku moja ungependa naninyi mfanye hivyo.....yaani unampa dalili zote kuwa wewe ni a good wife, lakini Njemba haitangazi ndoa....!
Inaweza ikafikia wakati ukahisi uvumilivu umekushinda na umechoka kupotezewa muda na hivyo kuchukua uamuzi na kumwambia kama kweli unanipenda ungefunga ndoa na mimi siku nyingi so ama unanioa ktk wiki moja au uhusiano umekufa......hapo lazima atatangaza ndoa ili asikupoteze ikiwa kweli anakupenda au anajua unampenda na hakuna mtu atakae mpenda kama wewe ila tatizo la hii kitu ni kuwa wewe mwanamke ndio unaonekana Desperate kuolewa hivyo unakuwa umelazimisha......ni bonge la noma!
Nikirudi nitakupa mbinuz za kumfanya mshikaji atangaze ndoa na kuifanya itokee sio mnakuwa wachumba kwa miaka 3 wakati tayari mmeishi pamoja kama wapenzi kwa miaka 5.....it's boring bana.
Usicheze mbali. Utachumbiwa lini.........?
Wengi tunaamini kuwa matunda ya mapenzi ni ndoa na sote tunatambua kuwa ndoa ni jambo zuri, la heshima (wengi wanafeli hapa), busara na chanzo cha familia bora (japo kuwa mimi siamini sana hapa). Kinachosikitisha ni kuwa huu uamuzi huwekwa wazi na mwanaume na sio mwanamke hata kama wewe ndio unataka kuolewa yaani umefika bei n aunajua kabisa Haruna ni the one lakini Haruna mwenyewe khabari hana (well kama haruna (muislamu) na haja adopt tamaduni ya watu na yuko karibu au juu ya miaka 25 lazima atatangaza ndoa kwa mujibu wa dini yake) hivyo bora nitumie jina la Jonathan hahahahaha.
Nimeona hapo chimi M3 anasema wanawake tuwe wagumu kutoa K kwani akisha onja hataki tena, nasikitika kusema kuwa swala la ndoa M3 ni zaidi ya K na vilevile swala hili linachanganya kiaina. Wakati mwingine mimi huwa naamini kabisa kuwa ndoa ni mapenzi na uamuzi (labda kwa vile kila nilietoka nae kama mpenzi alitangaza ndoa), wengine wanadai kuwa ni bahati na baadhi wanasema ni lazima kama ilivyo ktk kuzaliwa na kufa, si unakumbuka sherehe 3 hapa duniani kuwa ni kuzaliwa, kuolewa/oa na kufa.
Watu nitakao walenga ni wale ambao wako tayari kwenye uhusiano na wanapendana lakini wanataka wapenzi wao wawasapuraizi kwa pete ya uchumba au hata kwenda kutambulishwa kwao kuwa wao ndio wapenzi wa kudumu.
Mpenzi akifika bei unamjua tu, wala huitaji vithibitisho si ndio jamani? Lakini mapenzi yake kwako sio tiketi ya yeye kukufanya wewe wa milele hivyo suibweteke nakusubiri siku akijisikia atangaze ndoa wengine mpaka uwaonyeshe kuwa "U can live with or without them" ndio wanajisogeza zaidi, sasa fuata haya yafuatayo:-
1-Ni mwiko kumkutanisha/tambulisha kwaa wazazi wako au kumpa namba ya simu ya nyumbani kama sio ya baba na mama (ya wazungu waachieni wenyewe) haruhusiwi kuwazoea bila kuji-commit. Kumbuka kuwa mwanaume anatakiwa kulifanyia kazi hili na kuhakikisha kuwa anakutana na wazazi wako nakujitambulisha ikiwa tu pete iko kidoleni na mnakwenda huko kutambulisha uchumba rasmi nakufuata taratibu nyingine za mahari, barua n.k. sio mmekutana leo kesho yuko sebuleni angalia Tv au kucheza na wadogo zako kama sio kuwapeleka kwenye manunuzi pale soko mjinga au kwenye maonyesho ya saba-saba.
Kama kwa bahati mbaya tayari amekwisha kutana na wazazi wako kabla ya makala yangu hii basi hakikisha hapati tena nafasi hiyo,mpaka kuwepo na pete au hata yeye kuandika barua nakulipa mahali nusu na robo (mana'ke sio wote wanaamini ktk pete).
Ikitokea shughuli kubwa kwenye Ukoo wenu kama vile sherehe za ndoa au Msiba hakikisha unakwenda mwenyewe bila yeye, ofcoz unamwambia nini nimetokea (msiba)au kinakwenda kutokea(ndoa) na akiomba kushiriki au kwenda na wewe mwambie ungependa awepo lakini hudhani kuwa ni wazo zuri kwani utakuwa busy sana (hutokuwa na muda wa kuwa pamoja kama wapenzi) na sio hivyo tu bali unajaribu kum-save na too much hassle.....hapa atakuona wewe ni wa maana sana nakuna uwezekano mkubwa siki za karibuni akataka uwe wake wa daima milele(Daima).....Usisahau kuwa hayuko pale kupendwa na ndugu zako na wala haitaji kupenda na kuzoea nyumbani kwenu.
2-Kamwe aah ni marufuku kuhamia kwake au yeye kuhamia kwako ikiwa kila mmoja wenu anajitegemea (anaishi kwake), wengi hukimbilia ku-move in wakihofia wapenzi wao kuchukua watu wengine na kulala nao.....skia wewe, achakuwa tegemezi kihivyo (emotional) utakimbiwa, kila mtu anahitaji nafasi yake time to time, swala la kulala na mtu mwingine kama lipo basi anaweza na mtu huyo hotelini, nyumba za kulala wageni au hata ofisini wakati kila mtu katoka....swalamuhimu ni mapenzi ya dhati na uaminifu.
Ikiwa ulihamia kwake ili ukamuonyeshe umuhimu wako kama "mke" yaani kupika, kusafisha, kupiga basi, kumpangia nguzo shati na tai nzuri kwa ajili ya kazini n.k. na bado Njemba haina dalili yakutangaza ndoa basi ni wakati wa kuhamia kwako peke yako kama sio kurudi kwa dada/wazazi, na kumbuka unapo hama bakiza kachupi kako kadogo ambako anakapenda kukaona maungoni mwako.
Ukihamia kwa mpenzi wako kabla ya kuchumbiwa, itamafanya ajisahau navilevile atakujua kwa sana yaani mambo mengine ulitakiwa uyafanye baada ya miaka 5 yandoa wewe unayafanya kabla hata ya uchumba na nina kuhakikishia ndoa haitoangazwa unless baba na mama'ke wamwambie "hey bwan' mdogo unataka tufe kabla hatujamuona mkwe na mjukuu "ndio atatuma posa? Yaleyale......!
Kuhamia kwake kunaruhusiwa ikiwa tu ametangaza ndoa na maandalizi ya ndoa yameanza (tunaita trial), alafu mwezi mmoja kabla ya ndoa unarudi kwenu....sio kwako....kwenu kwa wazazi au ndugu.
3-Ni mwiko kujifananisha ninyi na pea inayo au iliyofunga ndoa hivi karibuni, yaani wewe unatakiwakua "nunda" when it comes kwenye maswala ya ndoa au uchumba wa watu wengine, hasa kama yeye anaonyesha kutokuwa na habari (kawaida wanaume huwa hawana habari wala wivu) basi na wewe kuwa kama yeye.
Siku umeenda kumtembelea Mpenzi amabe kafika bei ila swala la ndoa halipo eti mpaka ajenge nyumba......lini? (kumbuka hakuna kuishi pamoja mpaka achumbie)ukiwa unaongea na rafiki yako amabe kafunga doa hakikisha unasema sentensi za kuponda ndoa kwa sauti ili mpenzi asikie tena kwa kunogesha muulize "hivi inakuwaje unaweza kuishi na mtu yuleyule kila siku iendayo kwa Mungu?" Mimi sidhani kama nitaweza, nahisi itakuwa boring"......hehehe kwa yote unayomfanyia nakumridhisha kitandani, kwa jinsi unavyompenda na kumjali alafu anasikia hivyo.....yaani akili itamjia Njemba nyingine zinaweza niwahi hapa......ataenda itafuta pete ktk siku zijazo, wewe subiri tu.
Hakikisha unayasema yote hayo kuwa unajua kabisa anakupenda kwa dhati na maisha bile wewe ni bora kifo.....mana'ke ukisema haya kwa player ujue kashinda na atakung'ang'ania na pete usiione alafu anaenda kuoa mtu mwingineee.
Nakuja...kumalizia....acha nitengeze vijiseti vya kusukuma mwezi