Tuesday, May 1, 2018

KAMA Unafanya Mambo Haya Lazima Utaishi Maisha Mafupi.





Kwa kawaida maisha ya kibinadamu mwisho wake huwa ni kufa, hivyo kila mwenye pumzi hii leo mwisho wa maisha yake huishia kaburini.
Hata hivyo, kumekuwepo na viashiria fulani fulani ambavyo huweza kuashiria baadhi ya makundi fulani ya watu huenda wanaweza kuwa na muda mfupi wa kuishi duniani kutokana na sababu tofauti tofauti.
Miongoni mwa dalili ambazo huweza kuashiria mhusika anaweza kuwa na maisha mafupi duniani ni pamoja na hizi zifuatazo.
1. Watu wenye kupenda maisha ya anasa na starehe
Watu wa aina hii huwa katika hatari ya kupoteza maisha haraka hata kabla ya siku zao kutokana na kuwa na hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya zinaa.
2. Wavutaji wa sigara.
Watu wanaovuta sigara huwa katika hatari ya kuishi maisha mafupi zaidi kuliko wale ambao hawatumii sigara kwani watu wa aina hii huwa katika hatari ya kukumbwa na saratani ambayo huweza kukatisha uhai wa mhusika hata kabla ya siku zake.
3. Kushinda umekaa siku nzima
Wale ambao huwa miili yao haina mazoezi kabisa nao huwa katika hatari ya kupoteza maisha mapema kutokana na kushambuliwa na magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari nk.
4. Unywaji wa pombe
Watumiaji wa vileo na huwa katika hatari ya kupoteza maisha yao mapema kutokana na mambo mawili makuu
a) Kupata ajali kutokana na kutumia vyombo vya moto wakati wakiwa wamelewa na baadaye kujikuta wanapoteza maisha.
b) Ugomvi ambao huweza kuibuka kutokana na mihemko ya vilevi wanavyokuwa wamekunywa na kuweza kusababisha ugomvi mkubwa. Mfano kupigana na chupa na baadaye kupoteza uhai.
5. Ulaji wa vyakula vya viwandani
Kuna wale ambao mara nyingi wamekuwa wakila vyakula vya makopo ambavyo vinapotumiwa mara kwa kwa mara huweza kuwa na madhara kadhaa likiwemo tatizo la saratani. Hivyo kundi hili nalo linaweza kuwa katika hatari ya kupoteza maisha kabla ya siku zao