Wednesday, November 22, 2017

Picha: Hawa ndio wake 10 wa marais wa Afrika, wanaotajwa kuwa wazuri zaidi

Mwaka jana (2015) mtandao mmoja wa Afrika, uliwataja ‘Ma-First Lady’ 10 wa Afrika ambao wanaaminika kuwa ni warembo zaidi kuliko wengine. Orodha hiyo ilitolewa na kuchambuliwa na timu ya wahariri wa mtandao huo huku ikiwaachia wasomaji kutoa maoni yao.
10: Margaret Gakuo Kenyatta (Kenya)
Mke wa Kenyatta
Huyu ni mke wa Rais Uhuru Kenyatta ambaye ana umri wa miaka kati ya 50 na 51. Licha ya kuwa na umri huo, sura yake na muonekano wake ‘simple’ unamfanya awe na mvuto wa aina yake huku nywele nyeupe zikimpa utambulisho wa aina yake.
Baadhi husema anaonekana ana aibu pale anapokuwa mbele ya hadhara, lakini hilo linamuongeza uzuri wake.
 9: Dominique Folloroux-Ouattara (Ivory Coast)

Ivory Coast 2
Dominique, ni raia wa Algeria kwa kuzaliwa na ni mfanyabiashara. Ingawa ana umri wa miaka 61 (bibi), lakini kwa uzuri na urembo wake na jinsi anathibitisha umri sio kikwazo.
9. Olive Lembe di Sita Kabila (Democratic Republic of Congo)
Olive Lembe di Sita, ana umri wa miaka 38 unaomfanya kuwa miongozi mwa wake za Marais wenye umri mdogo zaidi Afrika. Aliishi kama mchumba wa Rais Kabila kwa muda mrefu kabla hawajafunga ndoa.
Congo
 7: Ana Paula dos Santos (Angola)
Angola
Alikuwa mwanamitindo maarufu nchini humo na mhudumu wa ndege (air hostess). Kazi iliyompelekea kukutana na mpenzi wake ambaye sasa ni rais wa Angola, Jose Eduardo Dos Santo.
6: Malkia Inkhosikati LaMbikiza (Swaziland)
Swaziland
Ingawa inafahamika kuwa Mfalme Mswati III ana wake 15, lakini Lambikiza ndiye mkewe wa kwanza ampendaye sana.
Ingawa LaMbikiza aliacha shule akiwa na umri wa miaka 16 tu, ili aolewe na Mfalme, alijiendeleza hadi sasa ana degree ya Sheria.
Hata hivyo, Degree ya sheria aliyonayo inabaki tu kuwa kwenye makaratasi kwa kuwa haruhusiwi kuifanyia kazi kwa hofu kuwa Mahakama zinaweza kumpendelea kwa kutumia kigezo cha kuwa Malkia.
5: Zeinab Suma Jammel (Gambia)
 Gambia
Zainab ni raia wa Morocco na mama wa watoto wawili mwenye urembo na uzuri wa aina yake. Hata hivyo, hukumbana na changamoto ya kukosolewa sana nchini Gambia ambapo watu humuita majina mengi mabaya kama ‘Gold Digger’, wakimaanisha anamchuna rais wa Gambia.
4: Hinda Deby Itno (Chad)
Chad
Hinda Deby, ni mwanamke mrembo anayependa mitindo ya mavazi na mpole. Muda mwingi amekuwa akivaa magauni mazuri yanayo-oana rangi na mitandio yake.
Pamoja na kuufunika mwili wake kwa mitandio na magauni marefu, bado uzuri wake huonekana dhahiri.
3: Chantal Biya (Cameroon)
Cameroon
Chantal Biya ni ‘first lady’  mrembo haswa, anayependa mitindo ya mavazi na kujiweka sawa kichwani kwa mitindo mbalimbali ya nywele. Mavazi mengi anayopendelea kuvaa huwa katika mtindo unaoendana na utamaduni wa nchi yake.
2: Princess Lalla Salma (Morocco)

Mfalme wa Morocco

Princess Lalla Salma ni mke wa Mfalme wa Morocco, Mohammed VI. Huyu ni mwanamke mzuri sio tu kwa sura lakini hata kiakili yuko ‘smart’ sana.
Kutokana na shughuli mbalimbali anazozifanya, amekuwa na ushawishi mkubwa kwa serikali ya Morocco.
1: Sylvia Bongo Ondimba (Gabon)
Gabon
Sylvia Bongo ametajwa kuifunika orodha hii ya wake za Marais wa Afrika wanaotajwa kuwa warembo zaidi. Sylvia pia anapewa nafasi ya kuingi kwenye orodha ya wake wa Marais warembo zaidi duniani.
Wapo ma-first lady wengi waliojaliwa uzuri na urembo, lakini mtazamo umewapa nafasi 10 za juu zaidi hawa.
Je, unaionaje hii orodha na ni yapi maoni yako?