Thursday, October 4, 2018

Wanawake: Mumeo akikukera usilale mpaka pakuche hamjasameheana




Usiku kama mumeo kakukera usilale mpaka pakuche hamjasameheana, hata malaika baraka hawawezi shuka kwenu. Huyo ulionae amezaliwa kwao kaja na tabia zake na wewe umezaliwa kwenu una tabia zako.

Sasa ukitaka kila kitu kiwe wewe unavyotaka atakuwa mwanao tena huyo sio mumeo samehaneni kwa kila mnalofanyiana.

Usiweke vinyongo tena ukajua unamkomoa mana unavyonuna ndo mchepuko unavopata chance ya kuwasiliana na si kila mwanaume anamchepuko wengine washkaji tu sasa ukijitia umenuna kisa umemuona kachat, sijui umekuta meseji sijui nini utakonda uzikwe na presha na unavyotiwa kaburini tu huku wenzio wanamtext pole kazi ya Mungu mpenzi.

Gangamala mtoto wa kike sio kidogo kununa kama unga wa ngano ulokosa amira. Tabasamu njia nzuri na sahihi ya kumuua mtu akikosea ukatabasamu ataanza kutafuta mchawi kumbe mchawi mwenyewe, ataanza kutoka kujua kwanini hujakasirika atatulia tu akiamini anakuvizia kumbe anajivizia.