Tango ,,Tunda hili linaweza kupambana na kuchakaa na kuchoka kwa ngozi kunakosababishwa na tabia mbalimbali. Pia lina uwezo mkubwa wa kusafisha ngozi hasa ya uso. Hiyo ni kazi moja kati ya nyingi zinazofanywa na tunda hili. Unachotakiwa kufanya ni kusaga tango moja, kisha kuchuja juisi yake. Chukua pamba na chovya kwenye mchanganyiko wako kisha pakaa usoni. Kaa kwa muda wa dakika 20 hadi 30. Osha uso wako, kisha kausha kwa kitambaa safi na laini.Ikiwa juisi itakuwa nyingi, unaweza kuihifadhi kwenye jokofu kwa ajili ya matumizi ya siku za baadaye. |