Kuna dada mmoja nje ya nchi ambaye anataka kuja hadi hapa Sikonge ili nimtungishe Mimba na hatimaye azae mtoto. Huyu mdada ni mtu ambaye ninafahamiana naye kwa miaka mingi kidogo tangu nikiishi nje ya nchi ambapo siku hizo, hakuwa au nilikuwa sijajua kama ni SHOGA.
Anasema yupo tayari kuwekeana kabisa mkataba na mie kwamba gharama zote za mimba na kulea mtoto hatanidai na mtoto ataandikishwa kwa jina lolote nitakalokubali mie na hata akitaka atanilipa. Sijui kaona kitu gani cha ajabu kwa Mnyamwezi mie ingawa kiukweli hadi leo hii sijawahi hata kumbusu, acha kutembea naye.
Kuhusu Mimba anasema inaweza kuwa kwa njia ya kawaida kwa kufanya mapenzi au kwenda hospital na huko wakafanya kupandikiza kama wanavyofanya kwa wale wanaotoa mbegu za Kiume na kuwapa akina mama ambao hata hawawajui.
Shida kubwa iliyopo ni kuona kuwa Mtoto wangu anaweza kukulia kwenye familia au nyumba ambayo Mama anaishi na GIRLFRIEND wake na kwa maana nyingine ni kwamba, hawa ni Wasagaji. Mbaya zaidi kakiwa ka kike, si ndiyo itakuwa shida kwa mtoto huyo? Itabidi ajifunze kuwa Mliberali mapema sana au aungane nao.
Hebu nyie wakali na wazoefu wa haya mambo mniambie, kwa hili NIKUBALI au NIKATAE?
ANGALIZO: Hii ni habari ya kweli, utani pembeni Bandugu