Wednesday, October 3, 2018

KUMBE WANAUME NAO HUINGIA KATIKA HEDHI!

Kwa wanaume ni kasheshe!
Mara nyingi nimekua nikiamini kwamba yale tunayoyafahamu kuhusu maisha ni machache sana ukilinganisha na yale tusioyafahamu. Kiasi cha miezi kadhaa iliyopita nilisoma utafiti fulani kuhusu hedhi. Awali nilipousoma niliona ni hadithi tupu. Lakini nilipoona ni vyema kuujaribu kwa kutenda miezi minne baadae nilishangaa. Hata wewe najua utashangaa utakaposoma makala haya. Lakini ombi langu kwako ni kukutaka ujaribu kufanya mazoezi ili uthibitishe ukweli huo.

Kikomo cha kuwa na hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume ni miaka 42. Hata wanawake ni hivyo hivyo. Kama mwanamke ataruhusiwa kuwa na uhuru wa kufanya mapenzi kila wakati kama apendavyo bila kuzuiwa na mila na desturi kikomo cha kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi ni miaka 42.

Hakuna tofauti kati ya wanawake na wanaume. Miaka ya hivi karibuni imegundulika kwamba hata wanaume hupata hedhi-ingawa wanaume hawana alama za nje za kuwaonesha kwamba wako kwenye hedhi, kama walivyo wanawake ambao hutoka damu siku zao za hedhi zinapofika na kukamilika.

Kwa karne na karne hakuna mtu aliyekuwa akifikiria kwamba wanaume wangeweza kuwa wanapata nao hedhi kama wanawake.

Kama mwanaume akiamua kuweka kumbukumbu zake kwenye dayari na kujiangalia kila siku hali yake inavyobadilikana kuwa ya kusikitika, ya kawaida, furaha na hasira……akiifuatilia hali yake namna hiyo kwa siku zote 28 za mwezi, halafu na mwezi unaofuata, akafanya hivyo hivyo, halafu mwezi wa tatu nao akatenda hivyo, na halafu ailinganishe miezi hiyo mitatu atashangaa.

Kuna siku tatu, nne au tano ambazo zitafanana katika dayari zote tatu, lini ana hasira ana masikitiko, ni mharibifu, na tabia nyingine kama hizo. Hivyo ndivyo vipindi vya hedhi kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake.

Zoezi hili anaweza kufanya mwanaume yeyote, akishindwa kupata matokeo anaweza kuwasiliana na blog hii ya Utambuzi na Kujitambua na kuuliza ni kwa nini nimeandika uongo.

Ni jambo ambalo lipo na limeshafanyiwa tafiti mbalimbali, hata mimi binafsi nimefanya zoezi hilo kwa miezi minne na limetoa majibu kama hayo.

Kwa kawaida mwanaume hana dalili za kimwili za kutoka damu kama mwanamke – ndio maana, karne na karne hakuna mtu aliyejali – lakini ni jambo la uhakika kwamba wanaume wanapata hedhi.

Dalili za mwanaume aliye kwenye hedhi ziko akilini zaidi na sababu ziko wazi: mwanamke asili yake ni kimwili zaidi, kihisia zaidi, na mwanaume ana asili ya ubongo zaidi.

Lakini mwanaume anapata usumbufu ule ule anaopata mwanamke anapokuwa kwenye hedhi. Tofauti ni moja tu, kwamba mwanaume hatoki damu. Lakini kila mwezi, baada ya siku 28, hali fulani ya kiakili na kihisia itakuwa inajirudia.

Na kama umejaribu kujichunguza kwa mwaka mzima, utashangaa kwamba, ulikuwa na hasira mgomvi, mwenye huzuni na vingine vya aina hiyo, si hivihivi tu bali ni kwa sababu ulikuwa kwenye hedhi.

Kama ukishafanya zoezi nililokwambia la dayari, jiulize, kama ulipokuwa kwenye hali hizo ulikuwa umekerwa na yeyote au chochote. Utagundua kwamba hukuwa umekerwa bali ulikuwa unasumbuliwa na hedhi yako.

Wanaume na wanawake wanabalehe au kuvunja ungo karibu muda ule ule; umri ambao ni miaka 13. Kwa hiyo kikomo cha kusikia hamu ya ngono hakiwezi kuwa tofauti; kitakuwa miaka 42. Lakini miaka hii 42 inategemea na majaaliwa ya asili.

Kama mwanaume sio mchafu wa kupenda sana ngono, basi miaka 42 hakitakuwa kikomo chake cha kuwa na hamu ya kufanya ngono, ataendelea kuwa na hamu ya kufanya ngono hadi atakapoenda kaburini.

Mwanamke kadhalika kama sio mpenda kufanya ngono kwa fujo naye hamu ya kufanya ngono itandelea hata baada ya kuvuka miaka 42. Vinginevyo kama mwanamke ni mwingi wa mambo, katika umri wa miaka 42 ataacha kuona hedhi yake.

Akishafikisha miaka 42 hamu yake ya kufanya mapenzi inaisha vilevile, katika umri huo huo. Kwamba kila mwanamke anayekoma kuona hedhi kwenye umri huo ni mwingi, hapana.

Mwanaume na mwanamke wameumbwa kwa ‘matofali’ yaleyale, kwa maumbile yaleyale na baiolojia ileile. Tofauti yao ni kwamba mwanaume ni chanya na mwanamke ni hasi kama tungekuwa tunazungumzia umeme.

Huwezi kupata umeme kwa kuwa na chanya mbili; wala ukitumia hasi mbili bali ukichanganya chanya na hisi. Hivyo, kama mwanamke anapata hedhi kama hatua muhimu kuelekea mwito wa kimaumbile, haiwezekani mwanaume asipitie hatua hiyo, ingawa kwa uchanya wake.

Kupata hedhi kwa mwanamke inaeleweka kwamba, ni kutokana na wito wa kimwili. Maana yake ni kwamba, alikuwa amefikia hatua ambapo kimaumbile alitakiwa kujamiiana ili apate ujauzito.

Je, kama hakuna mabadiliko kwa mwanaume, itawezekana vipi mwanaume kujamiiana na mkewe ambaye yuko kwenye hitaji hili la kimaumbile?

Ina maana basi kwamba mwanaume naye ni lazima kila mwezi awe na mabadiliko ambayo yatamfanya aingie mahali ambapo atavutana na mwanamke kimapenzi.

Hili ni suala la maumbile ili kufanya kuzaliana kuwepo. Utajuaje kuwa mwanaume ameingia kwenye hali hiyo? Ndiyo pale ambapo wataalamu wamegundua hizo siku nne au tano za mabadiliko ya kiakili kwa mwanaume!