Saturday, September 29, 2018

NJIA YA KUMPATA MWANAMKE MZURI UMPENDAE.(Kwa watu wazima tuu)


Sanaa ya Kutongoza(Art of Seduction) ni sanaa yenye mambo mengi,lakini mara nyingi ni sanaa ambayo inaconcentrate kwenye attention ambayo wanaume wengi wanapenda na wanataka kuipata kutoka kwa wanawake. 

Leo nikaona si vibaya kama nikishare tips muhimu ambazo zitawasaidia kumpata mwanamke yeyote yule unaetaka kuwa nae,

1. JITAMBULISHE VIZURI KISTAARABU (INTRODUCE YOURSELF PROPERLY)Kama ndio umekutana nae kwa mara ya kwanza,hakujui na wewe humjui,ni vizuri ukajitambulisha vizuri kwa ustaarabu(usela,mapozi na uhuni weka pembeni),kama alikuwa anatembea unataka kumsimamisha,tumia lugha nzuri kumsimamisha,na usije ukasimama ukadhani atakufuata,changamka mfuate wewe,mkiwa mnatembea wote,jitambulishe vizuri,epuka maneno yatakayomkera,usimuulize maswali yatakayochokonoa maisha yake binafsi kwa kuwa bado hamjazoeana sana(Dont ask her personal questions)

2. ONGEZA MVUTO WAKO WA KIMWILI (UPGRADE YOUR PHYSICAL ATTRACTION)Wanawake wengi wanapenda wanaume wenye mvuto,wanapenda wanaume wenye miili iliyojengeka kiume kimazoezi(six pack na blah blah nyingne za ziada),kwa hiyo ili iwe rahisi kwako wewe kumshawishi(kumseduce) mwanamke unayempenda,ni vizuri ukahakikisha mvuto wako upo juu tena sana.Kama ni mnene au una kitambi anza kufanya mazoezi upunguze mwili.

Kuwa Msafi(kama vipi oga hata mara 3 kwa siku),vaa vizuri upendeze,kwa sababu first impressions zinalast longer kuliko unavyoweza kudhania.

3. WASILIANA NAE MARA KWA MARA (CONTACT HER FREQUENTLY)Kila mwanamke anapenda mwanaume ambaye atakuwa anamjali,Mwanaume atakaekuwa teyari kusikiliza stori,matatizo na shida zake na kumsaidia kusolve,Mwanaume ambaye atamfanya ajisikie Special muda wote .Na kitendo cha wewe kuwasiliana nae mara kwa mara kitaonyesha kuwa unamuwaza muda wote,kitaonyesha kuwa unamjali n.k na pia kitasaidia kuwafanya mzoeane kidogo kitu ambacho ni kizuri kwako ukitaka kumake a move

4. KUWA MUONGEAJI MCHESHI (BE TALKACTIVE WITH A GREAT SENSE OF HUMOR)Hakuna Mwanamke anaependa kuwa bored,wanawake wengi wanapenda kucheka na kuwa na furaha muda wote,kwa kuwa bado hajakuzoea sana,itabidi wewe ndio uwe unaongea zaidi,jaribu kuongea mada(topics) ambazo anapenda(utajua kuwa anapenda kwa kuangalia the way anarespond),ukianzisha mada ambayo hapendi ni heri uiache uanzishe nyingine usije ukamboa.Pia jaribu kumtania ili atabasamu au acheke lakini usivuke mipaka(limits),utani unaweza ukawa wa kawaida lakini itapendeza zaidi ukiwa wa kimahaba.

5. NUNUA ZAWADI ZA KIMAHABA KWA AJILI YAKE(BUY ROMANTIC GIFTS FOR HER)Unapokuwa unachagua zawadi,usikimbilie kununua zawadi zenye Gharama kubwa sana,kwa mwanamke aliyetulia mwenye akili zake timamu,atapata hisia mbaya kwamba unataka kununua Penzi lake.(atahisi kuwa unataka kuchezea hisia zake kisha umkimbie).Itakuwa vizuri kama ukinunua zawadi ambazo sio expensive sana lakini ziwe na ujumbe wenye maana kimahaba.Unaweza kumnunulia Apple,Chocolate,hereni n.k(just try to be more creative,t always work).