Thursday, July 19, 2018

KISA Cha Kusikitisha 'Baba Yangu Alisababisha Nilale na Mjomba Wangu, Kamwe Sitamsamehe'



Nimeona leo nitoe siri yangu hapa ya muda mrefu ambayo imekuwa ikiniumiza sana pale tu ninapokumbuka, nakosa raha na amani inapotea.

Kwa ufupi kabisa, nilizaliwa mkoani Mara wilaya ya Musoma mjini maeneo ya Nyakato, mama yangu alibeba mimba yangu akiwa darasa sita hivyo hakumaliza shule. Ilibidi akae nyumbani mpaka pale alipojifungua, kwa wakati kulikuwa hakuna sheria kali kwa wanaowapatia wanafunzi mimba wakiwa shule. Na aliyempatia hiyo mimba naye alikuwa mwanafunzi mwenzake lkn alikuwa la saba yeye alimaliza shule. Baba yake mama ambaye ni babu yangu alikuwa na uwezo mkubwa hivyo hakushindwa kutulea mimi na mama. 

Nikiwa na miaka 6 ndipo nilipokuja kumjua baba yangu wakati huo nae alikuwa amekuwa mtu mzima, alikuja akanisalimia akaondoka, kwao pia walikuwa vizuri kimaisha.

Nikiwa na miaka 9 naanza darasa la kwanza wakati huo tulikuwa tunaingia shule tukiwa na umri mkubwa tofauti na sasa. Mama aliolewa na mume mwingine na alikuwa ni askari jeshi, alifanikiwa kuzaa nae watoto wanne jumla kwenye familia yetu tukawa 5 wasichana tukiwa wawili na wavulana wakiwa 3. Tuliishi vizuri sana, na familia ilikuwa na furaha sana na hatimaye tulijenga nyumba nzuri sana mtaa wa Majita road hapo hapo musoma. Nakumbuka nikiwa darasa la sita babu yangu kizaa mama alifariki duniani na ndiye aliyekuwa tegemeo la familia ya kina mama. Pia wakati huohuo baba yangu wa kufikia walikorofishana na mama kupelekea mpaka wakaachana na alihamishwa kuja Dar es salaam Lugalo. Sisi tulibaki Musoma tukiendelea na maisha.

Kumbuka wakati wote huo baba yangu mzazi ajaonekana kwa kipindi kirefu. Kwa upande wangu si kuwa na shida na nilifika mahali nikamsahu kabisa. Mama alikuwa anajituma sana alikuwa ana hotel yake hapo hapo Musoma hivyo alivyoachana na baba yangu wa kufikia akutetereka kiuchumi. Nilisoma na Mungu alinijalia kichwani nilikuwa vizuri toka darasa la kwanza nilikuwa nashika nafasi ya kwanza nikishuka sana nafasi ya pili mpaka la saba. Baada ya kuhitimu la saba Mungu alinijalia nikafahulu vizuri na kuingia kidato cha kwanza.

Wakati nikiwa kidato cha pili baba alikuja kutoka Arusha maana alikuwa anakaa huko, alipokuja alinikuta naendelea na masomo yangu vizuri. Alifika mpaka nyumbani nakumbuka mama alipomuona alimfukuza, wakaja watu kusuluisha na wazee kwamba ampe nafasi ya kumuona mwanae mama alikataa. Akamwambia wakati huo alikuwa wapi? Basi siku moja niko shule maana nilipangiwa hapo hapo Musoma sekondari, alifahamu ninapo soma kaja kaulizia walimu akanipata, niliitwa darasani nilipotoka nikamuona lakini sikumjua vizuri maana ni siku nyigi sana. Akanambia ni baba yako kwani umenisahau? Nilikataa kuongea lakini alinisihi sana mwisho nilikubali kuongea nae wakati anaondoka akanipa laki moja za matumizi akaondoka. Nilipofika nyumbani nilimpa mama hiyo pesa alishangaa nimetoa wapi, nikamwelezea yote basi mama akapokea. Kesho baba akaja akaomba msamaha hapo mama akamwambia kikubwa nataka umsaidie mwanao basi. Basi baba akaondoka.

Nilipofika kidato cha tatu mama alianza kuugua sana, tukaanza kuzunguka mahospitali kila akipimwa hakuna ugonjwa, tukaenda Bugando ugonjwa haukuonekana, tukaenda Muhimbili pia ugonjwa akuonekana kumbuka mama ndiye tegemeo la familia pesa za matibabu zilitoka kwake mpaka ikafikia hatua tukafilisika hotel ikafungwa hali ikawa mbaya sana. Tukaanza kuishi kwa shida sana. Tukashauriwa twende kwa waganga tukazunguka, alikuwa anapata nafuu kidogo kisha ugonjwa unarudi tena. Nikaanza kumtafuta baba ili atusaidie kila nikiongea nae kwa njia simu anatoa ahadi tu mwisho nikakata tamaa. Kwa baba wa kufikia aliyoko Dar nae alikuwa kimya sana alisahau hata familia yake kabisa. Hivyo tulikata tamaa kabisa na mababa hawa. Tukaamua kuishi maisha yetu bila kutegemea wao tena.

Nilisoma kidato cha nne kwa shida sana, tukitoka shule mimi na wandogo zangu tunaenda kutafuta vibarua vya kufanya ili tupate kula. Mpaka nikamaliza form 4, baada ya matokeo kutoka nikawa nimefahuru vizuri nikapagiwa shule ya advance huko Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro. Hapo ndipo ilikuja kesi ni wapi pa kupata pesa ya shule. Jamani umasikini mbaya sana, kama ujapitia mshukuru Mungu sana. Mama yangu wakati huo hali yake iliendelea kuimarika baada kwenda kwenye Maombi. Tuliangaika sana na mama lakini hatkufanikiwa kupata pesa ya kutosha.

Namshukuru Mungu kwa kipindi chote hicho sikuwahi kukutana na mume japo nilikuwa mzuri mtaani kwangu, walinisumbua mpaka waume za watu lakini hawakunipata. Lkn nilipata wazo nikasema baba yangu yuko Arusha na mm nimechaguliwa Mkoa wa Kilimanjaro ni mikoa iliyokaribu. Nilimpigia simu nikaongea nae nikamwambia nimefahalu lkn sina pesa akasema wakati unakuja shule pitia hapa Arusha nitakupa pesa za shule. Basi nikaona unafuu mkubwa, nikajianda maana muda ulikuwa ushafika. Arusha huko alikuwepo mjomba wangu tumbo moja na mama alikuwa askari wa FFU hapo Arusha lakini alikuwa na roho mbaya sana hawezi kumpa mtu msaada kirahisi. Nilimtaarifu pia kwamba nitakuja na nitafikia kwake alikubali.

Siku ya safari nilimtaarifu baba akasema sawa, nikamwambia nitafikia kwa Mjomba alafu ndio nakuja kwako kuchukua pesa za shule, tukakubaliana. Nilipofika Arusha majira ya saa 2 usiku mjomba alikuja akanipokea akanipeka kwake, mjomba alikuwa na mke na watoto wa 3, ila wakati nafika nilikuta mke wake ameenda kwao likizo, yupo mfanyakazi wa ndani na watoto, cha ajabu nilianza kutafuta baba kwenye simu akupatikana tena.

Nilikaa kwa mjomba siku 4 bila baba kupatikana kwenye simu sikuwa na pesa yoyote. Ikabidi nimwombe mjomba anisaidie angalau kidogo niende shule baba akipatikana akinipa nimrudishie mjomba alikataa katakata. Niliwaza sana sikujua ninzie wapi nilikata tamaa ya kusoma tena, ikabidi nimwombe mjomba nauli ya kurudia kwetu Musoma napo aligoma akasema subiri mpaka baba yako apatikane. Siku moja jioni katoka kazini akaniita chumbani kwake nilishutuka lakini akasema njoo nikupe pesa za shule, kweli nilipoingia ndani akanipa laki tatu, nikamshukuru sana sikuamini, nilipotaka kuondoka akanishika mkono akanitazama akanimbia naomba nilale na wewe usiku wa leo, niliogopa na kushituka sana, alifunga mlango akanitishia mwisho nilipoa akafanya anachotaka kufanya, aliniumiza sana maana sikuwahi kufanya kideto hicho. Baada ya kumaliza akanipa hizo pesa nikajianda kwenda shule kabla sijaenda akanifanya tena alinigeuza mke wake, sikumwambia mama yangu chochote maana angesikia yawezekana angekufa kabisa. Lakini yote hayo kwa sababu ya shida.

Nikafanikiwa kwenda shule, nilisoma vizuri na mjomba akawa anakuja hapo shuleni kuniletea pesa za matumizi siku za Jumapili nakunichukua kwenda gesti, maisha yangu yalikuwa hayo mpaka namaliza kidato cha sita, nikarudi nyumbani Musoma mama alifurahi sana aliposikia mjomba alinisomesha, lakini nilikuwa siri yangu. Mjomba alitaka nilirudi tena Arusha huku nikisubiri kwenda chuo kikuu. Nilikataa kabisa na mimi nilikuwa tayari nimetimiza malengo ya kishule sikuwa na hamu tena bali niliendelea kujutia dhambi niliyofanya.

Mungu alisadia nikapangiwa chuo cha Dar es salaam, nilipata mkopo hivyo ulinisaidia mpaka namaliza chuo, nikakutana na rafiki wa kiume mwanachuo mwenzangu, tulipohitimu tulifunga ndoa na sasa tuna watoto 2. Hii ni siri kubwa sijahawahi mwambia mume wangu. Baba aliposikia nimemaliza chuo akajitokeza, nilifukuza kwangu na kamwe sitaweza kumsamehe katika maisha yangu.