Wednesday, June 13, 2018

Msanii Jux Afuguka Ya Moyoni Jinsi Vanessa alivyoyabadili maisha yake toka waingie kwenye Uhusiano.

Mapenzi ya mwimbaji wa R&B Juma Jux na Vanessa Mdee a.k.a Vee Money sasa yamefikia kwenye ‘climax’. Licha ya kukiri hadharani kuhusu uhusiano wao lakini sasa kila mmoja wao amekuwa tayari kuelezea jinsi anavyompenda mwenzie hadharani ikiwa ni ishara ya kuwa mahaba yako kileleni.
Jux n vee-1
Jux katika kusheherekea siku yake ya kuzaliwa ambayo ilikuwa ni Sept 1, aliamua kuifanya kuwa siku maalum kumuandikia barua ya mapenzi Vanessa, lakini haikuwa barua ya kawaida kama tulivyozoea bali ni barua ya moyo wake kumzungumzia jinsi alivyobadili maisha yake toka wamekuwa wapenzi.
“Tomorrow is my birthday nitaifanya maalum kwa msichana aliye badilisha maisha yangu. Nitaiweka wazi barua ya moyo wangu ambayo huwa naisoma kila siku kwenye nafsi yangu.” Aliandika Jux Instagram siku moja kabla ya birthday yake.
Kupitia kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Fm, Jux akiwa na Vanessa walipata nafasi ya kuzungumzia mengi kuhusu uhusiano wao, na ndipo Jux alipewa nafasi na Diva kuisoma ile barua yake ya moyo kuhusu Vanessa.
Yafuatayo ni mambo sita ambayo Jux aliyasema kuhusu jinsi Vanessa alivyobadilisha maisha yake toka wawe couple.
1. Cha kwanza Jux alisema kuwa toka amekuwa na Vanesa Mdee mwaka 1 na miezi 8 sasa hajawahi kumcheat na msichana mwingine yeyote.
“Vanessa ni msichana wangu ambaye, huu ni ukweli naongea…ni mahusiano yangu ambayo nimekuwa na Vanessa halafu sijawahi kuwa na msichana mwingine yeyote, samahani kwa ma ex wangu nilikuwa nao lakini nilikuwa na maside chicks..Ni msichana ambaye nimekuwa nae na sijawahi kuwa na mwanamke mwingine yeyote kwa muda wa mwaka mmoja na miezi karibia nane.” – Jux
2.Kitu cha pili Jux alisema kuwa Vanessa amekuwa msaada mkubwa sana kwenye muziki wake kiasi ambacho hadi sasa kuna hatua kubwa ambayo ameipiga kutokana na miongozo yake.

“Pili ni msichana ambaye amechangia vitu vingi katika muziki wangu, mwanzo nilikuwa nafanya muziki lakini watu walikuwa wanajua sifanyi muziki serious lakini nilikuwa nafanya serious, nilikuwa nafanya vitu vingi biashara naenda shule, lakini Vanessa ni mtu ambaye alijaribu kunipangia, anajua mi napenda sana pesa nina ndoto nyingi sana, anajua Jux ni mtafutaji anapenda kutafuta pesa, akajua jinsi gani ya kuni approach ili nielewe muziki na nifanye serious..kwahiyo tangu niwe na yeye hata watu wanaweza wakaona kuna vitu ambavyo nimesogea kimuziki , sasa hivi video zangu zinachezwa international, pia nimechukua tuzo…naweza kusema kanibadilishia maisha yangu, maisha yangu namaanisha kimuziki ndio sana katika asilimia 100 asilimia 80 kanibadilishia kwenye muziki.”
– Jux

vanessa na Jux tattoo
3. Cha tatu alizungumzia tattoo walizochora kwenye mikono yao zinanozungumzia mapenzi yao.
“Kuna tattoo ambayo nimechora inasema ‘If not me who…’ na yeye anayo ‘if not now when’? Hata mimi nikiwa peke yangu hii tattoo yangu ina maana kubwa, inanipa nguvu ntakumbuka siku nachora hii tattoo nilikuwa na Vanessa kwahiyo nitazidi kumkumbuka kwenye maisha yangu, sio lazima tuandike jina Vanessa au nani.”-Jux
4.Kitu cha nne Jux amekiri kuwa Vanessa ndiye msichana wa kwanza kumfanya awaze kuingia naye kwenye ndoa pamoja na kufikiria kupata naye watoto, haikuwahi kutokea katika mahusiano yake yaliyopita.
“ Ni msichana peke yake ambaye amefanya nifikirie vitu vingi..nafikiria hata ndoa, engagement, nafikiria watoto, sijawahi kufikiria kwenye maisha yangu, kwahiyo yeye amenifanya nifikirie hivyo kwa vitu anavyo vifanya yaani huyu inabidi awe mke wangu yaani hizo fikra zinaniijia sijawahi kufikiria before, kwahiyo maisha yangu yamebadilika, kwahiyo hata kama baadae atakuwa mwingine huyu atakuwa ndo wa kwanza kunifanya nifikirie hivyo.” – Jux
5.Kitu cha tano Jux alielezea ndoto aliyonayo ya jinsi ya kum engage Vanessa siku watakapokubaliana kufanya hivyo.
“Dreams zangu siku yoyote ambayo atanikubalia nataka nimu engage katika ghorofa moja refu sana duniani kokote litakakokuwepo hiyo ni ndoto yangu” – Jux
6.Mwisho Jux alimaliza barua yake ya moyo kwa kuelezea nafasi aliyonayo Vanessa katika maisha yake kwa kufikiria itakuwaje siku akimkosa.
“Ni msichana ambaye kila siku najiuliza labda sikua atakapokua hayupo kwenye maisha yangu labda tumeachana nitakuwa kwenye hali gani, sijawahi kufikiria nyuma..kwahiyo Vanessa ni mtu ambaye namuhitaji zaidi hata ya mapenzi na kuwa girlfriend wangu…hata kama siku tukigombana natamani awe mshkaji wangu tuendelee, she is very smart ana huruma” – Jux