Wednesday, November 1, 2017
Jinsi ya Kuishi na Mwanamke Asikuloge au Kukupa Limbwata
Nipo tena kwa Mara nyingine katika kubadilishana uzoefu juu ya mambo mbalimbali yanayohusu mahusiano,kuna jambo limekuwa likiniumiza kichwa sana ni swala zima la kulogwa au kupewa limbwata na mwanamke.
Nidhahiri kabisa mambo haya katika jamii yetu yanafanyika kwa baadhi ya wanawake huwa wanawafanyia wanaume,na tatizo hilo limezidi kushamiri zaidi kutokana na ongezeko kubwa la waganga wa kienyeji.
Nimefanya research kwa baadhi ya waganga wameniambia wateja wao wakubwa ni wanawake na shida kubwa wanayokuwa wanahitaji ni kuolewa au kuwadhibiti wanaume zao.
Nami mekuja kugundua wanaume wengi huwa wanafanyiwa madawa ila wakati mwengine mungu huwalinda hawazuriki bila ya wao kujua na wanaume wengi ambao wapo katika hatari hiyo ni wale wenye kipato kidogo ambacho kinarizisha.
Sasa basi nimejaribu kutafuta prevention za ki psychology, ambanzo hazihusiani na mambo ya kishirikina ambazo zinaweza kukusaidia uepukane na janga hilo nimejaribu kutumia experience yangu ni kama zifuatazo:
Kwanza kabisa kama mwanaume unapoanza mahusiano ya kimapenzi na mwanamke unatakiwa umwambie mwanamke vitu ambavyo huvipendi na moja katika ya vitu ambavyo utamwambia hupendi ni mambo ya kishirikina na unatakiwa umsisitizie kwamba endapo kama wewe utagundua yeye anapenda mambo ya kwenda kwa waganga umwambie siku hiyo ndio itakuwa mwisho wa mapenzi yenu.
Jambo la pili ukiwa unaishi na mwanamke ndani usipende kula chakula peke yako hata kama umechelewa kurudi umerudi labda saa sita usiku mwambie mke wako mle wote chakula cause peke yako hujazoea kula au kama mna mtoto wenu ama ndugu wa mwanamke kula nae chakula.
Kwa kufanya hivyo mwanamke atajua hupendi kula peke yako na unampenda yeye na ndugu zake kumbe unalako moyoni unajilinda na limbwata,jambo la tatu pendelea kufanya ibada ukitaka kula na ukitaka kulala na mshirikishe mkeo katika ibada na wakati mwingine msomee maandiko ya vitabu vya mungu ambayo yanakataza ushirikina na adhabu zake watakazo zipata wanaofanya mambo hayo,mengine mnaweza mkaongezea.
Note:Mwanamke anaweza akawa sio mshirikina lakini akashawishiwa na marafiki zake akufanyie hivyo,kwa hiyo kama mwanaume ni bora ukachukua tahadhari mapema.