Saturday, May 5, 2018

Kumfanya Mwanamke Aanze kukubusu au Kukukiss Wa Kwanza

Hatua #1: Mpeleke sehemu ya faragha
Hii haimaanishi kumtoa katika klabu aliyokuwemo, kwa sababu anaweza kukataa kuacha marafiki zake nyuma.
Unaweza kuenda katika sehemu iliyotengwa pembeni ambapo mnaweza kuongea sirini bila kutatizwa. Ama mnaweza kujitenga pamoja (kama mko katika kikundi kikubwa) kwa kumuuliza aandamane na wewe katika baa ama sehemu nyingine kando na hio klabu.
Hatua #2: Hakikisha yuko shwari kuongea, kubanta na wewe kabla hujaendelea zaidi
Kwanza ruhusu dakika chache za kuongea na kujiskia huru kabla ya kuvunja utangamano wenu kwa kujenga tenshen ya mapenzi.
Jambo la mwisho ambalo unataka kwake ni kuona akijutia busu lako, hivyo hakikisha kwanza kuwa anainjoy company yako kabla hujakimbilia hatua yeyote ya ziada.
Hatua #3: Wakati anazungumza kuhusu hoja isio na msingi ama akiwa ana banta, unaweza kuangalia upande aliko na umkate katikati ya sentensi.
Mwambie "Kusema kweli ni kuwa simakiniki na mada unayoizungumza. Kile ambacho nafikiria sahizi ni kukubusu."
Anaweza kushikwa na haya, kunyamaza ama kutojiskia huru, lakini ufunguo hapa ni kuendeleza na maneno haya: " Lakini SITAKI kukukiss kwa sasa kwa sababu unaonekana hauko tayari kwa busu la hakika. Kile ambacho tutafanya ni kufanya mazoezi ya kukiss."
Hatua 4: Pindi utakapo mwambia, mwonyeshe vile inapaswa kufanywa.
Mwambie kuwa atulie na asiingiwe na wasiwasi kuhusu kukuss kwa sababu hautambusu. Mwanzo muahidi kuwa hutamkiss na pia yeye atoe ahadi yake.
Hii ni hatua muhimu - hivyo makinika!
Wakati umeshatoa ahadi yako, mwekee mikono yako kwake na umsogelee pole pole.
Unaweza kuongea na yeye kwa upole lakini uwe unamsogelea karibu hadi midomo yenu iko karibu kugusana halafu pole pole unajisogeza mbali.
Hatua #6: Muulize "Si imekuwa furaha?"
Nafasi kuu hapa ni kuwa umemchangamsha na atataka ujaribu tena.
Kama hakuchangamshwa, unaweza kumuuliza tena mjaribu tena zoezi la kikiss (bila kumkiss kiukweli). Kufikia huu wakati, tenshen itakuwa imejijenga na kila wakati utakapofanya 'zoezi' la kumkiss, ndivyo atazidi kutamani umkiss kiukweli.
Hatua #6: Kama atakukiss, jiachilie umkiss kwa dakika chache halafu kiulaini jivute nyuma na useme haya maneno kidhihaka "ok, imetosha mvunja ahadi"
Baada ya hapo unaweza kubadilisha mada na kuongea mambo mengine, kana kwamba hakuna kitu kilichotokea.
Hatua #7: Baada ya muda, unaweza kujaribu kumuuliza yeye ajaribu tena kufanya mazoezi ya kukiss. Kama wakati uliopita, mwambie akuhakikishie ya kuwa hatakukiss. Mfanye kama alivyofanya awali.
Kufanya hivi mara zaidi kutafikia yeye kukukiss tena, wakati huu ikiwa na ashki zaidi.
So wakati mwingine ukiwa unajiskia kumkiss mwanamke lakini unatatizika fuata hatua hizi saba - na anaweza kukukiss wa kwanza