Monday, April 23, 2018

ZIFAHAMU NJIA TANO ZA KUTABIRI JINSIA YA MTOTO KABLA HAJAZALIWA...

                                                                
jinsia ya mtoto inaweza isiwe muhimu sana kwa mzazi fulani lakini kuna baadhi ya jamii za watu ambao swala la jinsia ni muhimu sana na hufarijika sana wanapopata jinsia fulani japokua hii inaweza kua changamoto kwani mzazi fulani anaweza kutoa mimba akiambiwa mtoto wako ni jinsia fulani. baadhi ya sheria za nchi haziruhusu vipimo vya kutaja jinsia ya mtoto ili kuepusha uwezekano wa kutoa mimba au kumchukia mtoto hata kabla hajazaliwa.huko india inasemekana wanawake ndio wanatoa mahali kwa wanaume hivyo wazazi hawapendi watoto wengi wa kike kwani ni hasara lakini pia hata kwenye jamii zetu baba bila kupata dume haridhiki.kuna njia kadhaa za kuweza kutambua jinsia ya mtoto, baadhi ni uhakika yaani asilimia mia moja na zingine uhakika wake ni kama asilimia themanini kulingana na sababu fulani fulani.zifuatazo ni njia hizo.

kipimo cha picha ya utrasound; hichi ni kipimo kinachotumia mfumo maalumu wa kuangalia ndani ya tumbo la uzazi na kutuma taarifa zake kwenye kioo cha mashine hiyo. kikitumika na mtaalamu mzuri kinasoma jinsia ya mtoto kwa zaidi ya asilimia mia moja.utafiti unaonyesha mimba zinazopimwa kwanzia wiki ya 18 kwenda mbele zinatoa majibu ya uhakika kabisa.
                                                  

maji ya ndani ya kizazi cha mtoto; hii kitaalamu inaitwa amniocentesis and chorionic villus sampling ni kipimo ambacho maji ya mama ya nadani ya kizazi yanachukuliwa na kwenda kupimwa. kipimo hicho hakigundui jinsia tu bali hata magonjwa ya kurithi kama siko seli au ugonjwa ambao unaweza kua umempata mtoto tumboni.
                                                      

uzito wa mtoto; utafiti unaonyesha watoto wa kiume huzaliwa wakubwa na wazito sana ukilinganisha na watoto wa kike hivyo ukiona mimba yako ni kubwa sana kuliko kawaida kuna uwezekano mkubwa wa kuzaa mtoto wa kiume na mimba ndogo mara nyingi huleta watoto wa kike.
                                                

kichefuchefu na kutapika; baadhi ya tafiti zimeonyesha mama anayebeba mtoto wa kike hua anasumbuliwa sana na tatizo la kichefuchefu na kutapika kulilo yule anayebeba mtoto wa kiume, kitaalamu mtoto wa kike hua na homoni kama za mama akiwa bado tumboni huenda ikawa ndio chanzo cha dalili hizi.               
      
    
mapigo ya moyo ya mtoto; kwa kutumia kifaa cha mkononi kitaalamu kama fetoscope nesi au daktari anaweza kutambua mapigo ya moyo ya mtoto aliyeko tumboni. tafiti zinaonyesha katika kipindi cha mimba na mama akiwa hana shida yeyote au haumwi ugonjwa wowote mapigo ya moyo ya mtoto  wa kike ni zaidi ya 140 kwa dakika wakati wa kiume ni chini kidogo ya 140.
                                                        

mwisho; tafiti hizo zinaweza zisiwe asilimia mia moja kulingana na sababu mbali mbali kwa mfano mapigo ya moyo ya mtoto huweza kwenda mbio sana kama mama anaumwa au tumbo linaweza kua kubwa sana sababu ya unene wa mto binafsi lakini zimeonyesha uhalisia kwa asilimia kubwa huku kipimo cha picha ya utrasound na maji ya uzazi vikiwa vya uhakika kabisa.sijaandika makala hii ili utoe mimba kwa sababu zako binafsi. sheria inakuona.