Wednesday, April 11, 2018

Mambo matatu makuu yanayowapa wanaume udhaifu kitandani

Unhappy-couple
Ni kitu kinachofahamika kutokana na utafiti kuwa wanawake wengi hawaridhishwi kihisia kwasababu utendaji wa wanaume wengi kitandani umepungua.
Haijalishi unampa nini mkeo au mpenzi wako, kama huwezi kumridhisha, ataendelea kutokuwa na furaha, mlalamikaji na wakati mwingine kama akijaribiwa nje, huenda akajaribu bahati yake kwingine.
Tena kama mpenzi wake kabla ya kuolewa alikuwa akimtosheleza, usishangae akamtafuta kokote aliko kukumbushia (hata kama hana lolote).
Wakati mwingine wanawake hufeki maneno matamu ya pongezi ili tu kukupa moyo kuwa umefanya kazi nzuri. Cha ajabu hii imewafanya wanaume wengi kuboresha game yao na kujiamini.
Kipi kinachowapa udhaifu wanaume?
1. Kejeli kutoka kwa wanawake wao
Wanawake wengine hulalamika kiasi cha kuwaambia wapenzi wao bila kuficha kuwa hawana lolote kitandani. Katika hali hii, wanaume hujisikia aibu kiasi cha kupoteza kujiamini kwao. Hii inaweza kuwafanya wengine kuanza hata kuchelewa kurudi nyumbani kuepuka fedheha.
2. Uoga wa kumaliza haraka
Kufika kileleni haraka hutokea pale mwanaume anapoutua mzigo mapema wakati wa kufanya mapenzi kabla ya kumridhisha mwenzake. Wanaume wengine hupania na kuwa na wasiwasi. Hii inaweza kupelekea kumaliza haraka hara kabla mwanamke hajaridhika.
3. Upungufu wa nguvu za kiume
Utafiti unaonesha kuwa takriban wanaume milioni 30 duniani huathirika kila mwaka na tatizo hili. Hii ni hali ambayo uume husinyaa wakati wa tendo la ndoa na kupunguza ugumu unaohitajika. Tatizo hili hukosesha raha na husababisha msongo wa mawazo.