Tuesday, April 24, 2018

LIFAHAMU TATIZO LA KUKOSA USINGIZI NA SULUHISHO LAKE.

tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 9 mpaka 15 ya binadamu duniani wanasumbuliwa na matatizo ya kukosa usingizi, tatizo hili ni moja ya matatizo mabaya sana ambayo huweza kumfanya mtu ashindwe kutambua anaishi ulimwengu wa aina gani kwani muda mwingi anakua ni mchovu na hawezi kufanya kitu chochote kwa umakini.
ugonjwa wa kukosa usingizi huwasumbua zaidi watu wazima kwanzia miaka 40 kwenda mbele hasa wanawake kuliko wanaume japokua unaweza pia kuwashambulia vijana wadogo kulingana na matatizo mbalimbali lakini watu wazima sana ndio waathirika wakuu wa shida hii.

kuna aina tatu za matatizo ya kukosa usingizi
kukosa usingizi kunaweza kuja kwa aina tatu yaani kukosa usingizi ghafla, kukosa usingizi mara moja moja au kukosa usingizi kwa muda mrefu sana.
hali hii ya kukosa usingizi husababisha matatizo mbalimbali kama kunenepa,kupoteza kumbukumbu, kushindwa kufaulu darasani, kushindwa kua makini na kazi, kuchoka sana,wasiwasi, mgandamizo wa mawazo, na hatari ya kupata magonjwa yasiyotibika kama ugonjwa wa presha na kisukari.

nini husababisha kukosa usingizi?
watu sababu mbalimbali huweza kukosa usingizi kama ifuatavyo
mabadiliko ya mfumo wa maisha; hii inaweza kusababishwa na kazi unayofanya kama kuanza kufanya kazi usiku...kazi za ulinzi, kazi za uuguzi, na kadhalika lakini pia kuishi sehemu yenye kelele sana,kusoma sana usiku, baridi sana au joto sana.
matatizo ya kisaikolojia; watu wenye msongo wa mawazo unaosababishwa na matatizo mbalimbali kama kukosa ajira, matatizo ya kiuchumi, kuvunjika kwa mahusiano, magonjwa ya akili, kua na wasiwasi sana wa mambo yanayokuja, wasiwasi wa kuibiwa mali zako ukiwa ndani umelala hasa wamiliki wa magari na mali zinazolala nje.
magonjwa mbalimbali; kuugua magonjwa fulani fulani huweza kumfanya muhusika kukosa usingizi kabisa wakati wa kulala mfano pumu au asthma, magonjwa ya moyo, maumivu makali ya sehumu ya mwili,kiharusi, madonda ya tumbo, maumivu ya jino, na kansa mbalimbali.
mabadiliko ya kiwango cha homoni; hii hutokea wakati wa kipindi cha hedhi ambapo kunakua na mabadiliko madogo ya homoni za uzazi, kipindi cha ujauzito na ugonjwa wowote unaobadilisha kiwango hicho.
teknolojia; kulala na simu na kuendelea kuchati, tv au komputa chumba cha kulala,michezo ya gemu na kadhalika..hii imeathiri sana watu wengi kwani siku hizi kabla ya kulala utamkuta kila mtu anachezea simu angalau saa moja.
dawa mbalimbali; kuna dawa nyingi sana ambazo zimetajwa kunyima watu usingizi kama ifuatavyo
dawa za presha mfano propanolol,metoprol,losartan,atenolol,metoprol, captopril,enapril na solatol,lisinopril
dawa za msongo wa mawazo mfano fluoxetine na paroxetine
dawa za kushusha kiwango cha lehemu mwilini mfano simvastatin,rosuvastatin,lovastatin.
dawa za kupunguza maumivu ya mifupa mfano chrondotin na glucosamine
dawa za kutibu aleji mfano cetrizine
sababu zingine mfano kulala sehemu yenye kelele nyingi, kulala na mtu anayekoroma usiku, kulala sehemu yenye wadudu kama mbu na chawa

watu gani hasa wanasumbuliwa na shida hii?

  • watu wanaosafiri sana
  • watu wanaofanya kazi za usiku
  • wazee sana
  • wanaotumia dawa mbalimbali
  • vijana wadogo ambao mahusiano na ajira ni tatizo kubwa kwao.
  • wanawake waliofika mwisho kuona siku zao za hatari
  • watu wenye magonjwa ya akili
dalili za kukosa usingizi ni kama ifuatavyo..
  • kushindwa kulala kabisa
  • kuamka usiku sana na kukosa usingizi
  • kuamka mapema sana kuliko kawaida
  • kusikia usingizi baada ya kuamka asubuhi
  • kuchoka sana mchana wakati wa kazi
  • mgandamizo wa mawazo na kua na wasiwasi sana
  • kukosa umakini wakati wa kazi
  • kupata ajari za wakati wa kutumia vyombo vya usafiri.
  • kuumwa kichwa sana
  • kuharisha, kichefuchefu na kukosa hamu ya chakula
  • kushindwa kuongeza na watu
vipimo vinavyofanyika
daktari humuuliza mgonjwa mbalimbali kuhusu tatizo lake la kukosa usingizi, vipimo mbalimbali pia huweza kuchukuliwa pia kutafuta magonjwa ambayo yanaweza kumkosesha mtu usingizi.
kwa mtu kugunduliwa na tatizo hili lazima awe amemaliza mwezi mmoja bila kupata usingizi unaoeleweka
vipimo vya kisasa zaidi kama polysmonography huweza kutumika kwa mgonjwa aliyelazwa kupima usingizi wake wakati wa usiku
matibabu;
mara nyingi matatizo ya kukosa usingizi hua yanaaisha pale chanzo cha tatizo kinapotibiwa kwa mgonjwa husika, hivyo mara nyingi matibabu yanalenga kuondoa chanzo cha tatizo hili.
matibbu yamegawanyika katika matibabu yasiyohusu dawa yaani non pharmacological treatment na matibabu yanayohusu dawa yaani pharmacological treatment kama ifuatavyo
matibabu yasiyohusu dawa[ non pharmacological treatment]
ongeza nidhamu ya usingizi; epuka kulala sana au kidogo sana, epuka kulala na njaa, epuka kunywa kahawa na kuvuta sigara wakati wa kulala, hakikisha ratiba yako ya kulala haibadiliki, hakikisha unalala kwenye mazingira rafiki ya usingizi yaani bila kelele au usumbufu wowote.
muone mtalaamu wa ushauri; unaweza kuonana na mshauri akakusaidia kutatua tatizo lako la kisaikolojia linalokusumbua, huduma hiyo tunatoa pia.
epuka vitu mambo ya teknolojia yanayozuia usingizi; tabia ya kua na tv chumba cha kulala, laptop kitandani au kutumia simu usiku kabla ya kulala huweza kukunyima usingizi.
epuka kulala mchana; tabia ya kulala mchana huweza kukunyima kabisa usingizi wakati wa usiku, hivyo kaa mbali kabisa na kitanda wakati wa mchana.
pata matibabu ya tatizo lolote la kiafya linalokusumbua; kama kuna ugonjwa wowote unakusumbua hakikisha unatibiwa, kama ni ugonjwa usiotibika basi hakikisha unafuata matibabu ya kupunguza makali yake.
pata suluhisho la tatizo la kisaikolojia;kama una msongo wa mawazo sababu ya kuachwa kwenye mahusiano huwezi kulala kabisa, kama una matatizo ya kiuchumi, umefiwa, au msongo wowote wa mawazo basi hakikisha unapata suluhisho lake.
matibabu ya dawa[pharmacological treatment]
wakati mwingine chanzo cha kukosa usingizi kinaweza kua nje ya uwezo wa muhusika yaani hawezi kutatua tatizo linalomsumbua hivyo anahitaji matibabu ya dawa ambazo angalau zitampa usingizi alale kama ifuatavyo
ant depressant; mfano fluoxetine na paroxetine
anthistamine
ramelteon
melatonin