Thursday, April 26, 2018

HIZI NDIO SABABU KUMI KWANINI WANAUME HUFA MAPEMA KULIKO WANAWAKE.

                
ukifanya utafiti wako binafsi utagundua bibi wako wengi duniani kuliko babu lakini pia wanaume kwa kila umri ni wachache kuliko wanawake...unaweza ukadhani labda wanawake wanazaliwa wengi lakini hiyo sio hoja kuu. wanaume wanazaliwa wachache kuliko wanaume ni kweli lakini hufa mapema kuliko wanawake na kuwafanya waonekane wachache zaidi duniani. kuna tafiti nyingi zimefanyika lakini haya ni baadhi ya majibu yaliyopatikana.

wanaume huhatarisha sana maisha yao; ubongo wa mbele wa binadamu unaotufanya tufikiri, tusome na kutoa hukumu unakua taratibu sana kwa wanaume kuliko wanawake, hii inawafanya katika ile hali ya utoto kufanya vitu vya hatari mno bila kuogopa.watoto wa kiume ni wasumbufu na hawasikii.kukimbiza baiskeli, kuogelea na kujaribu kila kitu..wakishakua kidogo wanaume huanza kunywa pombe kali sana, kuvuta sigara, bangi na madawa ya kulevya na kuanza kuugua magonjwa ya kutisha.

wanaume wana miili mikubwa kuliko wanawake; kitaalmu katika biolojia viumbe vyote vyenye miili mikubwa hufa haraka kuliko vile vyenye miili midogo hii ni kwasababu ya mifumo inayofanya kazi kuendesha miili hii kuchoka mapema katika maisha lakini pia hatarini kushambuliwa na magonjwa au ajari mbalimbali.

wanaume wanafanya kazi hatarishi zaidi; majeshi yote duniani, machimbo yote ya madini na viwanda vikubwa huwatumia wanaume kwani wana nguvu sana na wana uwezo wa kuvumilia hali ngumu. kazi hizo ni hatari sana kwa maisha ya binadamu.

hali ya kujiamini sana; sio rahisi mwanaume kukubali kushindwa kupigwa na mtu fulani na mara chache sana mwanaume anaweza akaugua na kwenda hospitali, wengi hujikausha na kwenda hali ikiwa mbaya kabisa.

wanaume wanajiua sana kuliko wanawake; wanawake utawasikia wanasema tu kwamba ipo siku ntajiua lakini mwisho wa siku hawafanyi hivyo. lakini mwanume ukimsikia anataka kujiua toa taarifa mapema apate msaasa kwani atajiua kweli.

dunia haiwajali sana; kesi za wanaume kupigwa na wake zao sio muhimu sana kwenye jamii lakini wapo waliopigwa mpaka kufa, lakini pia kwenye matatizo yeyote ya magonjwa ya kulipuka au ajari basi watoto na wanawake ndio hupewa kipaumbele. historia inaonyesha wakati meli ya titanic inazama zaidi ya  miaka 100 iliyopita wanawake na watoto ndio waliokolewa sana.

wana msongo sana wa mawazo; dunia nzima inajua wanaume ndio wanaohusika kwa malezi ya familia yaani gharama za kuendesha familia. leo hii hata kama baba na mama wanafanya kazi basi ikitokea watoto wamelala njaa basi atalaumiwa mwanaume lakini pia migogoro ya mke wake na mama yake mzazi au dada zake inamuweke sehemu ngumu sana achague nani amuache nani. hii huweza kuleta magonjwa ya moyo na presha na kumletea kifo mapema.

wanaume ni wagomvi sana; huenda sababu ya wingi wa homoni ya testosterone kwenye damu zao, wanaume wanapigana sana kuliko wanawake na hii huwaweka kwenye hatari ya kuchomwa visu au risasi na kufa.

ni walengwa wa matukio yote hatari; ukitaka kuvamia sehemu yeyote kama jeshi au mashambulio ya kigaidi lazima ujue wanaume wako wangapi na hao ndio ukiwaua utafanikiwa kuchukua hiyo sehemu na bila hivyo haitawezekana.

wanakosa matibabu mazuri; sera za afya za nchi nyingi zinawalenga wanawake zaidi kuliko wanaume ndio maana utasikia matibabu kwa wanawake na watoto bure lakini wapo wanaume wengi wasio na uwezo wa kugharamia hizo gharama na hufia majumbani kwao.