Thursday, April 26, 2018

HIVI NDIVYO KISONONO KINAVYOSABABISHA UGUMBA KWA WANAWAKE NA WANAUME.[GONORRHEA]

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiwHJFXY5YazW42bWcihMQ396hmP8XBcaM4YSABxoI0axeevZCNNDuYrj_fU12LGwqlhzk475vcj1OhYu7WXBa89sQ-3HGMqciiJGhZWhKBJiQ2UhJaEgAICM10_ZD_OUhEpDYRheqdKCFY/s1600/nejm199307153290306_f1.jpg
kisonono ni nini?
kisonono ni ugonjwa wa njia ya uzazi kwa wananawake na wanaume ambao mara nyingi huambatana na kutokwa na usaa sehemu za siri.kisonono kinafahamika kama classical sti kwani iliinza kabla hata ya kuanza kwa ugonjwa wa ukimwi.

kisonono ni moja ya vyanzo vikuu vya utasa na ugumba kwa wanawake na wanaume na umeonyesha kupunguza sana idadi ya uzazi kwa jamii nyingi duniani.
ugojwa wa kisonono husababishwa na bacteria kwa jina la kitaalamu kama naisseria gonorhoea, bacteria hawa hawawezi kupita kwenye ngozi ya kawaida kama ya mkono au mguu na hupendelea ngozi laini kama ya uke, ngozi ya ndani ya kichwa cha uume, ngozi ya mkundu, ngozi ya macho na ngozi ya ndani ya mdomo.
ugonjwa huu husambazwa kwa njia ya kufanya ngono lakini pia watoto huweza kuambukizwa wakati wa kuzaliwa kutoka kwa mama mwenye kisonono.
hatari ya mambukizi baada ya ngono ni asilimia 20 mpaka 35 kwa wanaume na asilimia 60 mpaka 90 kwa wanawake.
dalili za ugonjwa huu huanza siku ya 2 mpka siku ya kumi baada ya kufanya ngono.

dalili za ugonjwa wa kisonono kwa wanaume.

  • kuwaashwa ndani ya njia ya njia ya mkojo
  • maumivu makali wakati wa kukojoa.kutokwa na usaa kwenye uume
  • kukojoa mara kwa mara na kushindwa kuzuia mkojo
  • kutoa mkojo wenye damu
  • mgonjwa asipotibiwa usaa huanza kupungua au kuisha kabisa lakini ugonjwa unakua umehamia ndani na hii ni hatari zaid.
dalili za kisonono kwa wanawake
asilimia 50 mpaka 80 ya wanawake hawana dalili kabisa na ndio maana ugonjwa huu unaweza kumfanya mwanamke akawa mgumba .
wakati mwingine usaha huweza kutokea kwenye mlango wa uzazi bila kuonekana nje
wanawake wengi hugundua walikua na ugonjwa huu baada ya kupata madhara yake kuonekana kama kushindwa kupata mtoto.

madhara ya kisonono wa wanaume

  • njia ya mkojo kuziba
  • majipu ndani ya njia ya mkojo
  • mkojo kujaa ndani ya kibofu
  • utasa na kushindwa kuzaa

madhara ya kisonono kwa wanawake.

  • ugumba
  • magonjwa ya njia za uzazi.
  • mimba kutungwa nje ya kizazi.

vipimo vinavyotumika..
usaha unaotoka huchukuliwa kwenye uume wanaume na ndani ya uke wa mwanamke na kupimwa maabara kuhakikisha kuwepo kwa ugonjwa huu.

matibabu
dawa mbalimbali zinaweza kutibu kisonono lakini kwa muongozo wa sasa wa wizara ya afya mchanganyiko wa dozi ya doxycline na ciprofloxacin kwa muda wa siku saba hutumiaka zaidi. kwa mama mjamzito au kwa ambaye ameshindwa kupona kwa dawa nilizotaja hapo juu sindano moja ya cefriaxon 250mg inatosha kabisa kumaliza ugonjwa huu.dawa za ciproflaxin na doxycline ni marufuku kwa wajawazito.

sababu za kushindwa kupona kwa wagonjwa wengi wa kisonono

  • kutoa dawa kidogo ukilinganisha na uzito wa mgonjwa
  • kutoa dawa za kisonono wakati ni ugonjwa mwingine unaofanana.
  • baadhi ya dawa kushindwa nguvu na bakteria wa kisonono
  • kutomtibu mpenzi husika wa mgonjwa na kusababisha maambukizi mapya.
  • kutomaliza dozi

jinsi ya kuzuia ugonjwa wa kisonono

  • kutoshiriki tendo la ngono kabisa
  • kuvaa condom kwa uhakika
  • epuka kua na wapenzi wengi
  • mpenzi wa mgonjwa lazima atibiwe hata kama hana dalili
  • kua na mpenzi mmoja muaminifu...