Thursday, April 26, 2018

FAHAMU JINSI YA KUKABILIANA NA MAUMIVU YA KIFO CHA MPENDWA WAKO...

kifo ni hali ya kawaida katika safari ya mwanadamu hapa duniani, tangu dunia imeanza mabilioni ya watu wameshafukiwa kwenye hii ardhi yetu. kimsingi kila baaada ya miaka 100 kizazi kinabadilika kwa maana nyingine baada ya miaka 100 kwanzia leo sisi wote tutakua wafu na kutakua kuna watu wapya kabisa.pamoja na historia fupi hiyo ya kifo bado hakuna mwanadamu ambaye amekizoea kifo kwani kila anayekufa kibinadamu hatutamuona tena. huu ni ukweli mchungu ambao mpaka leo hii binadamu tumeshindwa kuumeza.hata kama kuna maisha baada ya haya kama vitabu vitakatifu vinavyosema bado uwezekano wa kuonana ni mdogo kutokana na masharti magumu ya kuona pepo kama inavyosemwa.hivyo kama wewe ni mzima leo una wazazi na wote wawili lazima ujue ipo siku watafariki na itabidi ukabaliane na ukweli.
kumpoteza mpendwa wako huambatana na maumivu makali sana ambayo hayaponi kirahisi na kwasababu kila binadamu yuko tofauti basi pengo lake haliwezi kuzibika kabisa.kuna watu walichanganyikiwa, kuugua hata kujiua baada ya kuwapoteza ndugu zao. hatuwezi kuwalaumu lakini kila mtu ana njia yake ya kupokea habari mbaya.leo hii naenda kuzungumzia mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kuendelea na maisha yako baada ya kifo cha mpendwa wako.

ziachie hisia zako; usijibane kulia, unyesha hisia zako zote kipindi cha msiba  na baada ya msiba, kwani kulia sana hupunguza uchungu moyoni.kwa hiyo kama una maneneo ya kuomboleza au una uchungu mwingi..ongea maneneo hayo na ulie kadri uwezavyo.kumbuka kwamba hisia ni zako na sio kosa kuzionyesha.

acha hatua za maombolezo zipite;mwandishi elizabeth kubler kwenye kitabu chake cha ''on death and dying'' alielezea hatua tano za majonzi ambazo kila mtu anazipitia baada ya kifo cha mpendwa wake kama ifuatavyo.

  • denial/kukataa; hii ni hatua ya kwanza kabisa ambapo ukipewa habari hizo hautaamini kabisa na utabaki na ganzi ya muda fulani ukihisi labda ni utani au wamekosea kutoa habari.
  • anger/hasira; baada ya muda utagundua ni kweli, utapata hasira sana na kuanza kulaumu watu unaohisi wamehusika. labda kumlaumu dokta kwa kushindwa kumtibu mgonjwa wako, kumlaumu marehemu kwa kukuacha hata kumlaumu mungu.
  • bargaining/kubembeleza; katika hatua hii mtu huanza kuongea na mungu au nguvu za giza labda kwenye maombi au kuongea mwenyewe akiomba ikiwezekana huyo mtu arudishiwe uhai. watu wengine wamefikia mpaka kwenda kwa waganga wa kienyeji wakiamini wafu wao wamerogwa.
  • mgandamizo wa mawazo; hichi kipindi cha msongo mkubwa wa mawazo ambapo mfiwa anakua ametulia sana huku akihisi maumivu makali sana moyoni mwake na mfiwa asipoangaliwa kipindi hiki anaweza kujiua pia.
  • acceptance; hii hali ya mwisho kabisa ya hatua hizi ambapo mtu hukubali ukweli kwamba nimeshampoteza mtu na maisha huanza kuendelea kama kawaida, ni hatua ambayo inapatikana baada ya muda kadhaa kulingana na majonzi ya mtu.
omba msaada; usikae peke yako, ongea na ndugu jamaa na marafiki na wao watakupa moyo sana kulingana na uzoefu wao kwenye swala hilo pia unaweza ukamuona mtaalamu wa ushauri akausaidia jinsi ya kuendelea na maisha yako.
kaa mbali na kumbukumbu za marehemu kwa muda; kama ulikua karibu sana na marehemu kama mke, mume au mtoto basi kusanya vitu vyake vyote uweke sehemu moja usivione kwa kipindi hiki kigumu lakini pia unaweza ukachukua likizo ukasafiri kidogo kwenda maeneo mapya ambayo hukuwahi kwenda na mtu huyo na kama ulikua unaishi naye kwenye nyumba fulani ya kupanga basi unaweza kuhama kabisa eneo hilo kupoteza kumbukumbu.
jipe muda; mambo yote niliyoyataja hapo juu hata ukiyafanya kwa siku mbili bado maumivu makali yatakuepo, unatakiwa kujua kwamba maumivu haya yanataka muda... wazungu wanasema time heals everything. kuna watu kama wewe ambao wameshapoteza watu muhimu sana kama wewe lakini baada ya muda fulani walizoea.
                                               

mwisho; maisha na zawadi kutoka kwa mungu, tumia muda mwingi kuwaonyesha upendo watu wote unaowapenda na usiowapenda kwani siku za kuishi ni chache sana kuliko unavyofikiri na baada ya kifo familia  na rafiki watakumbuka upendo na muda uliotumia ukiwa nao kuliko pesa ambazo unatumia muda mwingi kuzitafuta..