Tuesday, March 27, 2018

Soma simulizi fupi ya kusisimua "Usimdharau usiyemjua undani wake"

Msichana mmoja alikuwa amempenda
kijana mmoja mtanashati na mcha
Mungu.. Malengo yao ilikua waje kuoana
baada ya muda.
Kijana huyu alijitoa sana kwa binti huyu
hadi wenzie wakamuona mjinga, lakini
ukweli ni kuwa alimpenda msichana yule
kwa dhati. Alimtafutia kazi alipomaliza
chuo, alimshauri kuhusu mipango ya
maisha na alikua akimuombea kila
alipopata nafasiya kuomba.
Siku moja binti alikua anasherehekea siku
yake ya kuzaliwa...hivyo akaalika marafiki
zake, na watu wengine muhimu akiwemo
mpenzi wake.
Wageni wote walifika kwa wakati isipokua
yule kijana alichelewa kidogo... Hivyo
msichana akatumia muda ule ambao
mpenzi wake hajafika kuwaeleza wageni
namna yule kijana alivyokua wa muhimu
kwake..
Akamsifia sana, akasema atamvalisha
pete ya uchumba soon, na akasema siku
hiyo ya birthday yake anategemea zawadi
kubwa sana kutoka kwa huyo mpenzi wa
nafsi yake.
Baadae kijana akaingia na kuketi high
table.. Muda wa zawadi ulipofika watu
wakamtunza binti zawadi mbalimbali na
kijana akawa wa mwisho... Hivyo wageni
wote wakawa na hamu ya kutaka kujua
zawadi aliyoleta hasa baada ya yule
msichana kumsifia sana.
Kijana akaamka na kutoa mfuko.. kila mtu
akataka kujua kilichokua ndani ya
mfuko..mara kijana akafungua mfuko na
kutoa mkate..!!
Lahaula... watu wote wakastaajabu..
mkate??? Lakini kabla hajasema lolote
kuhusu ule mkate, yule msichana akaanza
kulia.. akapandwa hasira kwa kuwa
mpenzi wake amemuaibisha..!!
Akiwa analia kwa kwikwi, akamkwida shati
na kumvua tai yake, akamwagia juisi,
kisha akauchukua ule mkate na
kuutupa.!!
Maskini..yule kijana akaukimbilia ule
mkate na kuuokota.. Kisha akarudi high
table na kusema "baby nakushukuru kwa
yote..Huenda umenidharau kwa kuwa
nimekuletea zawadi hii ndogo kwenye
siku yako muhimu kama hii. Lakini kama
ungetambua thamani ya zawadi hii,
usingefanya haya.."
Kisha akafungua ule mkate na kutoa vitu
viwili alivyoficha ndani ya mkate.. Kwanza
akatoa ufunguo wa gari, ambalo alikuwa
amemnunulia mpenzi wake na alitaka
amkabidhi siku hiyo ya birthday.
Kisha akatoa pete ya uchumba na kusema
"Nilimuomba Mungu anipe mwanamke
atakayenipenda katika hali yoyote.
Nilipanga leo nikuvalishe pete hii ili
kuelekea ndoto yetu ya ndoa..
..Lakini kwa kuwa uliangalia nje, uliona
mkate, badala ya pete hii ya thamani
iliyokua ndani.. Naamini mwanamke
niliyemuomba kwa Mungu bado
sijampata.. Nashukuru kwa yote
uliyonifanyia, nimekusamehe, nawe
naomba unisamehe kama nimekukwaza.."
Kisha akachukua mkate wake, huyoo
akaondoka. Msichana akaomba msamaha
lakini ilikua too late..
MORAL OF THE STORY..!
Usidharau kitu/mtu kwa kumtizama nje..
Mungu huangalia thamani ya kitu ndani
lakini Wanadamu huangalia nje.. Thamani
ya kitu/mtu ipo ndani na si rahisi
kuonekana..
Usiwe mwepesi wa kuhukumu kwa
kutizama umbo la nje.. Wale
wanaokudharau leo na kukuona mkate,
ipo siku watagundua haukua mkate wa
kawaida... kuna vingi vya thamani ndani
yako.
Wote wanaokudharau leo ipo siku
watakusalimia kwa heshima..!!
🌹TUELIMISHANE MEMA🌹 

Subra ndio inayotakiwa