Kwa asilimia miamoja watu wengi wanaofanya mapenzi kwa kuiba katika maeneo kama ya ofisini huwa hawakumbuki kuvaa kinga kutokana na mihemumko mikali na ya haraka kuliko kawaida wanayokuwa nayo kwa wakati huo. Ni vyema kujihadhali ma mihemuko hii kwani madhara yake ni makubwa.
Kumbuka unapaswa kuishinda faragha yako na kujitambua kuwa hupaswi kufanya mapenzi na mke wa mtu au mume wa mtu. Unapoona vishawishi kama hivi jaribu kuwa bize na kazi, chukulia poa tu japokuwa wadada wengi huwa na njia mbali mbali za kukufanya ukanasa kirahisi kwa mfano kama mnakumbuka skendo ya Monica Lewinsky na aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo walichokifanya ofisini na baadae kuja kuwa ni skendo kubwa sana.Hasara ya mapenzi hayo ya kiwizi wizi katika masaa ya kazi ni kupata maambukizi ya Ukimwi bila kufahamu kwani utakuwa umemzoea mfanyakazi mwenzio kwa jinsi alivyo smati katika kazi, hivyo hutafikilia kama anawatu wengine nje ya kazi. Pia kuna maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ambayo kwa wanawake hujificha kwa muda kabla ya kuonekana haraka kama wanaume.