Monday, March 26, 2018

Kujitibu Vipele vya Chunusi Kwenye Uso Kwa Njia za Asili Tiba Mbadala

Kuna  idadi  kubwa  ya  watu   wanao  kabiliwa na  tatizo  la   vipele vya  usoni

(  Chunusi  ). Kuwa  na  chunusi  ni  jambo lenye  karaha  sana,  kwani  linakufanya upoteze  mvuto  wako  wa  asili  na  hivyo kukukosesha  raha.

Zipo  njia mbalimbali   za  asili  zinazo  weza kutumika  kutibu  tatizo  la  chunusi  na  vipele vya  usoni.

 Ifuatayo  ni  miongoni  mwa  njia   bora kabisa  na  ya  uhakika  itakayo  kusaidia kuondokana  na  tatizo  la   Chunusi  au  vipele kwenye  uso.


Komamanga:  Maganda  Ya   Mkomamanga  yaliyosagwa, yakichanganywa  na  habbat  sodah  ya unga, hutengeneza  dawa  nzuri  ya  asili  ya  kuondoa  tatizo  la  vipele  vya  usoni  (  chunusi  )


Habbat Soda : Hii  ni Habbat Sodah Ya Mbegumbegu. Habbat  Sodah  iliyosagwa  ndio  inayo hitajika katika kutengeneza   dawa  ya asili  ya  kuondoa  tatizo  la  vipele  vya  usoni  ama chunusi.

MAHITAJI :
Habbat  Sawdah  ya  Unga  iliyo sagwa.
Nusu  kikombe  ya  maganda  ya komamanga  yaliyo  sagwa.
Nusu  kikombe  ya  siki  ya tofaha(apple )

MATAYARISHO   NA MATUMIZI 
Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu)
kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple).

Paka katika sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila  siku  usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubarid.

NJIA HII IMETUMIWA NA WATU WENGI NA IMEWASAIDIA SANA. JARIBU NA WEWE KUTUMIA NJIA HII UONE MAFANIKIO YAKE.
Kwa  habari  na  taarifa  mbalimbali  kuhusu masuala  ya  tiba zitokanazo  na  dawa  za mimea  na  vyakula lishe