Sunday, March 25, 2018

Jua namna na nini cha kuongea wakati wa utongozaji, ili kumtongoza mwanamke kwa mafanikio zaidi.

Jua namna na nini cha kuongea wakati wa utongozaji, ili kumtongoza mwanamke kwa mafanikio zaidi.
"Ulishawahi kujikuta unatamani kumtongoza msichana mzuri sehemu flani japo upate namba yake ya simu ila unajikuta huna jinsi yeyote au wazo juu ya nini cha kufanya au kuongea, unatamani kumfata nguvu miguuni zinakua zimekuishia unashindwa hata kupiga hatua moja kumsogelea, lile wazo pekee la kutaka kumsogelea linakufanya moyo uwende mbio, mikono iloane na jasho jembamba kukutoka huku akili yako ikishindwa kufikiria vizuri nini cha kuweza kuongea iwapo ukimsogelea?."
Leo tunaangalia mwendelezo wa mada ya jinsi ya kutongoza ni ngumu, ila kwa mjuzi wa kutongoza hufuata njia hizi, Unajua nini?, haipaswi kuwa hivi ndo maana kiumeni.com ipo kwa ajili yako ili kumaliza maswala madogo madogo kama haya, kukuondoa katika mazingira ya kutokua na maamuzi dhabiti na kutokujua nini cha kufanya ndani ya sekta ya utongozaji na kukufanya uwe mwanaume kiongozi na mtanashati kwa kujua ni nini cha kufanya na mda gani unapaswa kukifanya ili kuwa mtaalamu katika sekta ya mahusiano.
Kujiamini ni kitu kinachochukua nafasi kubwa na ndo msingi mkubwa katika mahusiano na hasa wakati wa utongozaji, na ndicho kitu mwanamke hutumia kumpima mwanaume na kumpa nafasi ya uwezekano wa kuwa na yeye au la, ila mara nyingi mtu hushindwa kujiamini kutokana na hofu ya kutokujua ni nini cha kufanya au kuongea wakati wa utongozaji.
Mwanamme ambaye huwa hafanikiwi kwenye utongozaji hufanya makosa madogo madogo kama kumpandisha hadhi mwanamke anayemtongoza mpaka kiasi ambacho anaifanya hadhi yake binafsi kuonekana ndogo na siyo tu anamtongoza mwanamke kwa wasiwasi na kutojiamini, bali anamtongoza hovyo hovyo bila mpangilio na zaidi ya hapo anamuweka wazi mwanamke kwamba anataka kumjua zaidi ya kawaida na anajitangaza bila kujijua kwamba, anahitaji na huyo mwanamke apendezwe naye hapo hapo.
Nayajua haya kwa sababu kwa muda mrefu na mimi nilikua hivi hivi, mtaalamu wa utongozaji huwa anasubira na huwa hapaparuki hovyo hovyo tu, kutongoza ni sanaa na inahitaji uelewa mkubwa na hata mimi iwapo ningelikua ndo huyo mwanamke sidhani kama ningelikubali hivi hivi, lazima atake kukujua kwanza ndo mambo mengine yafuate.
Ukitaka kuishia kusonywa na matusi juu ingia na mstari wa "Dada samahani nimetokea kukupenda nataka tuwe wote, kila nikikaa nakuwaza wewe, nikinywa maji nakuona kwenye glasi", bila kuangalia mazingira na papara za kusema yaliyo moyoni mwako, huu mstari lazima utakutokea puani, mwanadada ndo amekuona siku hiyo hiyo, hata alikua hajui mtu kama wewe upo katika hii dunia, hakujui na unategemea akuambie anakupenda pia, we vipi?, hapo unapoteza nafasi na utaishia kuambiwa usiyoyataka na kuumia moyo tu.
Naamini kabisa mwanaume yeyote mwenye mtazamo sahihi na mwenye hamu ya kujifunza anaweza kuelewa jinsi ya kutongoza mwanamke sehemu yeyote na mahali popote pale, kutongoza hakuitaji kukalili mistari ya kutongozea wala kumpulizia dawa kutoka kwa mganga, kama unania ya kujifunza endelea kusoma nakala za waulizewanaume.
Mwanaume mtongozaji hajishushi na anatumia mbinu ya kuonyesha ujasiri wa kimaongezi na akiongea na mwanamke, mwanamke hutambua ya kuwa huyu jamaa ana nia naye kutokana na lugha anayoitumia wakati wa maongezi.
Makosa makubwa mawili ambayo nilikua nafanya wakati wa kutaka kumtongoza msichana, moja nilikua nasubiri na kusita kwa muda mrefu mpaka nakuta mwana si wangu tena na pili kutojua nini cha kuzungumza iwapo nikimsogelea karibu huyo mrembo.
"Unakuwa na dakika tatu kutoka unapomuona msichana anayekupendeza na mpaka pale utakapomsogelea na kuanzisha mazungumzo yanayompendeza, ukisubili sana nafasi yako itakupita kama upepo na kupoteza nafasi hiyo muhimu".
Kama ni kwenye sherehe ndipo ulipomuona, piga moyo konde na mwendee na mwambie,
>>"Nimekuona kutoka mbali ila moyo wangu ukang'ang'ania mpaka nije nikusalimie, mambo?"
>>"Siku yako inaendaje?"
>>"Upo upande wa bibi harusi au bwana harusi?"
>>"Oooh, upande wa bibi harusi, ndo maana dada yako amewahi kuolewa!, ukoo wenu mzima inavyoonyesha umelaaniwa kwa uzuri!"
Mchokoze kwa maneno matamu, muulize maswali ya kumfanya afurahie maongezi na kama ukiwa unatoa sifa ifiche ndani ya sentensi inayovutia, ukitaka kumjua uliza maswali ambayo majibu yake ni mepesi na rahisi, kama ukitaka kujua anachofanya muulize,
>>"Kwa hiyo familia nzima mwanafunzi amebaki ni wewe tu, maana dada yako tayari ameshaolewa?"
Kwa maswali ya namna hio atajikuta anajiongelea kuhusu yeye na kukufanya akuzoee mapema, na ukiona maongezi yanaelekea ukingoni unatakiwa unakuwa shapu na mbunifu kwa kuanzisha mada nyingine inayovutia zaidi, itakayoleta maongezi matamu zaidi.
Kujua kitu cha kusema wakati wa kutongoza ni ngumu, ila inabidi ujiamini na ufanye kujisahau na kuweka akili kama upo unaongea na dada yako ila maongezi yaweke yawe ya kuvutia zaidi na uyapambe kwa sifa bila kuonyesha nia yako moja kwa moja, mwisho wa maongezi muombe namba ya simu au omba umtoe mtoko akuonyeshe maeneo hayo maana wewe ni mgeni na maongezi yamekupendezea na ungependa kuyaendeleza siku nyingine.
"Ukweli ni kwamba haijalishi utakachokiongea, unaweza ongelea kitu chochote kile ili mradi maneno yawe katika hali nzuri kihisia, onyesha tabia ya kujiamini na mipaka yako."
Acha kuwa na wasiwasi na kufikiria nini cha kuongea, we mfate kwanza na maongezi yatajitengeneza yenyewe kwa jinsi ya mazingira mliyopo na weka akilini kitu kimoja, huyo msichana unayeenda kumtongoza inawezekana anatongozwa mara tano au zaidi kwa siku tokea alipokuwa na miaka kumi na nane, kwa hiyo inawezekana ameshatongozwa zaidi ya mara 1000, kwa hiyo usifanye vitu ambavyo ameshavizoea kila siku na kuishia kutoa maamuzi ya kutokubali maombi yako kama wengine waliokataliwa waliotoa maombi yao hapo mwanzo kabla yako, kuwa mbunifu na tumia mazingira yako kwa usahihi na uzuri zaidi.
Hakikisha katika maongezi yako usiongelee wala kugusia vitu vifuatavyo,
  • Usimsifie sana, atakuona kama unambeza.
  • Usijaribu wala kumuuliza kama ana mtu, ana mshikaji wake au anamahusiano na mtu yeyote yule.
  • Usimuulize maswali magumu ambayo yanahitaji uelewa wa kitu fulani.
Vitu vifuatavyo ni ambavyo hutakiwi kuvifanya wakati wa utongozaji,
  • Usiongee kwa sauti ya juu sana,
  • Usijibu kitu au jambo kwa haraka sana,
  • Usiwe unaondoka ondoka au kuhamisha mapozi, usiwe na papara na kuwa mtulivu.
Kitu cha kuweka akilini zaidi usifikilie sana unachokiongelea, ukifikiria sana utakaribisha wasi wasi na kutokujiamini.
Wakati wa maongezi yako ya utongozaji, hakikisha unahusisha mambo yafuatayo,
  • Vitu ambavyo anashauku navyo na anavipendelea,
  • Vitu ambavyo unashauku navyo,
  • Hadithi zenye vichekesho na mguso wa mahaba,
  • Jifunze jinsi ya kuhadithia hadithi za kuvutia,
  • Mfanye acheke na kutabasamu kwa kile unachokiona,
  • Michezo ya furaha na ya kuvutia,
  • Unaweza kujikweza kidogo ila usipitilize.