Thursday, March 8, 2018

HIZI NDIZO SIKU ZA HATARI ZA MWANAMKE KUSHIKA MIMBA


HABARI za leo wasomaji wangu? Kabla ya kuanza mada hii ya leo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mungu kwani ameniwezesha kufika siku hii.Mada leo inahusu siku za hatari ambazo mwanamke  akifanya ngono bila kinga basi anakuwa katika hatari ya kushika mimba.

Nimeamua kutoa mada hii baada ya kugundua kuwa ongezeko la matukio ya utoaji mimba na kutupa watoto  na hata kuwa na watoto wa mitaani yanasababishwa  zaidi na mimba ambazo hazikutarajiwa.
Mimba nyingine zinaingia kwa sababu mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga asipate.

Ni muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, mizunguko hiyo iko katika makundi makuu matatu ambayo: Mzunguko mfupi wa siku 25 kurudi nyuma, mzunguko wa kawaida wa siku 28 na mzunguko mrefu wa siku30-35.

Wanawake wengi mzunguko wao  huwa  ni wa kawaida yaani siku 28 hawa ndiyo leo nitawaongelea zaidi.
Ili kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi unatakiwa kuhesabu kuanzia siku ya kwanza kuona damu ya hedhi hadi siku ya kwanza ya kuona damu ya hedhi ya mwezi unaofuata. Kwa mfano ukiona damu ya hedhi tarehe 15 Oktoba  basi hiyo ndiyo siku yako ya kwanza.

Kwa mtu mwenye mzunguko huo wa siku 28 siku zake za hatari za kuweza kushika mimba ni siku ya kumi na nne 14, hivyo kuanzia siku ya 12 hadi siku ya 16 kama atafanya ngono bila kinga anaweza kushika mimba.

Najua mtu anaweza akajiuliza kama siku ya hatari ni ya 14 sasa kwa nini akifanya ngono siku ya 12 anaweza akapata mimba?Hii ni kwa sababu mbegu za kiume zina uwezo wa kudumu kwa masaa 24 hadi
48 baada ya kujamiiana hivyo kama mwanamke atafanya ngono tarehe 12 na yai likatoka tarehe14 bado litakuta zile mbegu zikiwa hai hivyo zitarutubishwa.