Monday, January 15, 2018

SABABU ZA KITAALAMU NA ZA KISAYANSI KWANINI WANAUME WAOE WANAWAKE WENGI NA WATOKE NJE YA NDOA


1.Takwimu za kidunia zinaonyesha kuna idadi kubwa ya wanawake kuliko wanaume ,wanawake wamewazidi wanaume kwa 20%.Tukichukua ratio kila mwanaume asimame na mwanamke basi 20% ya wanawake watabaki pekee yao,je kila mwanaume aoe mwanamke mmoja hawa 20% wataolewa na kusitiriwa na nani? unakuta mwanamke ana miaka 36 yupo single siyo kwamba kapenda ila Takwimu za kidunia zimemfanya awe single.


2.Takwimu zinaonyesha wanaume ndio wanafungwa jela sana tofauti na wanawake,ukienda magereza mbali mbali na kutafuta idadi ya wafungwa basi utaona wafungwa wa kiume wapo wengi kuliko wa kike ,asilimia 90 ya wafungwa ni wanaume na 10% ni wanawake 

3.Sababu nyingine ni matukio ya vifo ni wazi kwamba wanaume wanakufa mapema na kwa wingi kuliko wanawake,idadi ya vifo ya wanaume kwenye vita ni kubwa ,Mara nyingi kwenye vita wanaume ndio hupelekwa mstari wa mbele kupigana na machafuko yote wanaume ndio hupigana na idadi kubwa ya wapiganaji hupoteza maisha pia wanaume hufa sana kwenye ajali kama za pikipiki Leo hii ukienda hospitali za muhimbili na mwananyamala na kutafuta idadi ya waliokufa kutokana na bodaboda basi asilimia kubwa ni wanaume ,ukienda migodini idadi ya watu wanaofukiwa na vifusi ni wengi,mapigano baina ya wakulima na wafugaji wanaopoteza maisha wengi ni wanaume bado hatujazungumzia wanaokufa maji kutokana na shughuli za uvuvi .Wanaume pia huongoza kuuliwa kutokana na wizi na ujambazi ,mifano tunayo mingi mamia ya watu huchomwa moto,hupigwa mpaka kufa kutokana na uporaji,ukwapuaji nk na 99% ni wanaume 

4.sababu nyingine ni ongezeko la mashoga ni wazi kwamba kwenye ulimwengu wa sasa wa utandawazi kumekuwepo na matatizo ya wanaume kugeuzwa kuwa wanawake na tumeona mataifa makubwa duniani yakipigania haki za mashoga na kumekuwa na NGOs nyingi zinazopigania haki za mashoga kama umebahatika kuona maandamano ya lgtb huko USA hakika utaona msururu wa maalfu ya wanaume mapusti yakipigania haki zao na hata huku Tanzania kuna idadi kubwa ya mashoga ukienda mitandaoni utawakuta wengi tena wengine wanajitangaza wazi,ukienda kwenye njenje,taarabu,klabu nk utakutana na wanaume wasioridhki wengi..

5.Kuna idadi kubwa ya wanaume wasiokuwa na uwezo wa kuzalisha na wana upungufu mkubwa wa nguvu za kiume,Leo hii ukipita barabarani utakutana na matangazo mengi ya kutibu nguvu za kiume,wauzaji wa mihogo mibichi wameongezeka nk,uwepo wa vyakula feki zenye sumu na mafuta mengi yamewafanya baadhi ya watu kupoteza nguvu za kiume na uwezo wa kuzalisha.

6.ongezeko ya watumiaji wa dawa ya kulevya "mateja". Hakika dunia ya leo imekumbwa na idadi kubwa ya watu wasiokuwa na mbele wala nyuma "mateja" tuchukulie mfano hapa kwetu Tanzania tumeona vijana wengi walioathiriwa na dawa za kulevya walivyopotea ,watizame mateja waliopo stendi za mabasi,mitaani walivyochoka na kudhoofika na teja siku zote hawazi mwanamke yeye mwanamke wake ni heroin na teja haoi ,kuna mateja wa aina nyingi hawa mateja matajiri tuwaache tuwazungumzie mateja wasiokuwa na pesa ambao wanashinda stendi,vibarazani,vichochoroni nk na wapo wengi sana ,

Takwimu zinasema wanawake wapo wengi kuliko wanaume duniani na shirika la utafiti duniani wamesema wanawake wamewapita wanaume kwa wingi wa 20% ,Leo hii kila mwanaume apewe msichana 1 hakika 20% ya wanawake watabaki single ..

Sasa kama wanawake wapo wengi kwa 20% kuliko wanaume ukijumlisha na ongezeko kubwa la mashoga,idadi kubwa ya vifo kwa wanaume,idadi kubwa ya wafungwa wanaume kuliko wanawake,idadi kubwa ya mateja wasiokuwa na future,idadi kubwa ya watu wasiokuwa na uwezo wa kuzalisha na wenye upungufu mkubwa wa nguvu za kiume. Hakika wanawake wengi zaidi watakosa wanaume..

kama ki idadi tu wanawake wengi wapo single kutokana na upungufu wa idadi ya wanaume, je vipi factors 5 hizo zingine si itakuwa hatari zaidi ,ongezeko ya wanawake wengi kuwa single itakuwa kubwa zaidi 

NB: ewe mwanamke ukimuona mwanaume wako anachepuka usikasirike sababu wanawake wenzako pia wanahitaji kusitiriwa sababu nature wanaume wapo wachache sana je wewe ukiwa mchoyo wenzako watapata huduma wapi na pia watakuwa single milele 

Pia nashauri wanaume tuoe wanawake wengi au tuchepuke sababu demand ya wanaume ni kubwa ,supply ni chache kutokana na scarcity ya wanaume iliyopo ..hivyo tusipo oa wengi na kuchepuka tutakuwa hatuwatendei haki wanawake