Wednesday, January 17, 2018

Mvuto Hauna Maana Kama Huongezi Nguvu Na Akili


Sababu kubwa ya kwa nini watu wa kisasa  wanachukia   urafiki na uchumba ni kwa sababu kila mtu anavutia mwingine  lakini hakuna mwenye kutumia nguvu na akili  ya kutaka kumjua zaidi  mtu anayevutiwa naye.
Sio kwamba mvuto hauko pale , upo, Lakini hakuna nguvu wala akili ya  katika yote. kuanzia kwenye meseji za kawaida zilizo rahisi kwa ajili ya kupata muda wa kuwa pamoja, Kila mara kuna kitu kinakosekana , kitu fulani hakiko sawa na kila mara inaonekana kuna ugumu katika kukutana .
Mvuto ni wa muhimu lakini mvuto bila ya kutumia nguvu na akili hutaweza kufika popote.
Nguvu ina maana , kujaribu, ina maana ya kuwa na muda wa pamoja hata kama unaogopa , Ina maana kumpa mtu nafasi  kabla ya kuamua kama hujawa tayari.
Nguvu ni jinsi ya  kuonyesha kumpenda mtu , ni jinsi unavyoenda kuongea naye ili kumfahamu , na ni jinsi unavyoenda kutaka kuwa pamoja kwa muda wa kutosha na kuonyesha kuwa unataka kushirikiana naye katika maisha.
Nimekuwa nikiweka hisia za kimwili na mvuto juu  kuliko kitu chochote, Na pale ninapofikiria ni vya muhimu.  Nimetambua kuwa havitoshelezi bila ya kuongeza nguvu zako  na kutunza maneno   unayosikia kutoka kwao . kufahamu kuwa mtu kukupenda  haitoshi kama hutajiongeza.
Nafahamu maoni ya wengi ni kuhusu kiwango  cha mtu  kilingane na kiwango cha mwingine, ni kweli  lakini haina maana kuwa  hakuna maendeleo  kwa sababu hakuna mawasiliano ya kutosha. Ina maana ya kutumia uwezo zaidi wa kiakili, kujua mbinu mbalimbali.
Kwa sababu kama utaweza kutumia nguvu  na kutambua kuwa ni wewe pekee ndio  unajitahidi lakini upande mwingine hakuna, hapo itakuwa ngumu kuendelea.  Ni ngumu kuendelea kwa sababu mwingine hatumii nguvu kukutafuta ili muweze kukaa pamoja na kufahamiana. Huwezi kutunza kama  hupati ushirikiano.
Kwa hio Wakati mwingine sitaangalia mvuto tu  au hisia tu, Nitatazama nguvu iliopo. Nitaangalia mtu mwenye kutafuta muda wa kuwa na mimi. Mtu ambaye haogopi kuuliza maswali, Mtu ambaye hasubiri muda sahihi wa kuniomba kutoka naye. Nitatazama mtu ambaye anajaribu , mtu anayeweka nguvu na kunifanya mimi niongeze nguvu zaidi.
Kwa sababu hicho ndicho kila mtu anakihitaji . Uhakikisho. Tunahitaji kujisikia kukubalika na kutazama jinsi kila kitu kinavyoendelea. Kutazama kitu gani kinatokea unapoongeza  nguvu ya pamoja.  Kutazama jinsi mahusiano yatakavyokuwa mazuri