Nakupenda sana mwandani wangu ndiyo maana moyo wangu hupatwa kidonda ninaokuona na mwingine
hasa anapokuwa hana sifa, nahisi kama anakutumia wewe kama mdori wake wa kumfurahisha. Uwe makini ua la moyo wangu.
Mpenzi wangu kukutana nawe ilikuwa ni bahati, kukuchagua kuwa rafiki yangu ilikuwa ni maamuzi yangu, lakini kuanguka kwenye penzi lako haikuwa hiyari yangu. Umeniteka moyo na akili yangu pia.
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako,
naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
Fungua macho yako uone kopa za mahaba ninazokumwagia, fungua mikono yako na upokee mapenzi yangu, fungua simu yako uone ni jinsi gani ninavyokukumbuka japo kwa kukutumia sms mpenzi wangu, Nakutakia usiku mwema
Utamu wako ni zaidi ya asali, ni wa asili usiohitaji kuongezewa ladha ya sukari, nitaumiss endapo kama ukiwa mbali "NIACHE NIKUPENDE SWEET"