Monday, January 15, 2018

Kwa wanawake tu; Fanya haya kumchizisha Mpenzi wako kitandani


Mtaalam wa mapenzi, Bi. Layla Quinn, anasema wamaume ni viumbe rahisi sana kuridhishwa tunapokuja katika suala la unyumba. Mwanzoni, kitu kinachomhamasisha mwanaume kujamiiana ni muonekano wako (mwanamke) tu wakimahaba, lakini kadri siku zinavyokwenda ndani ya mahusiano, inakuwa ngumu kupandisha munkari wake, hata kama wewe ni mwanamke mrembo barabara!
Bi. Layla anaendelea kusema kuwa, kumridhisha mwanaume wako kitandani inaweza ikawa rahisi kama tu utakumbuka kuweka mambo katika hali ya mvuto ( Remember to keep things intereting!). Tafuta namna ya kuleta hamasa, iliyokuwepo siku za mwanzo mwanzo, na kwa hakika utakamata usukani. Sasa swali linakuja…..Nini unatakiwa kufanya, ili kumridhisha mwanaume wako kitandani? Kujibu swali hilo, Bi. Layla amekuja na sheria 10 zifuatazo, ambazo kama zitazingatiwa kwa makini, basi mwanamke hatokuwa na shida ya kumridhisha mwanaume wake kitandani na nyanja nyingine muhimu za mahaba.
# 1 Vaa vizuri. Utamu wa kujamiiana unaweza ukawa kwenye tendo lenyewe, lakini matamanio ya kufanya tendo hilo, yanategemeana na mambo mengine mengi. Vaa vizuri wakati wa kulala wakati wote, na sio tu wakati wa usiku, ambao unataka kufanya mapenzi. Vaa nguo nyororo, yenye mtelezo unaomwagika mwilini. Kwa vazi hili na mtembeo wa kimahaba chumbani, mwanaume wako hatotaka kutoa mikono yake mwilini mwako.
#2 Usiwe mtu wa aibu aibu linapokuja suala la kujamiiana. Mwaume anaweza akakupenda kwa mapozi yako na aibu kwanza (lugha iliyotumika hapa ni “innocence”), lakini hamna mwanaume atakaye endelea kuvumilia mwanamke, ambaye anastushwa kirahisi na kila kitu (mitindo ya kujamiiana), isipokuwa mtindo wa kifudi fudi, maarufu kama “Kifo cha Mende”. Wanaume wanapenda wanawake, ambao ni wataalam kitandani. Wanaume wanapenda wanawake, ambao wanajiamini na wanabuni manjonjo mbalimbali wakati wa shughuli. Kama unataka kumridhisha mwanaume wako kitandani, basi soma mbinu mbalimbali, ambazo zinatumiwa na wapenzi mbalimbali.
#3 Fanya mazoezi na onekana Bomba. Wanaume ni watu wakujali sana muonekano wa mwanamke. Kwahiyo, sio lazima kuonekana kama walimbwende wa vichupi, lakini mtazamo wa karibu na hapo, utakuongezea mvuto zaidi kitandani. Ndio, mwanaume wako “anakupenda kama ulivyo” na tila lila nyingiiiii…..lakini lazima tuukabili ukweli kwamba watu wenye kufanya mazoezi wanaonekana na mvuto zaidi, hakuna kupinga hilo. Hata kwetu Bongo katika nyakati hizi za utandawazi, wakina kaka wengi wanawaona wanawake kama wakina Naomi Campbell na Jennifer Lopez, ambao wanatamani kuwa nao. Lakini hauhitaji kuwa kama wakina Naomi na Jennifer kumridhisha mwanaume wako, bali hakikisha tu upo katika umbo zuri la kumpelekesha kirahisi kitandani, Basi!
#4 Kuwa Mchokozi. Hapa haimaanishi ule uchokozi wa kuleta ugomvi, lahasha! Bali, ni ule uchokozi, ambao kwa lugha ya kingereza unafahamika kama “Tease”, kwa maana hiyo basi tunasema “Tease him”. Cheza nae michezo mbalimbali na burudika nae ipasavyo, na michezo isiwe ya kitandani tu, kama karata na kadhalika, bali michezo ya hata nje ya kitanda kama kukimbia na kucheza kidali po! Kama unataka kuwa mjuzi kitandani, basi unatakiwa umfanye mwanaume wako akutake wakati wote na popote pia. Kujamiiana sio kitasa ambazo unawasha na kuzima mnapokuwa chumbani tu. Mchokoze chokoze wakati mnasakata muziki jukwaani, na mchokoze chokoze (katika mitindo ya kimahaba, bila kuvuka mipaka) wakati yupo na marafiki zake.


#5 Jiamini na Jipende. Ndio, utaonekana vizuri zaidi ukipunguza maunene, lakini hiyo haimaanishi kwamba haupo bomba. Hakuna kinacho kera wanaume, kama mwanamke, ambae anauonea aibu mwili wake mwenyewe wakati anafanya mapenzi. Jiamini kuhusu mwili wako wakati upo mtupu, na jaribu mambo mbalimbali na mwanaume wako.