Thursday, January 11, 2018

MAMBO MABAYA 10 YA KUTISHA WANAUME HUWAFANYIA WAKE ZAO

Ok ,  wewe sio yule mwanaume wa kutisha. Lakini yapo mambo mabaya ambayo unamfanyia mke wako  na kuharibu uzuri wa ndoa yako. Mke wako anastahili  kitu bora kutoka kwako  kuliko hata   haya mambo kumi mabaya unayoyafanya kwake.
1.Muhimu
Tafadhali  jiangalie  na  usimwekee mitego mke wako  na kuanza kumlalamikia kwa kitu ambacho unajua wazi kuwa umemtegea. Chagua  kuona mambo mazuri kwake. Msifie  kwa kila kitu ambacho anakifanya kilicho sahihi. Wakati mwingine ambapo unataka kumwambia  kitu ambacho hukipendi  tafadhali jiangalie kwanza ,  badilisha hicho kitu kwa kitu kingine kizuri kama kumpa sifa  atapenda.
2.Kutawala
Amini usiamini,  hauko sahihi kila wakati. Na mke wako mzuri  yuko vizuri kwa kufanya maamuzi yake.  ( na hufanya maamuzi mazuri  siku zote)  kwa hio acha  kumfuatilia kila kitu anachokifanya, kutaka kujua ameenda wapi,  anafanya nini,  mbona kelele  uko wapi,  umetumia shilingi ngapi.
Badala ya kuwa na hizo stress ni bora wote muwe kama timu, fanyeni kila kitu pamoja, Kusaidiana na kupongezana . Mwache mke wako ajitambue kuwa yeye ni nani.Tena mpe mabawa ya kumwezesha kupaa.
3.Unamfanye kama chombo cha kutumia.
Tafadhali, wanaume! Mke wako sio chombo cha kutumia unapotaka kutumia, Ni mke wako., ni rafiki yako na huyo ndio  queen wako. Mara zote mpe heshima yake , hasa inapokuja wakati wa urafiki wa kimapenzi.
Heshimu mwili wake  na fanyia kazi hisia zake   ili muweze kushirikiana pamoja kwenye  mapenzi ya kirafiki. Sex itakuwa ni nzuri ,  yenye ukamilifu wa ndoa yenu  wakati mnapokuwa mnafanya kwa ushirikiano.
4.Huna muda wa kukaa nae na kumsikiliza
Una mke, una bahati sana. Tafadhali usimsahau. Usiwe na  bize nyingi  hata usiweze kumpigia hata simu, kumtext na kumtakia kazi njema. Ukirudi mkumbatie  kwa upendo  ili ajue kuwa  alikuwa kwenye mawazo yako  ingawa ulikuwa kazini. Mwambia kuhusu vyote ulivyokutana navyo siku hio, ongea nae mambo mengi yanayohusu kazi. Kaeni pamoja  kusikiliza taarifa mbalimbali za habari. Mwambie mawazo yako,  wasiwasi wako. Lakini kuwa makini katika kuongea huko kunaweza kutokea jambo. Usisite. Tekeleza kwa wakati.
5.Unatumia lugha mbaya
Mwanaume. Ikiwa tayari umeoa wewe sio kijana mdogo ( hata hivyo lugha mbaya haina maana)  angalia mdomo wako, chunga ulimi wako, acha hiyo tabia mbaya, na ondoa  maneno machafu ulionayo. Tumia maneno mazuri unapokuwa na mke wako .Mke wako anastahili kusikia maneno mazuri kutoka kwako yenye upole , sio ya kufoka. Jaribu maneno mapya, na mke wako atakupenda hata wewe utajisikia vizuri.
6.Kuangalia picha za uchi
Hii kitu inaharibu ndoa nyingi, maisha yako  sasa na baadae. Acha kuangalia hizo picha zitakufanya  uchanganyikiwe kila mahali unapokwenda. Chagua njia bora . kama umekuwa ukiangalia hizo picha , tafuta mtaalamu wa saikolojia akusaidie. Au tafuta mshauri akusaidie kuanza  process ya kuondokana na kuathirika kwako ili uwe huru. Anza kubadilika  ili na wale unaowapenda wabadilike. Kwa hio amua  kwa akili, ni aina gani ya maisha  unayotaka .
7.Una matarajio makubwa
Kitu cha mwisho ambacho mke wako mpenzi anataka kukisikia ni  kwamba  hutarajii kitu kikubwa kupita  ukweli uliopo. Tafadhali usimlinganishe mke wako  mwili wake, ujuzi wa bajeti na wazazi wako, au na watu wengine wa mtaani. Kulinganisha kwako kutacrush hadhi yake. Amua kuwa mwema , mvumilivu kuwa mtu wa kusamehe.
Ukiwa unamsifia kwa mambo mazuri hata kama alikuwa hana sifa zingine , atajitahidi kuwa nazo  na kuwa yule mwanamke ambaye ulitarajia kumpata na zaidi .
8.Husaidii chochote nyumbani
Hii ni kweli? Unaweza kuwa wewe ndio unaleta kila kitu au  kila mtu analeta nusu kwa nusu.  Lakini hio haina maana kwamba wewe ukae tu bila ya kumsaidia mke wako hata kufua, na kufanya usafi. Kwani kabla hujaoa nani alikuwa akikufulia nguo, na kufanya usafi wa chumba chako. Ulikuwa hupigi pasi mwenyewe?
Badilika anza kufanya kazi hizo, osha hata vyombo . kwani kuna tatizo gani. Au wewe ni mtu wa kusikiliza maneno ya watu?  Fanya kitu ili mke wako ajisikie thamani . Fanyeni kama timu. Na nyumba yenu itakuwa na furaha.
9.Unakasirika kila mara
Umekuwa mtu mzima sasa, kulalamika kila mara mbele ya mke wako  sio vizuri. Haina maana na haisaidii kitu.   Kuanza kufoka, kutupa vitu, kumwaga chakula , kutukana, hio ni dharau. Unaweza kujifunza jinsi ya kuondoa hasira na kuitawala, na utaweza kujifunza kuwa na utulivu  kwa kuwa na upendo .  mke wako atajisikia kuwa na amani na kujiona yuko salama kila wakati atapenda kuwa karibu na wewe.
10.Uongo na Usaliti
Kama unafikiria kuwa unaweza kutoka na mwanamke mwingine huko kazini na kwamba mke wako hatajua, Unajidanganya mwenyewe na kukosa  uaminifu kwako.Ukweli ni kwamba hata kama mke wako hatajua. Bado itakuwa sio sahihi. Usitake kujipatia  msongo wa mawazo bila sababu . chagua kuwa mkweli, chagua kuwa mwaminifu. Ishi na ahadi yako ulioahidi kwa mwenza wako. Anastahili hicho na zaidi.
Sasa basi, kama umejiona kwenye moja ya tabia hizo hapo juu . Usihofu, Amua kuwa bora sasa na fanya mabadiliko. Tafuta  mafunzo yatakayokuongoza ,  na mke wako,  mtaishi maisha bora  na ndoa ya furaha  ambayo ndio ulitarajia kuwa nayo .