Friday, January 19, 2018

Fanya Mambo Haya Ili Mpenzi Wako Achanganyikiwe Juu Yako Na Kukupenda Zaidi.

Na DOKTALOVE
"Kwenye mahusiano ya kimapenzi ni vizuri uzito wa mahusiano uwe pande zote mbili, mapenzi huwa matamu zaidi iwapo umpendae naye anakupenda kwa kiwango umpendacho wewe, na si vinginevyo maana tofauti na hapo mapenzi huwa kama kero au mzigo na hisia hukupelekea kujiumiza moyo na kujiharibu kisaikolojia".Wewe ni mtu mzuri na unampenda sana msichana wako, kiasi kwamba unamkubali sana mpaka unampa dunia yako kumuonyesha unavyomjari, ndani ya muda mrefu mliopo kwenye uhusiano umeshajitoa kwa mengi, kimuda na hata kifedha, unamchukua kutoka kazini kila siku ndani ya juma ili tu asije kuchosha miguu yake mizuri na laini.
Unamsaidia kwa kila jambo analohitaji na umeacha kutumia muda wako na marafiki zako ili kusudi uwe na muda mwingi zaidi wa kutumia naye, umemnunulia gauni la gharama na vingine vingi ili apendeze bila kuchoka huwa unabadilisha ratiba zako ili ziweze kuendana na za kwake ili muwe pamoja na kumuonyesha jinsi gani alivyo na nafasi kubwa ndani ya moyo wako, na unafanya yote haya bila ya kumtaka kitu chochote kutoka kwake.
Na hata hivyo ni mara moja tu siku ule ulipokua unaumwa ambapo ulimuomba akupikie ugali na akakuchukulie mishikaki unayoipenda pale uswazi teki awei, ambapo alikataa kwa upole na kukwambia hajui kupika vizuri ugari na wewe ulikubali kwa roho safi maana hupendi kuwa kero kwake.
Sasa turudi kwenye uhalisia.
Rafiki sijui nikuambieje ili unielewe, kaka hapa unatiketi moja tu inayokwenda bila kurudi ambayo kupeleka kwenye nchi ya mvunjiko wa moyo ambapo wapo wapenzi wake wa zamani aliowaacha.
Ni muda wa kumuuliza, "Hivi ni kipi umenifanyia mimi hivi karibuni?".
Kila ukiwa unamfanyia kitu kizuri nahisi labda unaona kama unajiongezea pointi nyingine za ziada, lakini kiukweli ni kwamba kama yeye hatojihusisha na kuchangia kwa kukufanyia wewe hayo mambo mazuri unayomfanyia yeye kwenye uhusiano wenu, jua kabisa nguvu zako zitakua hazina faida yeyote ile, ni kama maji mtaroni yanayopita tu, na hapa ndipo kiumeni.com tunapokwambia kwanini!.
Kikawaida tunaweza kuwapa ushauri wanaume wengi wanaokutana na haya wavunje uhusiano tu pale mwanamke anapomtumia mwanaume bila kurudisha upendo wowote ule anaofanyiwa, hapa simaanishi yale mambo yetu mengine ya kitandani.
Lakini kama kweli umejiweka kwenye huu uhusiano kwa roho yote na unataka uhusiano uendelee kuwa wa muda mrefu lazima ufanye na yeye awekeze hisia zake na hata pesa zake kwenye huu uhusiano hata kama ni asilimia 50%.
Hapa haijarishi wewe ni tajiri kiasi gani, ni mzuri kiasi gani au ni mwanaume mwenye mahaba yote duniani kiasi gani, kama mwanamke hana kitu chochote alichowekeza kihisia, iwe ki muda au ki fedha lazima atakuacha iwapo mtu mwingine ambaye yuko zaidi ya wewe akitokea. Kama sheria za kiumeni.com zinavyosema(kama msomaji utakua unazijua), "Mtu mpya na ambaye ni zaidi yako huwa yuko nyuma anakuja, anasubiri ukosee kidogo tu", na kama hata jiwekeza kwako likija dili ambalo ni zaidi ya wewe unalompa lazima ataondoshwa tu
Bado hujaniamini tu?
Kama ukiwekeza kiasi fulani cha muda na fedha kwenye mpango flani, iwe kununua nyumba au kuanzisha biashara, utakua unajua uchungu na uzito wa kitega uchumi chako tofauti na ukiwa umepewa bure.
Sheria hizi hizi ndizo zinazofanya kazi kwenye mapenzi, ni ubinadamu kuona uzito na uchungu kwenye kitu ambacho umekiwekeza, sasa nini swali kwako, "Ni nani anayechangia sa kwenye uhusiano wenu?, ni wewe au ni malaika wako mrembo?
Fikiria kwa umakini maana uhalisia wa jibu lako tayari limeshafanya kazi kubwa kuutengeneza uhusiano wako jinsi ulivyo sasa.
Mwachie baadhi ya malipo afanye yeye...
Inabidi uwe kama vocha isiyorudishwa, fikiria kila saa msichana wako akienda kununua mahitaji yake, analipia kwa vocha na anapata muda wa maongezi, atafanya hivi kwa kipindi kirefu mpaka ndani ya muda atakuwa na muda wa maongezi ambao anaweza kuutumia kuongea kwa miaka mingi, sasa vipi kampuni nyingine ya vocha ikiingia na kumpa ofa nzuri zaidi?, kwa unavyofikiria anaweza kubadilisha kampuni?
Kama hata kuwa na muda wa maongezi mwingi na wewe, basi kuna nafasi kubwa atabadilisha kampuni bila kujiuliza na kwa upande mwingine kama atakua na muda wa maongezi mwingi wa miaka kumtosheleza maongezi yake kutokana na jinsi alivyowekeza, hawezi kubadilisha kampuni. Umeipata pointi yamgu, Rafiki?
Kazi yako...
Ni kazi yako kumfanya msichana wako awekeze muda na hela kwenye kampuni yako ya vocha ili ikija kampuni nyingine isiweze kumchukua akili kwa ofa nzuri itakazokuja nazo.
Kwa kuwa sasa hivi nimeshakuelewesha umuhimu wa kumfanya msichana wako awekeze kwenye uhusiano, sasa utafanyaje ili aanze kuwekeza?
Omba misaada: Kitu muhimu cha kuangalia sasa hivi ni misaada, kama akikupa msaada atajishauli amefanya hivyo kwa sababu unamvuto kwake na unastahili kufanyiwa hicho alichokifanya, acha sasa hivi akuhudumie vizuri, mwache sasa hivi akupikie, saa zingine mwombe aje akupitie kazini na mwache alipie baadhi ya vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wake.
Ukiishiwa vocha usione aibu kumtumia tafadhari niongezee salio mara moja moja.
Hii ni moja ya sababu hutakiwi kuweka mayai yote kwemye kapu moja, na ndio maana huwezi kumwacha mwanamke ambaye hakujali kwa sababu wanaume wengi wanakuwa wamewekeza muda mwingi na fedha kwa huyo mwanamke.
Muda ni pesa: unaweza kumwongezea hamasa zake kwako kwa kumfanya atumie muda mwingi na wewe kwa kufanya vitu unavyovipenda na sio anavyovipenda, hii itamuonyesha uzito wako kwake.
Sio mbaya kumbeba mwanamke kama dhahabu, ila hakikisha ndani ya uhusiano kila mmoja anawekeza na sio uhusiano uwe unaegemea upande mmoja tu, kama kweli anahisia na wewe basi hisia zake zitamwendesha na yeye akujali wewe kama ambavyo zinakuendesha wewe.