Sunday, December 10, 2017

SOMA KUHUSU MANENO YAJENGANGAYO NA KUBOMOA MAHUSIANO.

Maneno ndiyo hubomoa na kujenga uhusiano.
Hatari iliyopo ni kuwa wanaume wengi wanapowazoea wapenzi wao, hushindwa kutamka neno hilo lakini mwanamke hupenda kusikia akiambiwa hivyo.
Mwambie mpenzi wako jinsi unavyompenda, mthibitishie kuwa mapenzi yako kwake ni makubwa kupita kiasi.
VIPI KUHUSU WANAUME?

Wanawake wengi hulalamika kuwa wanaume ni watata kwenye mapenzi.
Hulaumu kwamba ni ngumu kubaini vitu ambavyo wanaume huhitaji kutoka kwa wanawake.
Wanadai kuwa wakati mwingine hujitahidi kadiri ya uwezo wao kuhakikisha wanawapa furaha lakini wanaume huwa hawana hata msisimko.
Hapa chini, nimekuandalia vitu ambavyo wanaume huhitaji kwa wanawake wao. Moja kwa moja, mambo yakienda chanya huwa ni zaidi ya chombezo na hupagawa.
MAPENZI (Love)
Siku zote wanaume huangalia mapenzi kwa wenzi wao.
Mara nyingi wanaume huwa wepesi kuonesha mapenzi kwa wanawake wao lakini ndani ya nafsi zao, hutegemea mambo mengi kama malipo (return) ya upendo waliotoa kabla.
Wanapenda, kwa hiyo nao huhitaji kupendwa ili waone mambo yanakwenda sawa.
Wanawake wengi huwa wanaficha hisia za kupenda, hili huwaumiza wenzi wao.
Onesha mabadiliko, muoneshe jinsi unavyoridhishwa na upendo wake kisha mtamkie kwamba kwake umefika, halafu thibitisha hilo kwa vitendo.
MVUTO (Attractiveness)
Wanaume huhitaji wapenzi wao wawe na mvuto. Hii inawezekana isiwe na maana kwa wanawake kwa kushindwa kutambua mvuto wao, unavyoweza kuwa kibwagizo murua cha mapenzi.
Vaa vizuri upendeze, hakikisha muda wote unakuwa nadhifu.
Muonekano wako ndiyo utamfanya mwenzi wako ajiamini popote.

Kwa hiyo, kupendeza kwako ni bonge la chombezo kwa mwenzio.
UAMINIFU (Trustful)
Wanaume hupenda wanawake wenye uaminifu wa asilimia 100.
Mwanaume huhitaji mwanamke ambaye muda wote atakuwepo kwa ajili yake kimapenzi, kubadilishana mawazo na kumshirikisha katika siri za maisha yake.
Bahati mbaya wapo wanawake wengi ambao hawana uaminifu hata chembe.
Hilo huwafanya wanaume kukosa imani kwa wapenzi wao.
Jiamini kisha uwe muaminifu.
Mfanye mpenzi wako asikutilie shaka ya aina yoyote kisha uone jinsi maisha yanavyoweza kusonga mbele.
FAMILIA (Family)
Wazo la kila mwanaume anapopata mwanamke, hufikiria ajenge naye familia haraka iwezekanavyo. Hivyo basi, huhitaji mwanamke ambaye yupo tayari kwa hilo.
Kitu ambacho huwakera wengi ni pale wanapokutana na mtu aliye na mawazo ya kurukaruka.
Kama umeshaolewa, muoneshe mumeo jinsi ulivyo fundi wa kuiweka familia pamoja.
Ukifanya hivyo, utakuwa umempatia, kwani hakuna jambo ambalo wanaume huwa hawapendi kama kuona familia inasambaratika.

UKARIMU (Kindness)
Wanaume huwa na matarajio ya kuwaona wanawake wao wakiwa wapole, waungwana na wakarimu. Jitazame na ujitengeneze kuwa hivyo ili umvutie mwenzi wako.
Ukorofi, ubishi na roho mbaya siyo sifa ya kike.
UCHESHI (Funny)
Wanaume hupenda wanawake wanaojua kucheka. Akiwa naye, wazungumze na wacheke. Wanaume huwachukia wanawake wanaopenda kununa. Kama una tabia hiyo, jirekebishe ili umkune mwenzi wako.
U-MWANAMKE (Femaleness)
Kwa kawaida, wanaume hupenda wanawake ambao wanajitambua kuwa wao ni wanawake.
Huwachukia wale wanaojipa sifa ya u-dume au wababe, wanaopenda kutoa amri.
Huhitaji wanawake wanaotimiza wajibu wao kama wanawake kulingana na jamii inavyotambua. Hupenda wanawake wanaojali, kujiheshimu na kadhalika.
Wale walevi hukosa sifa ya u-mwanamke ambayo wanaume huihitaji