Friday, December 15, 2017

Mwanamke Mwenye Tabia Hizi 4 Muogope Kama Ukoma.

Wanaume wengi hupata tabu kutambua wasichana wa kuwa nao kwenye mahusiano ya kudumu, sababu ikiwa wao wenyewe pia ni waongo kiasi wanawake nao wameanza kujanjaruka na kutafuta njia ya kuwa nao bila wao (wanawake) pia kuumia mtima, na pengine kwa wengine ikawa ni maamuzi yao na wakawa ni wenyekutafuta kutimiza haja zao tu na si kuwa kwenye mahusiano ya kudumu. 

Kwa kawaida wanawake wamekua siku zote wamekua wakiwaza, kupata elimu, kisha wapate kazi nzuri na baadae wapate familia bora. Lakini mwenendo huo umekua mgumu sana kutimia kwani wanaume wanaotaka kufata mlolongo huo wamekuwa wachache sana. kiasi wengi wameamua kuwa na mahusiano na eidha mwanaume zaidi ya mmoja, au mmoja tu anayekidhi ashiki zake au kumpatia fedha, bila kuwa na nia ya kuolewa na wala kuwa na familia.

Ikiwa unahitaji mahusiano ya kudumu na mwanamke mmoja angalia ishara hizi na ujiepushe na :-

Shangwe za kila wakati.
Unakutana na  mwanamke kila siku ya weekend yuko katika klabu za usiku. Daima yeye huwa na rafiki zake wa kike wakinywa pombe, wakivuta bangi, shisha au sigara na wala huoni muda analipa bili. Utaona picha zake akiwa na rafiki zake na ukiangalia kwa makini utamwona akiwa na marafiki tofauti wa kiume katika kila picha kwenye mitandao yake ya kijamii.

Uhusiano na wanaume tofauti kwa wakati mmoja.
Mwanamke wa aina hii  huwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume tofauti kwa wakati mmoja. Kazi yake kubwa ni kujisifu kwa wenzie kuhusu mahusiano yake na wanaume hao ambao yuko nao na kuchat nao kwenye simu wakati wote. Simu zitakua chache, na  atakupa visingizio vingi tu, yule rafiki yangu tu, yule nafanya nae kazi, yule tumekuwa wote mtaani. Na inaweza kuwa kweli lakini lazima kuna mtu katika hao aliokupa maelezo yake ambaye tayari ameshakuwa nae, au yuko nae kimapenzi.

Hujitongozesha/Hujilengesha.
Na kwa tabia hii, hujikuta yuko kwenye mahusiano na mwanamume aliye na familia ama mwenye mchumba anayetaka kumuoa. Pia haogopi ‘kumuiba’ mume wa rafiki yake ama dadake.

Muziki anaoupenda.
Utawajua wanawake hawa kwa muziki wanaosikiza ili kujiliwaza. Hii hapa orodha:

Freak like me – Adina Howard

I’m a survivor- Destiny’s Child

Miss Independent – Neyo

Irreplaceable- Beyonce

Single Ladies- Beyonce

Girl on Fire- Alicia Keya

No scrubs- TLC

I’m every woman- Chaka Khan

Mwisho wa yote, samaki mmoja akioza haimaanishi wote ameoza.