Tuesday, December 12, 2017

JINSI YA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATIZO YATOKANAYO NA KUKUA KWA TEZI DUME KWA KUTUMIA VYAKULA HIVI VI 5



Kichocheo cha testosterone au kwa Kiswahili , japo huusishwa zaidi na upande wa mwananume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanamme pia.kadiri umri unavoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testerone kupungua, kupungua kwa kichocheo hiki kunaambatana na ukuaji wa tezi dume (prostate gland),kupotea kwa nywele na pia saratani mfano saratani ya tezi dume.
.KAZI KUBWA YA KICHOCHEO HIKI NI KUONGEZA MSUKUMO NA HAMU YA TENDO LA NDOA, KUIMARISHA MISULI NA MIFUPA MWILINI.
NINI KINAHITAJIKA ILI KUZALISHA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE?
Ili kuhakikisha uzalishaji wa kichocheo cha kiume unafanyika, mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali, baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya ZINC na vitamin D3,  vitamini D inaweza kuzalishwa na mwili pale ngozi yako inapokutana na mwanga wa jua, hapa nazungumzia mwanga wa asubuhi
wakati jua ndo linachomoza na pia lile jua la jion karibia na kuzama, hivyo utakubaliana na mimi kuwa wengi wetu tunakosa vitamini D kwa sababu muda mwingi tunautumia tukiwa ndani tukiendelea na shughuli zetu. Zinc ni madini muhimu ambayo hupatikana kwenye baadhi ya vyakula.
NINI HASA KINASABABISHA KUPUNGUA KWA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE KWENYE DAMU
Mawazo au stress ni muuaji asili wa kichocheo cha testerone, pale unapokuwa na stress basi Tezi ya Adrenal hutengeneza kichocheo iitwayo Cortisol ambayo inapoenda kwenye damu hupunguza ufanyaji kazi wa kichocheo cha kiume cha testosterone ndani ya mwili. Hivyo kama unataka kuepusha tatizo hili ni wazi kwamba unahitaji kupuza stress na kiwango cha cortisol.
AINA ZA VYAKULA AMBAVYO HUSAIDIA KUONGEZA UZALISHAJI WA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE
Ijapokuwa kuna njia nyingi za kusaidia kuongeza kiwango cha kichocheo cha kiume au Testosterone, uzalishaji wa kichocheo hii unategemea zaidi upatikanaji wa viini lishe fulani ambavyo vinapatikana ndani ya vyakula tunavyotumia.
1.      KOMAMANGA (POMEGRANATE)
Tunda hili zuri lenye rangi nyekundu likiwa limeiva limekuwa likitumika kama dawa kwa karne nyingi sasa. Kutokana na uwezo wake mkubwa kama kiondoa sumu (antioxidant), pia upatikanaji wa vitamini A,C, E na madini ya chuma, tafiti za kisayansi zinasema kuwa unywaji wa glass 1 ya juisi kwa siku itokanayo na matunda haya inaongeza kwa asilimia 16 mpaka 30 ya hamasa ya tendo la ndoa. Lakini pia inashauriwa zaidi kula tunda lenyewe ili kwanza kufaidi nyuzinyuzi (fiber) ambazo zina umuhimu kiafya pia itakusaidia kutokula kiwango kikubwa cha sukari kilichopo kwenye matunda.

2.      MAFUTA YA MIZEITUNI
Mafuta ya mizeituni yana uwezo mkubwa sana wa kuongeza kiwango cha kichocheo cha Testesterone kinachozalishwa na mwili. Tafiti zinasema watu wanaotumia mafuta ya mizeituni kila siku,kiwango cha testosterone huongezeka kwa asilimia 17 mpaka 19 ndani ya week.
3.      NAZI
Mwili unahitaji mafuta mazuri ili kuengeneza kichocheo nyingi, ikiwemo kichocheo cha testosterone. Nazi na aina zingine za nuts kama karanga zinasaidia mwili kutengeneza mafuta mazuri ambayo yanahitajika na mwili, pia mafuta yanayopatikana kwenye nazi husaidia mwili kuwa na uzito mzuri na pia kupunguza mafuta mabaya yasiyohitajika na mwili na hivyo utagundua kuwa kurekebishwa kwa uzito wa mwili basi kunasaidia uzalishaji wa kichocheo cha kiume na utakubaliana nami kuwa uzito mkubwa ni chanzo cha tatzo la upungufu wa nguvu za kiume kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa kichocheo cha kiume.
4.      MBOGA ZA MAJANI
Mboga za broccoli na cauliflower zinasaidia mwili wa binadamu kutoa kiwango cha kichocheo cha estrogen kilichozidi ndani ya mwili na hivyo kuongeza kiwango cha testosterone ndani ya seli
5.      PROTINI ITOKANAYO NA MAZIWA
Protini hii ambayo hupatikana kwenye sehem ya maji ya maziwa inazuia mwili kutengeneza kias kikukwa cha kichocheo cha cortisol na hivyo kuongeza uzalishwaji  na ufanyaji kazi wa wa kichocheo cha  Testosterone, hapa ielewele kwamba kichocheo hizi mbili huwa zinapishana moja ikiwa nyingi kwenye damu basi ingine huwepo kwa kias kidogo kwenye damu.

DALILI ZIFUATAZO ZINAONESHA KWAMBA UNA UPUNGUFU WA KIWANGO CHA TESTOSTERONE
·         Mwili kukosa nguvu mara kwa mara
·         Upungufu wa nguvu za kiume
·         Kupungua kwa hamasa ya tendo la ndoa
·         Kuongezeka uzito kupita kiasi
·         Shinikizo la damu kupanda
·         Kupungua kwa uwezo wa misuli kufanya kazi
NJIA ZIFUATAZO ZITASAIDIA KUONGEZA KIWANGO CHA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE NDANI YA MWILI NA KUEPUSHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
1.      MAZOEZI YA MWILI
Kupunguza uzito usiohitajika na mwili ni njia mojawapo asilia ya kuongeza kiwango cha kichocheo cha kiume.
2.      PUNGUZA KIWANGO CHA MSONGO WA MAWAZO
Mwili Unapokuwa na msongo wa mawazo basi hupelekea uzalishaji kwa wingi wa homoni iitwayo cortsol ili kupamban na hali hiyo, lakini uoande wa pili ni kwamba kiwango kikubwa cha cortsol kwenye damu hupelekea ufanyaji kazi ya homoni ya kiume yaani testosterone kupungua
3.      PUNGUZA MATUMIZI MAKUBWA YA VYAKULA VYENYE SUKARI NA WANGA
Matumizi makubwa ya vyakula vyenye wanga na sukari hupelekea mwili kutengezeza kiwango kikubwa cha homoni ya insuini ili kubadilisha kiwango hcho cha sukari na kukihifadhi kama mafuta, hivo mpenzi msomaji tambua kwamba kadiri unakula wanga na sukari nyingi ndipo kias kikubwa cha insulini kinavomwagwa kwenye damu na ndivyo ufanini na utolewaji wa homoni ya kiume unavopungua.
 TEZI DUME NI NINI?? Na UHUSIANO ULIOPO KATI YA TEZI DUME NA UZALISHAJI WA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE
TEZI DUME NI NINI
Hii ni tezi (kokwa) ambayo inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa ni kutengeneza maji maji ya uzazi kwa mwanaume(shahawa) ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizotengenezwa kutoka kwenye korodani na husaidia kusafirisha mbegu za kiume na kuzifanya zibaki hai kwa muda unaostahili. Kikawaida wanawake wana kiwango kidogo sana cha kichocheo cha testosterone kwa maisha yao yote
Tezi hii huwa inaongezeka uzito au ukubwa kadri umri wako unavyozidi kukua. Na nimekwambia kuwa tezi hii ipo katika shingo ya kibofu cha mkojo na hivyo basi ukuaji wake unaweza kuathiri mfumo mzima wa utoaji mkojo kwenye kibofu(Incomplete bladder emptying) .
Tafiti zinaonesha kwamba tezi huanza kuongezeka uzito kuanzia miaka 25, na huendelea kukua kila siku kadri umri unavyo enda. Kuongezeka kwa uzito wa tezi yako ya kiume sio tatizo kimatibabu kwani kipimo cha kuonesha moja kwa moja umefikia hatua sio nzuri ni pale unapoanza kupata dalili zenye kuzuia mkojo kutotoka vizuri (obstructive symptoms). Hivyo uzuri ni kwamba kuanzia pale tezi inapokuwa inaongezeka ukubwa hadi kufikia kuonesha dalili mbaya ni hadi unapofikia angalau umri wa miaka 60 na kuendelea , pia inaweza hata ikatokea hata unapokuwa una umri chini ya miaka 50 inategemea na mwili wako kibaolojia. Basi kukua huku kwa tezi bila sababu ya msingi tunaweza tukawa na hitimisho la magonjwa makuu mawili au matatu,Kwanza Benign Prostate Hypertrophy (BPH) aka Kukua kwa tezi dume, pili Prostate cancer Hii ni kansa ya tezi dume na Tatu Uvimbe kwenye kibofu cha mkojo.
Tafiti zinasema kwamba tatzo la Tezi dume linaweza kuziwa kutokea kwa njia za nje, yaani namnisha kwa kutumia ama kula vyakula fulani fulani, kiwango kikubwa cha kiini lishe kiitwacho lycopene husaidia kuondoa uwezekano wa mtu kuugua tezi dume. Lycopene hupatina akwenye matunda yanya. Hapa mpenzi msomaji unaweza kujiuliza kama tunatumia nyanya kila siku kwenye mboga je iweje tuugue tatizo la tezi dume?? Jibu ni kwamba hapana kwa sababu kiasi kidogo sana  cha lycopene hufonzwa na mwili kutoka kwenye matunda ya nyanya tunayokula hivo inahitaji ule mamia ya nyanya kila siku ili kufidia hilo gepu la kiasi chote kinachotakiwa.
HITIMISHO
Mpenzi msomaji baada ya kuona kuwa Testerone ndio kichocheo kinachomfanya mtu awe mwanamme, yaani kuweza kufanya majukumu ya kimwili kama mwanamme, ni wazi kuwa utakubaliana nami kwamba  upunguvu wa kichocheo hiki moja kwa moja kunapelekea TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME ambalo linasumbua watu wengi sana kwa sasa.
 LAKINI KAMA TAYARI UMESHAPATA TATZO LA KUKUA KWA TEZI DUME AMA UNA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME BASI TUMEFANIKIWA KUTENGENEZA KIRUTUBISHO CHENYE KIWANGO KIKUBWA CHA LYCOPENE, kitasaidia kupenya ndani ya tezi dume, kuua bacteria na pia kukarabati sehem zilizoathiriwa na bacteria na hivyo kuzuia kutokea kwa saratani ya tezi dume.