Friday, December 1, 2017

Haya ndio makosa makubwa wanayofanya wachumba kabla ya kuingia kwenye NDOA au Kabla ya KUOANA


Bila ya shaka kwa rehema za muumba sote tu wazima wa afya....na wale ambao afya zao zina mtikisiko Mungu bwana wa majeshi yupo upande wenu katika kipindi hiko kigumu......

Kwa kawaida kila mwanadamu anapenda na kutamani kuwa na furaha wakati wote wa maisha yake......na hakuna kati yetu asiyejua kuwa ni furaha iliyoje kufunga ndoa na kuishi na mtu ambaye huba zenu zimeshibana......hii inawafanya wapendanao wajihisi kama wapo paradiso.......

Lakini kinyume na matarajio ya wengi.....furaha zao na raha zao zinapotea mara tu baada ya kuingia kwenye maisha ya NDOA na wale ambao walidhani ni chag


uo la nyoyo zao......

Mara nyingi mioyo yetu inapoangukia penzini akili zetu huzidiwa akili na mahaba hata kushindwa kuyaona makosa au kuyapuuzia makosa ambayo kwa wakati huo yanaonekana sio kikwazo....lakini baadae huonekana kuwa ni mwiba mkali kwenye NDOA yenu takatifu....na mtu kuishi maisha ya ndoa kama yupo gerezani......

Yapo mengi lakini yafuatayo ndio makubwa zaidi ambayo yamebomoa ndoa nyingi sana na zingine zinapumulia mashine....

>Kukaa kwenye uchumba kwa muda mrefu..
Kuwa wachumba kwa kipindi fulani ni jambo zuri kwani ni kipindi ambacho watarajiwa mnapata kujuana kiundani zaidi na hatimaye kufanya maamuzi sahihi ya kuingia kwenye ndoa....lakini kipindi cha uchumba kinapokuwa kirefu sana.....kinapunguza afya na uhai wa ndoa.....kwani mnajikuta mnazoeana sana kabla ya kuhalalishwa kuishi na hata mkiingia kwenye ndoa mnakuwa kwenye hali kuwa bored kwa ni mtu yule yule mliyekuwa naye kwenye uchumba kwa miaka zaidi ya mitano.....

>Kuonjana onjana wakati wa uchumba
Kwa kawaida kila mwanadamu anakuwa na msisimko na kitu kipya.....kitu ambacho hana dhana nacho.....kitu ambacho hana jibu lake kamili......
Lakini kwa wachumba kwa kadri mnavyofunuana ndivyo inavyopungua hamu ya kufunga ndoa.....kwani maisha ya ndoa yanakuwa hayana msisimko na shauku....kwani mambo yote ya wanandoa mmeshayafanya mkiwa wachumba.....hivyo kupelekea ndoa kukosa afya na hatimaye kuyumba kama sio kuvunjika kabisa.......

>Kudhani kuwa utambadilisha mkeo/mumeo mtarajiwa........

Wakati wa uchumba ni wakati wa kupimana kwenye mizani ya kuishi kwenye maisha ya ndoa.....unatakiwa mpaka unaingia kwenye ndoa una jibu kamili na umefanya maamuzi sahihi......

Wengi wetu kwenye uchumba tunakutana na tabia au viashiria vya tabia ambavyo kwa namna moja au nyingine hatupendezwi navyo.....kwa mfano
~ Ulevi
~ Kutokuwa muaminifu
~ Uongo
~ Uchafu nk.
Lakini kwa kuelemewa na pendo na shauku ya ndoa tunajikuta tunazipuuzia na hatimaye tunajikuta tupo vifungoni kwenye ndoa ambayo tulitegemea kupata furaha....kwani kuna baadhi ya tabia ni ngumu mtu kumbadilisha kwa hiyo ni vyema kufanya maamuzi magumu wakati wa uchumba kama unaona wazi kuwa tabia ya mwenzio inakunyima raha na amani kwenye mahusiano yako.......

>Tofauti za kiimani
Kuingia kwenye ndoa mkiwa na imani tofauti kwa mwanzo inaweza isionekana kuwa ni tatizo lakini kwenye maisha marefu ya ndoa hilo ni tatizo kubwa sana.....kwani wanandoa ni kama mwili mmoja na hivyo kuishi miaka mingi ya ndoa kunatakiwa kuwe na vitu vingi vinawaunganisha.....sasa kama kuna vitu vingi vinawatenganisha hasa jambo zito kama la imani....basi hapo ndoa ipo mashakani

Chukulia picha ni raha iliyoje wewe na familia yako mkijiandaa jumapili moja tulivu kwenye kanisani....
Chukulia picha ni raha iliyoje wewe na mkeo kipenzi mkiwa na watoto wenu kwa pamoja mkijadili vifungu vya biblia kwa furaha....

Chukulia picha wewe na familia yako mkiwa na sehemu yenu ya kuswali kwenye nyumba yenu na nyote mkajumuika kwa pamoja kwenye sala....!!!

Chukulia picha wewe na familia yako mkifungua madrasa ya familia mkifunza qoran tukufu na wapendwa wako.....!!

Hakika ni matukio yenye kupendeza.....na kugusa moyo.....

Lakini sio kila ikifika siku ya kuabudu kila mmoja anashika njia yake utadhani ni wapangaji......




Nimalizie kwa kusema kuwa nawatakieni siku njema na yenye baraka tele....na Mungu awasimamie katika lenye kheri na nyie....na awaepushie kila lenye shari na nyie......

Amen.....