Tuesday, December 26, 2017

About Love; Siku ya Kwanza Kunywa Kiroba Ndio Siku Safari ya Mapenzi Hadi Ndoa ilianza..Soma Kisa Kizima Hapa

Safari yangu ya ndoa ilianza kwa namna yake! nikiwa mitaa fulani ya kijitonyama' baada ya kuhitimu na kuamua kuacha kazi ili nijikite kwenye ujasiriamali nilikutana na ukata ambao sikuwahi kufikilia kama ungewahi nitokea' hata hivyo mtembea bure si sawa na mkaa bure' maana mkate ulikuwa unapatikana!!

Nilikuwa na kibanda cha huduma fulani pembezoni mwa barabara' hivyo watu wakishuka mitaa ya sayansi walikuwa wanapita usoni mwa banda langu lakutafutia liziki kwenye ile barabara yakuelekea Kwa Ally Maua(watu wa k'nyama wananielewa vizuri hapa) 


Kumbe kati ya wale wapita njia ambao huwa nawaona asubuhi na jioni wakiwa wanaenda na kutoka maofisini moja wao ni ubavu wangu lakini kwa hali yakawaida ilikuwa fumbo zito kwangu. Mara mojamoja ilinipa wakati mgumu hasa pale nilipokuwa naona wapendanao wakiwa wanasindikizana na wamependezana'' kilichokuwa kinaniumiza ni maswali mengi niliyokuwa nayo kichwani yasiyokuwa na majibu' lini mambo yangu yatanyoka? Lini takuwa na mtu ambaye tutamatch tukiongozana mtaani watu watutolee macho? Lini takuwa na familia yangu?

Jioni moja nikiwa na jamaa yangu
Kwenye mgahawa karibu na akachube road' baada ya msosi si tukaagiza safari ili kukata kiu' nikahisi kama vile haitoshi na mfukoni nimebaki na buku, kwakujitutumia mhudum lete kiroba' nikachanganya kiroba na safari!! Bwana kilichofuatia..

Wakapita wadada wawili walipendeza sana lakini sura ya mmoja wao ilikuwa imezoeleka machoni kwangu' kwakuwa kiroba kilikuwa kimeanza kazi nikashindwa kukumbuka kwaharaka (kumbe alikuwa ni mmoja kati ya wale ambao huwa wanapita mbele ya kibanda changu na sometimes huwa anakuja kupata huduma kibandani kwangu). Ila mara nyingi huwa anavaa earfone na anakuwa anaongea na sim mda wote akipita' na leo yupo casual tofauti na muonekano niliozoea kumuona!!

Basi bwana kiroba kikiwa kimechanganya dada si akapita karibu yetu'
Mimi; dada karibu
Dada; Asante
Mimi; agiza moja
Dada; Asante' situmii!!
Nikadakia ina maana niharam kwako? Dada akamuita mwenzake fanya haraka tuondoke'
Mimi' dada acha dharau mim nakukaribisha wewe ndo kwanza kama vile huniskii!
Dada; samahani kaka yaishe!

Basi akili ya kiroba ikaanza kazi' mimi; unajifanya jeuri sio' takuonyesha leo! Nikamkunja dada wawatu kichapo kichapo' mamwela sijui walitokea wapi wakakuta dada anachezea kichapo wakanianzishia sikufanya ajizi nikamdaka alikua na kihelehele chakushuka kwenye gari nikampa kichapo akaangukia mtaroni' bwana wee kama nilichokoza nyuki nilishambuliwa nawale jamaa na virungu' na sikujielewa kuja kutahamaki nipo mabatini kwenye kasero kadoogo! 


Nisijue kumbe nilimsababishia jeraha yule dada' baadae nikayaweka sawa pale kituoni na nikatakiwa kulipa gharama za matibabu! Basi nikaenda kumuona yule dada na kumuomba msamaha' nashukuru nilikuta anaendelea vizuri' ikanibidi niulize gharama za matibabu ingawa nilikuwa sina chochote mfukoni' dada akaniambia atagharamia mwenyewe! Nikajifanya kumbembeleza pale kumbe moyoni nashukuru kwelikweli maana navyowajua wale jamaa dada angekomaa alipwe nao wangeongeza chao!

Mazoea yakaanza' kati yangu na yule dada katika kipindi ambacho alikuwa anauguliwa maana ikanibidi niwe mtu wa matunda juice juice kuonyesha kwamba kilichotokea sio hulka yangu ilikuwa bahati mbaya tu na ndio ukweli!! Lakini kwakipindi hicho nilijifunza kitu kwake na akaendelea kunivutia zaidi na zaidi lililokuwa kubwa zaidi sikuwahi kukutana na mtu ambaye ningehisi au kutambulishwa kama shemeji(yaani mpenzi wake) kila nilipokuwa nikienda kumuona!!

Siku zikasogea, miezi ikaenda, mwaka ukakatika!! Nikagundua kwamba Ana sifa zote na vigezo vyakuwekwa ndani... Issue ikawa taanzaje kumueleza hisia zangu juu ya hilo!! Nikajipa moyo mimi mtoto wa kiume woga wangu waweza kuwa umaskini wangu nikajitutumua' bwana wee ikawa kama nimetaka kuvunja urafiki!!
Basi nikajituma mwanaume miezi ikakatika' akaanza kuniekewa taratibu tukawa wapenzi' siku zikaenda mara nikatangaza ndoa! Hatimaye sasa nimama wa mtoto mmoja na nampenda sana na sijawahi jutia kuwa naye!!

Yote kwayote tunapaswa kujua mambo mengine yanatokea kwasababu fulani! Mimi sio mlevi na wala sikuwa mnywaji au mtumiaji wa pombe lakini siku hiyo nilikunywa safari tena nikaongeza na kiroba kumbe ulikuwa ndo mwanzo wa safari yangu ya ndoa!! Siisahau siku hiyo maana ndo ilikuwa siku yangu ya kwanza na mwisho yakutumia pombe lakini pia ndo ilikuwa mwanzo wa mahusiano hatimaye mke!!

Hivyo ndio namna safari yangu ya ndoa ilivyoanza' wewe ulie kwenye mapenzi ilikuwaje paka umefika hapo ulipo? Nawewe uliye kwenye ndoa safari yako ilikuwaje?