Thursday, December 28, 2017

About Love; Fahamu kuwa mwanamke wa kumuoa hana sifa za kuwa mpenzi..Check Out

Jumanne ya leo Mungu ameniwezesha kuwafikia tena, ninakuja na mada nzuri sana. Kwamba, Mwanamke wa Kumuoa Hana Sifa za Kuwa Mpenzi.Wengi wanaweza kupingana na huu utafiti wangu lakini nawaomba wasome mada hii mwanzo hadi mwisho ili wajue nina maana gani au nimeshika vigezo gani!

UTAFITI WA KAWAIDA
Nilibahatika kufanya utafiti wa kina kupitia kwa wazee, wakiwemo mababu ambao walinipa maelezo mazuri sana na nikakubaliana nao.Ukweli ni kwamba, wanaume wengi huwa hawapendi kuoa wanawake wazuri sana! wanasema si waaminifu, wanatongozwa na wengi, wako wanaume hutumia gharama zozote kuwapata na mambo kemkem kama hayo.

Baadhi ya tafiti zinasema wanawake wa kundi hili sifa yao kubwa ni kuwa wapenzi lakini si kufikia hatua ya kuweka ndani kama mke. Wanaume wanakiri kwamba, kumpata mwanamke mzuri kama mpenzi hakumpi kujiamini kwamba yuko peke yake katika uhusiano, wengi wanajua wako kibao, lakini anaendelea kuwa naye kwa sababu siku akimtaka kutoka naye anampata. Hiyo ndiyo sifa ya mwanamke anayefaa kuwa mpenzi.

Wanaume wanaendelea kusema mwanamke anayefaa kuwa mpenzi ni yule ambaye akivaa hupendeza, huvutia, kila nguo inamkubali, ana sura nzuri, lakini macho ya kimapepe, akili zao kila wakati ni kuchuna mabuzi na kupewa mtoko.

Lakini wanaume wanakiri kwamba, wanawake wa kundi hili wakiingia nao kwenye kundi la watu kama baa au ukumbini, macho ya watu humkodolea yeye kutokana na uzuri wake wenye mvuto.

WANAWAKE KATIKA MAKUNDI
Wazee au mababu wanasema wanawake wapo katika makundi matatu, wazuri sanaaa, ndiyo hao ambao wanaume wengi wanawakwepa kuwaoa! Wazuri wa wastani na wabaya!

WAZURI SANAA!
Kundi la wanawake wazuri sana ndilo linalotingisha ndoa au kutotulia kwenye ndoa. Hapo ukiachia mbali tabia ya mwanamke mwenyewe.

Wanawake wazuri wanajijua, kwa kuambiwa na wengine, kusifiwa na wanaume, kujiona kwenye kioo cha katika picha hivyo wengi wao hupoteza sifa ya kuwa mke kwa sababu, wanaume husema wanakodolewa macho na kila mtu! (wanaume wakware).

Mara nyingi wanawake wa kundi hili ikitokea wakaolewa, huwa wagumu kutii sheria za ndoa au maagizo ya mume ndani ya nyumba kwa sababu wanajua hata wakimwagwa, watapata wanaume wengine kwa vile wanatongozwa sana.

Pia, wengi huwa malaya! Yaani ana ndoa lakini nje bado anataka kwa kuwa kila mara anatongozwa na wanaume kwa sababu ya mvuto wake na kujikuta wakiangukia kwenye vishawishi.

WAZURI WA WASTANI
Kundi la wanawake wazuri wa wastani, mababu ndilo wanalolitaja kuwa lina wake wengi, yaani mwanamke mwenye sifa ya kuolewa anapatikana humo! Wanawake wa kundi hili hata wenyewe wanajijua kwamba, uzuri wao ni wastani, si tishio mtaani  hivyo huwa wanaishi maisha ya kawaida. Mara nyingi wanawake wa kundi hili hawapati usumbufu wa kivile njiani kutoka kwa wanaume wakware na wanaume wengi huangukia kwao kwa ajili ya ndoa.

WABAYA!
Si kama nakandia lakini kusema ule ukweli wapo wanawake wabaya! Wabaya kwa sura, maumbo hata mwendo achilia mbali mambo mengine. Utakuta mwanamke ana umbo linaitwa sanamu ya michelini, nyusi alivyozitinda na kupaka rangi, we acha tu! Halafu jioni akitoka, anavaa suruali ya kubana huku akijijua ana kitambi hichoo, matiti yaleee!

Lakini utafiti unaonesha kwamba, mabadiliko ya maumbile ya kundi la wanawake hawa husababishwa na malezi ya asili, mlo, maisha na kujiachia.

WAPO HAWA
Pamoja na maelezo yote hayo bado nakubaliana kwamba, wapo wanawake ambao ni wahuni bila kujali daraja la uzuri. Hapa namaanisha kwamba, wapo wanawake wazuri sana na wametulia, wapo wazuri wa wastani ni mcharuko na wapo wabaya na ni wachepukaji balaa!
Jiangalie wewe upo kwenye kundi gani kisha badilika!