Thursday, December 28, 2017

About Love # Fahamu kuhusiana na Ngono ya mdomo na inavyoweza kusababisha Saratani ya Mdomo na Koo.

Ngono ya mdomo maarufu kwa kiingereza kama oral sex imekuwa ikiongezeka kwa kasi hasa kati ya vijana. Aina hii ya ngono hujumuisha kunyonya/kulamba sehemu za siri za mwanaume au mwanamke kwa lengo la kumridhisha kimapenzi. Pamoja na uzuri au umaarufu wake ngono ya mdomo huleta hatari ya kupata magonjwa kama ilivyo ngono za ukeni/kinyume na maumbile.

Tafiti zilizofanya hapa nchini na sehemu mbalimbali duniani zinaonesha kuwa ngono ya mdomo huongeza hatari ya mtu kupata saratani ya mdomo na koo, hasa kwa wanaume. Taasisi ya Saratani ya Ocean Road katika tafiti zake imeonesha asilimia 20% ya wagonjwa wa saratani ya mdomo na koo imechangiwa na ufanyaji wa ngono ya mdomo.

Saratani ya Mdomo na Koo Ni Nini?

Saratani ya mdomo na koo ni aina ya mabadiliko ya seli ambazo hukua bila kudhibitiwa na mwili. Huathiri sehemu za mdomo, koo, kisanduku cha sauti na mrija wa chakula.

Ngono ya Mdomo na Saratani ya Mdomo na Koo

Licha ya kuwa na visababishi vingine, tafiti zimeonesha kuwa ngono ya mdomo huchangia kutokea kwa saratani ya mdomo au koo.


Je, ni nini katika ngono ya mdomo husababisha hili?

Maambukizi ya virusi viitwavyo Human Papilloma Virus (HPV), ambavyo pia husababisha saratani ya shingo ya uzazi (cervical cancer), husababisha kutokea kwa saratani hii.

Maambukizi ya virusi hivi vya HPV hutokea kutokana na kufanya ngono zembe. Maambukizi haya huweza kuleta dalili na kusababisha ugonjwa wa zinaa uitwao genital warts, na kwa wengine usilete dalili kabisa lakini virusi vikaendelea kuishi kwenye sehemu zao za siri na kuambukiza wengine kwa ngono.

Virusi hivi hukaa kwenye majimaji ya uke kwa na shahawa, na hivyo katika ngono ya mdomo mtu hupata virusi hivyo ambavyo huenda kushambulia utando wa seli za mdomo au koo na hivyo kuweza kusababisha saratani kutokea baada ya miaka kadhaa. Ni asilimia ndogo  ya watu wenye maambukizi ya virusi vya HPV mdomoni au kooni kutokana na ngono za mdomo hupata saratani kutokana na virusi hivyo. Uwezekano wa saratani kutokea huongezeka zaidi pale mtu anapokuwa na tabia hatarishi nyingine kama kuvuta sigara au unywaji wa pombe kali.

Pia, tafiti zinaonesha kuwa virusi hivi huwa kwa wingi  kwenye majimaji ya uke ukilinganisha na shahawa, na hivyo kuna hatari zaidi kwa wanaume kupata saratani ya mdomo au koo kutokana na kufanya ngono ya mdomo kwa wapenzi wao.

Tabia zifuatazo katika ngono ya mdomo huongeza hatari ya kupata saratani ya mdomo:

Kufanya ngono za mdomo na watu 4 au zaidi maishani mwako.


  • Kuanza ngono katika umri mdogo (chini ya miaka 18).
  • Athari Nyingine za Ngono ya Mdomo.

Ngono ya mdomo inaweza kusababisha  kuambukiza magonjwa ya zinaa kama kaswende, kisonono, klamidia na herpes. Maambukizi haya hasa hutoka sehemu za siri kwenda kwenye mdomo na koo.

Je, naweza kufanya ngono ya mdomo salama?

Ndio inawezekana. Na hii hasa ni pale ambapo hamna maambukizi ya virusi vya HPV wewe na mpenzi wako. Hatari ya kupata virusi hivi huongezeka kama mtu ana idadi kubwa ya wapenzi au amewahi kuwa na wapenzi wengi maishani mwake.

Njia nyingine ni;


  • Kutumia kondomu ya kiume wakati wa kufanya ngono ya mdomo.
  • Kutumia dam (aina fulani ya plastiki laini ambayo hufunika sehemu za siri za mwanamke kuzuia maambukizi) wakati wa kufanya ngono ya mdomo.