Tuesday, November 14, 2017

Wakati Mwingine Wanawake Wanataka Kupigwa, Mume Wako Si Shoga Yako

Unakumbuka yule rafiki yako ambaye mkigombana au mkitofautiana kidogo utaongea au yeye ataongea mpaka basi. Kitu hakitaisha na mtakumbushiana mambo yazamani ambayo mliwahi kukoseana mpaka basi. Mtatukanana au mtakuwa mkisutana kwa mafumbo na maneno ya kejeli.
Mtatukanana weee mpaka mtakapoagana na kila mmoja kwenda kwake na kesho yake mkakutana tena mkiwa mmenuniana na kama hamkuyamaliza vizuri basi mkaendelea na ugomvi. Huyo ni rafiki yako, acha kufanya hivyo kwa mume wako rafiki yako anaweza kuvumilia maneno yako lakini mumeo hawezi.
Wanawake wengi hupenda kelele, akishikilia mada moja basi utatamani kuhama hata nyumba, ataongea, atanuna atasuta na atazodoa hata akiombwa msamaha kitu hakitaisha. Hakuna mwanaume ambaye anapenda mambo ya namna hiyo, narudia hakuna mwanaume ambaye anapenda kelele za namna hiyo.
Yaani katoka kazini kazinguliwa na bosi wake na wewe unakuja kumpigia kelele usiku mzima eti kisa kasahau kuwa shoga yako anaolewa na alitakiwa kupitia gauni lako kwa fundi! Kila saa unamkumbusha kuhusu kitu kile kile na kulalamika kuhusu kitu kile kile. Amekuambia kuwa kashakuelewa na atajirekebisha bado unakumbushia na hutaki yaishe.
Hapo kuna mawili, atatoka kukwepa kelele zako au  atakutandika makofi ili ulie na yeye alale kwa amani. Mwanamke unatakiwa kumjua mume wako, kujua ni wakati gani ulete mdomo na wakati gani unayamaze. Usilazimishie kupigwa kwani tofauti na rafiki yako ambaye mtajibishana na kusutana kwa midomo mumeo atakusuta na kukujibu kwa makofi.
Akishakuambia basi yameisha hembu yaishe kweli na si kuendeleza mambo yalayale. Kumuongelesha kama mtoto mdogo, kumkumbusha kitu kilekile kila wakati kana kwamba hajielewi kukumbuka. Unapaswa utambue kuwa kelele zako hazitaishia katika kumfanya akutandike makofi tu bali pia zitamlazimisha hata kutoka nnje kutafuta amani.
Sio kwamba usilalamike kabisa, kwa afya ya ndoa yako mwanamke anapaswa kulalamika na kununa, kuongea sana na kulia. Hii ndiyo namna ambavyo wanawake hutoa hasira na sumu ndani ya miili yao. Wanawake ambao hawalalamiki na kulia wanapokasirika huumia zaidi na kujaza sumu katika miili yao.

Lakini hii isikufanye kulalamika mpaka kero, jaribu kujizuia na kuangalia mood ya mwenza wako. Sio anakuambia mambo ya msingi yaliyotolkea kazini wewe bado unalalmika kuhusu mchango wa Kitchen party ya rafiki yako ambaye hata harusi yenu hakuhudhuria. Kosoa kw akiwango, ongea kwa kiwango, lalamika kwa kiwango, usimsute kabisa mumeo.