Sunday, November 19, 2017

VILIVYOKULETA NDANI YA PENZI SASA VINAKUTOA NJE



Katika mahusiano yawezekana kabisa vile vitu au kile kilichokuvutia kumkubali mpenzi wako na kuamua kuwa naye maishani baada ya muda fulani wa maisha ya pamoja kitu hicho au vitu hivyo vikawa kikwazo cha kukushinikiza kutamani kutoka nje ya ndoa hiyo, kwa mfano, ulipenda kumwona anavyo kupenda na kila saa akitaka kujua aliko, unafanya nini, nanani, wewe ukadhani hayo yalikuwa mapenzi, ukashindwa kujua kuwa huo ulikuwa wivu wa kawaida tu na sasa wivu huo umezidi, umekomaa, umeota mizizi na umekufanya unashindwa kustahimili kwa jinsi anavyo kubana pumzi kama kiranja wa shule ya msingi na unatamani kuachana naye. Mfano wa pili, pesa nyingi alizokuwa anakupa kabla hamjaoana, ulizifurahia sana na kuona kuwa umefikia mwisho wa matatizo yako, wewe ulitafsiri kuwa hilo ndilo penzi na huyo ndiyo mwanaume anayejali, sasa pesa hizo zimeongezeka, badala ya furaha nayo kuongezeka kwenye mahusiano yenu,  kila siku unakerwa na kiburi chake cha pesa, siku hizi anahonga wanawake kama alivyokuhonga wewe miaka hiyo. Sasa hapa unaona wazi ya kuwa ulichokipenda na kikakuvutia kuingia ndani ya penzi sasa kitu kile kile kinakushinikiza kutoka nje. Jifunze kuwa macho na makini sana katika vile vinavyokuvutia kuingia kwenye mahusiano ili kupunguza majuto mengi ya kesho. Usisahau, “what goes around, comes around”