Sunday, November 19, 2017

Dalili Kuwa Mpenzi Wako Ameanza Kukuchoka Na Anakaribia Kukuacha

Katika mapenzi suala la kuchokana ni jambo la kawaida na inapofikia wakati mwenza wako akaanza kukuchoka ni vyema ukajua ni dalili gani ili  muweze kurekebishana mapema kabla penzi halijavunjika. Watu wengi hujisahau na kusubiri mpaka mambo yanapoharibika ndiyo hujaribu kusuluhisha na wanakuwa wameshachelewa. Ingawa zipo dalili nyingi lakini kwa leo nimeamua kuchambua dalili hizi 12 kwaajili yako rafiki yangu wa nguvu.

{1} Hapokei simu zako, anachelewa kujibu meseji; Katika ulimwengu huu wa teknolojia naamini hii ndiyo dalili kubwa ya mtu kuanza kumchoka mtu. Utakuta unampigia simu mara tatu kwa siku lakini hapokei na jioni anakupigia huku akijifanya alikuwa bize. Kuna ambao ni kawaida yao kufanya hivyo lakini kama zamani hakuwa hivyo, alikuwa akipokea au kukupigia kutwa mara tatu, jua ushaanza kukuchoka.
Lakini pia unaona anachelewa sana kujibu meseji zako kuliko kawaida yake au hajibu kabisa na ukimuuliza anakuwa na sababu zisizoeleweka kama vile sikuiona, nilikuwa bize, au sikuwa online wakati ulimuona online au kwenye magroup anachangia kama kawa. Wakati mwingine anaweza kweli kuwa alikua bize au hakuziona meseji zako lakini kama anafanya hivyo kila siku jua kuwa ameanza kukuchoka.
{2} Hataki muda wa nyie wawili tu; Mlishazoea kutoka mara kwamara wawili, mlishazoea kufanya mambo kwa pamoja lakini ghafla yuko bize, hataki kuwa tena karibu na wewe na kila mara anakuwa na visingizio. Mkipata kamuda ka wawili pamoja nnje ya kitandani atakuwa bize na simu yake na unaona kama uko peke yako, atatafuta sababu tu ya kuondoka. Ukiona hizo dalili basi jitathimini angalia kuna kitu hakiko sawa.
{3} Anakukatisha kila mara unapoongea na kukukosoa kidharau; Ndiyo unakuta kila mkiwa na marafiki zenu ukiongea kabla hujamaliza anatafuta kakitu ka kukukosoa na kukuzodoa, tena ile kwa dharau kana kwamba hujui chochote. Atawaunga mkono wengine lakini si wewe, anajaribu kukushusha mbele ya marafiki zake na marafiki zako na wakati mwingine hataki uongee kabisa, anatamani usiwepo mnapokuwa na marafiki wenu.
{4} Anakosoa kila kitu unachomfanyia; Yaani katika kila kitu unachomfanyia atajaribu kutafuta kitu kidogo tu cha kukosoa ili tu ujisikie vibaya. Ukimfanyia kitu cha upendo anakipokea kwa shingo upande na atakiangalia na  miwsho atakitoa kasoro, hata kama ni kitu ambacho awali alikuwa akikipenda kwa dhati na kukifurahia hakifurahii tena. Atakosoa kitu hicho na kukosoa kwake hakuishi, unaweza kumpa zawadi akaikosoa na kuiacha mpaka ikaharibika bila kuitumia.
{5} Anakumbushia makosa ya zamani; Kuna makosa ambayo alishakusamehe na mlishasahau lakini ghafla umefanya kitu leo utamsikia. “Hii ndiyo kawaida yako, unakumbuka mwaka juzi tukiwa chuo, ulifanya hivi hivi?” Anaweza kununa au kama mlikuwa sehemu kuondoka kabisa kwakuwa tu amekumbuka kitu ambacho ulimfanyia miaka kumi iliyopita.
{6} Kitandani ni kazi tu, hakuna ‘Romance’ wala baba yake kushikana; Zamani mpaka mnaanza mechi mlikuwa maingia bafuni pamoja, sijui manjonjo yote lakini sasa hivi ni kama adhabu au mko jeshini ni kazi tu na mkishamaliza anaweza kukuambia ondoka niko kesho natakiw akuwahi kazini au kama yuko kwako akaondoka bila mazungumzo wakati mwingine hata kuoga hataki, inakuwa kama mnalazimishana.
{7} Anawasifia watu wa jinsia tofauti mbele yako kama vile haupo; Yaani mko tu kapita mwanamke mzuri anasifia tena anasifia kitu ambacho anajua kabisa huna na anajua itakukera, kapita mwanaume anasifia bila kujali hisia zako. Mwanzoni hakuwa hivyo alikuwa makini kulinda hisia zako lakini sasa wala hajali. Anaweza hata kuwaisfia marafiki zako mbele yako na wakati mwingine kuulizia kuwa wanaendeleaje hata kabla ya kukuuliza unaendeleaje.
{8} Anataja mtu wa ndoto zake ambaye si wewe; Utasikia napenda nioe mwanamke mweupe wakati wewe ni mweusi au anasema anataka mfupi wakati wewe mrefu, yaani kila anachoongea ni kinyume nyume  na wewe ulivyo. Mbaya zaidi hakuongelei kwenye mipango yake ya baadaye, haongelei kitu anachokipenda kutoka kwako, bali anachopenda kutoka kwa wengine.
{9} Haonyeshi kuvutiwa tena na wewe; mwanzoni hata kabla ya kuvua nguo alikuwa shapagawa anakuvamia na mnaanza kuvuana, ila sasa umevua nguo uko mbele yako wala hastuki ndiyo kwanza yuko na simu anajibu meseji, mpaka umshike na kumvutia kitandani ndiyo anastuka. Unamhitaji na uko sexy balaa lakini utamsikia subiri kwanza nimalizie kuangalia mpira au hii tamthilia, jua kuna kitu jiongeze.
{10}  Amefuta picha zako katika mitando ya kijamii; hapa ndipo ujue unakaribia kauchwa, alikuwa ameweka picha zako, na status za kimapenzi lakini taratibu anaanza kufuta, alikuwa anacomment kwanye kurasa zako lakini hafanyi tena, ukimtag anaondoa tag. Wakati mwingine anaweza kukuambia anajitoa kwenye mitandao ya kijamii lakini baada ya muda unakuta kaanzisha akaunti nyingine. Hapo alikuwa anaogopa kufuta picha zako hivyo kwa kuanzisha akaunti mpya hatakuwa na sababu ya kukupost.
{11} Anazungumzia sana kuhusu kuwa single na kuachana; Yaani utakuta hakuambii nakuacha lakini unakuta kila mara anzungumzia kuhusu kuachana, kuwa single, anasifia watu walio single kila mara, anaponda mapenzi, anajifanya kukata tamaa za kimapenzi na mambo kama hayo. Ukiona hivyo jua anataka kuachana na wewe lakini hajui ni namna gani ya kuachana.
{12}  Hakung’ang’anii tena; Awali ukimuambia uko bize msionane basi atakubembeleza mpaka utaona poteli ya mbali ngoja nikamuone hata kama ni kuongea tu. Sasa hivi hata kama ukisema uko bize kwa utani utasikia tu “Poa nitakucheki basi…” na baada ya hapo ndiyo nitolee hakuna cha kukucheki wala kuku cash, mpaka umtafute tena na yeye kujifanya yuko bize. Akikuambia nitakupigia au nitakutafuta baadaye ujue ndiyo imetoka hiyo mpaka umtafute wewe.
Hizi ni baadhi tu ya dalili, zipo nyingi kutegemeana na mtu, muhimu ni kumjua vizuri mwenza wako na kuangalia kama kuna mabadiliko yoyote. Hii inatokana na ukweli kuwa wakati mwingine mpenzi wako alikuwa hafanyi kabisa vitu nilivyo taja hapo juu hivyo akawa hajabadilika na ikawa ndiyo alivyo, lakini kama alikuwa akifanya na sasa amebadilika basi kuna umuhimu wa kujiangalia mapema, kuongea naye na kujua nini tatizo.